MADHARA NA HASARA ZA KUVAA WIGI AU NYWELE BANDIA.
uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususan wakina dada na wanawake wengi Wa kiafrika.
zifuatazo ni baadhi ya hasara au madhara kiroho na kiafya ya uvaaji wigi na usukaji wa nywele za bandia..
1.KUTENGWA NA MUNGU MILELE.
Ukifa katika hali bado unavaa mawigi na nywele bandia zote ni unakwenda Jehanam ya moto moja kwa moja kwa sababu umeshindwa kumheshimu Mungu.
2.UNAKUWA UNAABUDU MIUNGU BILA KUJUA.
Asili ya mawigi haya yanayotokana na nywele za wahindi, ni miungu inayoabudiwa huko na miungu hio inatolewa sadaka za nywele na hatimae mawigi yanatengenezwa,sasa unaevaa vitu vilivotolewa sadaka kwa sanamu moja kwa moja unashiriki ibada za miungu.
3.UNAPOTEZA MUDA NA FEDHA.
Wengi wanaovaa mawigi wanahitaji kuwa nayo mengi ili kubadilisha lakini pia wale wanayafumia kichwani kabisa ni gharama sana kufanya hivo.Okoa fedha zako acha kuwaa mawigi mwanamke.
4.MAUMIVU YA KICHWA.
kutokana na kuvalia mawigi wengi wanakuwa na maumivu ya kichwa kwa sababu ya kubanwa sana kichwani na mawigi.kichwa hakipumui wakati wote kimefunikwa na helmet yako(wigi lako)
5.KUPATA MBA NA HARUFU MBAYA.
Mba zinakuja kwa sababu ya kichwa kukosa hewa ya kutosha kitaalam inajulikana kama scalp hypixia ambayo inaweza kuleta harufu mbaya sana kama mba hizo zitachanganyikana na jasho.
6.UNAWEZA KUPATA MZIO(ALLERGY) NA KUNYONYOKA NYWELE.
wigi linakuwa na chemikali ambayo zinaweza kukusababishia madhara kwako kama hazitaoana na mwili wako. Na nywele pia zinaweza kuanza kunyonyoka na kichwa kuwasha sana.
Madhara hayo yote unaweza kuyapata wewe mwanamke unaeendelea kung'ang'ania mawigi yako ila mbaya zaidi ni Kutengwa na MUNGU Milele na kutupwa Jehanam ya Moto.
Mungu alikuumba,tayari aliona unapendeza na lazima tuishi katika viwango vya Adam na Hawa ambao Mungu alipowaumba akasema "na Tazama ni chema mbele zake", wanapendeza hivo hivo walivyo bila kuongeza makorokoro yoyote.
USIDANGANYIKE WIGI NI HATARI KWA MWILI NA ROHO YAKO. CHUKUA HATUA,UWE SALAMA.
#Jesus is #coming soon.
Na Isaiah Membe.
Barikiwa mtumishi wa,Mungu
ReplyDeleteBarikiwa mtumishi wa,Mungu
ReplyDelete