KIPIMO SIO KWENDA KANISANI
Watu wengine siku za ibada kama Jumapili au jumatano, wanakuwa katika mambo yao wenyewe, wengine watakuwa bar, wengine shambani, wengine kwenye biashara zao nakadhalika.
Kutokana na hili sasa wengi watawachukulia wale wanaokwenda kanisani kuwa ndio watu wa Mungu Na wale wasioenda ni watu wa shetani.
Lakini jambo hapa la kufahamu ni kuwa hata katika kundi hilo la watu waendao kanisani kuna wengi pia ambao wako mbali sana na Mungu.
Wengine wanaenda kanisani kupotezeza Muda tu, wengine kutafuta wachumba, wengine kutafuta uponyaji, wengine kutafuta baraka tu nakadhalika.
Bwana Mungu anasema watu hawa wanaenda ibadani na hukaa kama watu wa Mungu lakini sio watu wanaompenda Mungu. EZEKIEL 33:30-33. MARCO 7:6.
Sikiliza kipimo si kwenda kanisani, kipimo sio kuhubiri wala kufundisha, Kipimo sio kujionyesha kwa watu kwa unafiki tu LAKINI Kipimo ni kuishi MAISHA YAKO sawasawa na NENO la MUNGU.(ZABURI 119:6,9).
Wengi wa hao waendao makanisani hawalifurahii NENO la MUNGU, kwa sababu silo walilolifata hapo, hawataki kukemewa Maovu yao wala hawataki kuonywa KINYUME chake wanapenda MANENO LAINI YADANGANYAYO, ISAYA 30:9-11.
Wako wengi wanaenda kanisani lakini hawataki maisha yao ya dhambi yaguswe Kabisa katika mahubiri kwa sababu Ndani yao hamna kitu, wako kanisani kwa Lengo lingine kabisa!
Kuwa watu wa Mungu ni vile tunavolitii na kulifurahia neno la Mungu (ZABURI 119,9,103), Vile tunavyokuwa Tayari kukemewa na kuonywa kwa Neno la MUNGU (ZABURI 119:105), Kuwa mtu wa Mungu ni jinsi gani tunavyonyenyekea na kuwa tayari kuongozwa na NENO la Mungu.
Ukisema unampenda Mungu wakati neno lake hulipendi ambalo Ndilo hasa linalotusafisha na kututakasa (YOHANA 17:17), NENO ndilo linagusa maisha yako ya dhambi na kuweka wazi uchafu wote wa uovu na kutufanya Kutubu, KAMA HULIFURAHII NENO rafiki, HAPO hakuna kumpenda Mungu,
kumpenda Mungu ni kuzishika amri zake YOHANA 14:21,23-24. wakati unakuja ambapo Magugu na ngano vitatengwa.Maana Yesu alisema yaacheni magugu na ngano vikae pamoja ila wakati unakuja atakapoyatenganisha magugu na ngano na hapo ndipo itakuwa wazi nani alikuwa MBUZI na nani alikuwa KONDOO,
USIKUBALI KUWA katika kundi la Mbuzi au Magug, Kama unaamua Amua kuwa mtu wa Mungu kweli kwa Kumaanisha kulishika Neno lake lote bila kuchaguachagua ya kushika na yanayokugharimu unayaacha.ZABURI 119:6,9,11,98-100.
Ubarikiwe sana.
Isaiah Membe,Mtumwa wa Kristo.
No comments:
Post a Comment