Tuesday, January 16, 2018

ITAFUTE KWELI, USIFATE UMATI

USIFATE UMATI WA WATU, ITAFUTE KWELI YA NENO.

Yesu alisema wazi kabisa kuwa njia inayoenda uzimani ni nyembamba sana, tena imesonga na zaidi ni wachache wanaoiona na wanaopita njia hio. lakini pia wengi watajitahidi kuingia kwenye njia hio wasiweze.(Mathayo 7:13-14).

Kinyume chake, Njia ni PANA sana, hakuna kubanana, kuna uhuru mwingi na WENGI wanaenda katika njia hio ambayo inaenda UPOTEVUNI kwa shetani.

KATIKA NJIA PANA
#Kuna uhuru wa kufanya lolote unalotaka kufanya bila kujali biblia inasema nini

#kuna mafundisho laini yadanganyayo,yanayofundishwa na wachungaji ambao nao wako katika njia pana vilevile.

#hakuna kukemewa kwa dhambi na uovu, wanaangalia pesa yako tu basi.

#Injili ya kweli ya utakatifu haihubiriwi katu, ni mafanikio tu ya kimwili ambayo shetani anajua watayaacha yote hapo na kwenda Moja kwa moja motoni.

#Watu wanavaa wanavyotaka kwa mafundisho kuwa Mungu haangalii mambo ya nje anaangalia roho.Mavazi ya hovyo sana yaruhusiwa kanisani bila shida.

#Watu wanaambiwa wako huru ndani ya Yesu kwa hio hakuna shida hata wakivaa wanavyotaka, wakijipamba wanavyotaka.wanafarijiwa wanaenda mbinguni hali wako katika njia PANA.

#Kuna watu vuguvugu ambao hawana nafasi katika uzima wa milele maana watatapikwa na Bwana Yesu watoke katika kinywa chake.

Kwa sababu hio ni UMATI mkubwa wa watu leo wako katika njia pana.

KUPITA njia nyembamba ni gharama, inahitaji kweli kujikana nafsi, kuwa tayari kuacha yote ya dunia, na kuuchukua msalaba wako na kumfata Yesu kwa kila neno.(Luka 9:23-26, Luka 14:25-33, Mathayo 10:27-29).

injili ya Kweli ni ngumu sana, maana wapo wanaohubiri kweli ila sio kweli yote(Zaburi 119:6). haitakuwa rahisi kupita katika
njia hii bila kweli kudhamiria.

#hesabu gharama kabla hujajenga mnara. Itafutwe kweli ya neno itakayokupeleka mbinguni sio umati wa watu kwa mitume na manabii ambako utaishia Jehanam ya moto.

YESU ANARUDI, SAA YA MAAMUZI NI SASA.

Na Isaiah Membe.

No comments:

Post a Comment