Tuesday, January 16, 2018

USIFANYE MCHEZO NA WOKOVU, KILA KITU KINATIMIA MACHONI PETU.

USIFANYE MCHEZO NA WOKOVU, KILA KITU KINATIMIA MACHONI PETU WAZIWAZI.

Tupo katika wakati ambao tunatakiwa kuwa makini sana kufatilia na kuzingatia mambo yanayoendelea duniani.Trump ameutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa israel, december 6,2017.

Zingatia: Israel na palestina wote wanadai Yerusalemu kuwa mji wao mkuu na mtakatifu(holy land).

Ukweli:Jerusalem umekuwa mji mkuu wa wayahudi toka zamani zile za mfalme Daudi katika maandiko{2nyakati 6:4-6; 2NYAKATI 12:13, EZRA 7:14-15,27} Mpaka wakati ule wa 70 AD ambapo wayahudi walitawanyika duniani kote katika mataifa mbalimbali.{ WALAWI 26:33, EZEKIEL 36:19, KUMBUKUMBU 28:64}.

Kitu cha kuangalia hapa:

Hii itaenda kuongeza chuki kwa wapalestina na kuwafanya  palestina na mataifa mengine ya kiislam yainuke kinyume na Israel, Chanzo cha vita kuu ya Tatu ya Dunia.

Wayahudi wanahitaji kujenga hekalu la tatu na la Mwisho kama maandiko yanavyosema, HEKALU ambalo vifaa vyote vya ujenzi  tayari vimesha andaliwa, na Ni Lazima HEKAKU lijengwe Yerusalemu, sehemu ileile ya DOME OF THE ROCK,Mahali ulipo msikiti wa Al-aqsa ambapo waislam wanapachukulia kama sehemu muhimu katika mashariki ya kati yote.

Ikumbukwe toka hekalu ya Pili la suleimani mtoto wa DAUD, kubomolewa mwaka ule wa 70 A.D wayahudi hawajawahi kuwa na hekalu, leo ni takribani miaka 1947 Imepita.

Chochote kinaweza kutokea kuanzia sasa:

Mambo yatajayofuata baada ya hayo sasa ni kama ifuatavyo.

1.Yerusalem Wote  utakuwa mji mkuu wa Israel.

2. kunyakuliwa kwa kanisa, Kupisha dhiki inayokuja.

3.Kujengwa kwa hekalu la Mwisho katika mji wa Jerusalem,Kama maandalizi ya ujio wa mpinga kristo.

4. Kufunuliwa kwa mpinga kristo, mnyama Na utawala wake.

5. Dhiki kubwa Kwa miaka saba Duniani na Harusi ya mwanakondoo Mbinguni Kwa miaka saba.

6.Kuja kwa Yesu kristo mara ya pili duniani na watakatifu wake aliowatwaa wakati wa kunyakuliwa kanisa(Watu waliookoka) Na vita vya Har-magedoni

7.Utawala wa Yesu kwa miaka 1000 duniani Pamoja na watakatifi.

8. Vita vya Gogu na magogu.

9.Hukumu ya mwisho, kwa wote waliohai na waliokufa.Kuharibiwa kabisa kwa dunia hii ya dhambi.

10. Mbingu mpya na Nchi mpya.

11. Waliomwamini Mungu wataishi na Mungu katika uwepo wake, milele na utukufu utakuwa nao milele yote.

12. Wenye dhambi wote(walioukataa wokovu) watadumu katika ziwa la moto, wakilia na kusaga meno, milele na milele.

Hakuna muda tena wa kupoteza, me naanza na wewe unaesoma ujumbe huu....

Mpendwa, umesikia yote. Anza kuvua roho za watu wasiolewa haya ili wasiingie katika maangamizo haya yanayokuja.

Lakini pia jichunguze wewe mwenyewe, jitathmini, tembea katika njia ya Neno. Angalia kama kuna mahali umeanguka, ukatubu, na kulifata Neno tokea hapo.

Ule mwisho uko mlangoni! kwa sababu hio, tafadhali shirikisha na wengine Haya, inaweza kuokoa maisha ya mtu fulani.

Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment