Wednesday, January 17, 2018

WOKOVU NI AMANI

WOKOVU NI AMANI MAISHANI MWANGU, SIJUI KWAKO???

✔Wokovu au ukombozi umenitoa katika utumwa mzito wa dhambi na uovu mwingi.
Wokovu ni zawadi ya moyo mpya wa nyama na roho mpya.

✔Wokovu unapatikana kwa njia ya mwana wa Mungu YESU KRISTO pekee, MATENDO 4:10-12.
Wokovu unauhusiano mkubwa na ufalme wa mbinguni ambao hata sasa tunao kwa njia ya Yesu kristo alietupenda.

✔Wokovu upo kwa wale wanaomtii na kumfata YESU,na hii ndio siri ya injili.

Wokovu katika biblia unaelezwa kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo.
1. Ni siri ya MUNGU iliofunuliwa kwetu.
▪Waefeso 3:9, 6:19

2. Ni mpango wa MUNGU uliowekwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.
▪Waefeso 1:3-14

3. Ni nuru iliofunuliwa kwa mataifa
▪Luka 2:30-32

4. Ni kupita kutoka mautini na kuingia uzimani
▪Yohana 5:24

5.Ni ujumbe maalum kwa wenye dhambi wote utakaowageuza nia zao.
▪Marco 2:17

6.Ni zawadi ya neema tunayoipokea kwa imani wala si kwa matendo
▪Waefeso 2:8-9

7.Ni haki ya MUNGU iliofunuliwa au iliodhihirishwa kwa wanadamu wote
▪Warumi 1:16-17,Warumi 4:22-25.

8.Ni upatanisho wa MUNGU na wanadamu
▪2Wakorintho 5:18-19

9.Ni kuzaliwa mara ya pili katika roho.
▪Yohana 3:1-11.

10. Ni kuwa mfu katika dhambi na kuwa huru mbali na dhambi zote
▪Warumi 6 yote.

11. Ni kuwa na Amani na MUNGU
▪Warumi 5:1

✔Wokovu ni badiliko halisi la kimwili na kiroho ambalo lina ushuhuda wa wazi kabisa kwa mtu.
Msingi wa wokovu ni kutubu dhambi zote kwa kumaanisha kuziacha kwa imani na kuambana na ubatizo wa maji tele
▪Matendo 2:38, 20:21.

✔Lakini Wokovu si kutubu dhambi tu lakini ni kutubu dhambi na kuzaa matunda yapasayo toba na kuweka imani yako kwa YESU
▪Marco 16:15, Yohana 6:47.

✔Kwa YESU tulichaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu(waefeso 1:4), kwa imani tumeokolewa(warumi 8:24) Na kwa njia ya msalaba ni Nguvu kubwa ya MUNGU kwa wale wanaondelea kuokolewa( 1wakorintho 1:18).

✳RAFIKI, UTAPATAJE KUPONA NA HATARI YA KWENDA MOTONI USIPOUJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII?

✳TUBU LEO NA KUAMUA KUMFATA YESU ANAEBADILISHA, ACHANA NA MAFUNDISHO MANYONGE ,ACHANA NA DHAMBI NA UOVU, LITAFUTE NENO LA KWELI LA KRISTO LINALOHUISHA MWILI NA ROHO.

✔ISAYA 55:6-7
"Mtafuteni BWANA maadamu       anapatikana,
mwiteni,maadamu yu karibu.
Mtu mbaya na aache njia yake,
na mtu asiehaki aache
mawazo yake;
Na amrudie BWANA,
Naye atamrehemu;
Na arejee kwa MUNGU wetu, Nae atamsamehe kabisa..

No comments:

Post a Comment