UZURI/UREMBO BANDIA, UTAKUPELEKA MOTONI.
UFUNUO 21:27 "Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilichokinyonge,wala yeye afanyae machukizo na uongo,bali wale walioandikwa katika katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo".
Andiko hilo kwa kiingereza,NIV linasomeka hivi , "Nothing impure will ever enter it, nor will anyone who does what is shameful or deceitful, but only those whose names are written in the Lamb’s book of life"
Yeyote alie Mnyonge [impure] na anafanya machukizo [Abomination/shameful] na ni mdanganyifu/mwongo [deceitful/false] hana sehemu katika UZIMA wa milele.
Kwa msingi huo sasa yeyote anaetumia;
NYWELE BANDIA [FALSE HAIR]
KUCHA BANDIA [FALSE NAILS]
LIPS BANDIA [FALSE LIPS]
NYUSI BANDIA [FALSE EYELASHES]
USO BANDIA [FALSE FACE/MAKE UPS]
UZURI BANDIA [FALSE BEAUTY].
Wote hawa wanafanya machukizo na Uongo na hawana sehemu katika uzima wa milele.
UFUNUO 21:8, Waongo wote (all lairs/false) seheme yao ni katika lile ziwa la Moto na kiberiti.
Wanawake wengi wanakwenda motoni kwa sababu ya mambo haya au yanayofanana na haya.
Njia ile ni Nyembamba, wanaiendea ni wachache na ni wale wasio na machanganyo yeyote wala hawafanyi machukizo yeyote yale. Ni watakatifu(holy and pure) katika njia zao zote.
Huu ni wakati wa kutubu na kuacha mambo yote ya uongo(false/fake) ya ibilisi na kumaanisha kukaa kwenye kweli(neno la Mungu) kwa gharama yeyote.
Amua moja Kutubu au upotee milele,
#Yesu anakuja kulitwaa #kanisa takatifu lisilo na #doa wala #waa wala #kunyanzi.
Na. Isaiah Membe.
No comments:
Post a Comment