ASOMAE NA AFAHAMU;
Niliweka ujumbe katika post yangu iliopita kuhusu maandalizi ya ujenzi wa hekalu israel, lakini wamekuwepo watu ambao hawaelewi uhusiano uliopo kati ya ujenzi wa hilo hekalu na kunyakuliwa kwa kanisa.
Kwa faida ya wengine pia nitajaribu kueleza kidogo ili waelewe uhusiano uliopo katika mambo hayo mawili.
Hekalu linalokwenda kujengwa ni hekalu la tatu na la mwisho katika israel, ambapo ndipo litakapokuja kusimama chukizo la uharibifu DANIEL 9:27. Chukizo hili ni mpinga kristo ambae pia ni Asi, mpingamizi au mnyama!.
Ikumbukwe tu katika wakati wa dhiki kubwa wa miaka saba ndipo mpinga kristo huyu atakuwa wazi sana, na kipindi hicho cha dhiki kubwa kinagawanywa katika sehemu mbili, miaka mitatu na nusu ya mwanzo au miezi 42 au siku 1260 na kipindi cha pili cha miaka mitatu na nusu mingine.
Katika kipindi cha kwanza mpinga kristo atafanya agano thabiti na israel na kuisapoti israel sana hata katika ujenzi huo na isrel itadanganyika sana LAKINI baadae sasa mwishoni mwa miaka mitatu n nusu ya mwanzo atalivunja agano na atawageuka waisrael na ndipo chukizo hilo litasimama sasa!
Ikumbukwe kuwa wakati wa dhiki kubwa ni israel peke yao ambao wana neema ya kuokolewa maana wakati wa mataifa(majira ya neema yatakuwa yamefika mwisho), ikiwa israel watafata maelekezo ya Bwana Yesu katika MATHAYO 24:15-22.
Sasa haya yote hayawezi kutokea kabla ya kanisa kunyakuliwa, yaani mpinga kristo hawezi kufunuliwa wazi kwa sababu kanisa bado lipo duniani na ndio linalozuia 2WATHESALONIKE 2:3-7, nanukuu mstari wa 6 na 7 "na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake, Maana ile siri ya kuasi inatenda kazi hivi sasa,LAKINI yuko azuiaye hata atakapoondolewa.
Kuja kwa Bwana Yesu kulinyakua kanisa(watakatifu) itakuwa inamaana ya kupisha kipindi cha dhiki kubwa duniani na kufunuliwa kwa mpinga kristo sasa. Mungu wakati kabla ghadhabu yake haijashuka huwa na anawatenga wenye haki kama ilivokuwa kwa nuhu, luthu na hata Lahabu..
Kanisa halitapitia kwenye dhiki kubwa ya miaka saba kama wengine wanavyodai, ndio maana Bwana Yesu atawanyakuwa juu mbinguni kupisha dhiki kubwa duniani.
Sasa basi kama ukisikia habari za israel kufanya agano au kuweka mkataba na umoja wa nchi za ulaya ukiwa duniani ujue tayari umeachwa!!!
BWANA AMSAIDIE KILA MMOJA WETU ASIWE MTU WA KUACHWA BAADA KUSOMA HAPA,AMEN!!!
HIO HAPO CHINI NI PICHA YA RAMANI ILIONDALIWA AMBAYO NI YA HEKALU LA TATU LINALOTARAJIWA KUJENGWA ISRAEL AMBALO WANASEMA LITACHUKUA MUDA WA MIAKA MITATU KUKAMILIKA!!!
No comments:
Post a Comment