tunapouendea mwaka mpya, ni muhimu sana kuzingatia neno hili KUTUBU.
19 TUBUNI basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
➡Matendo ya Mitume 3 :19.
"30 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali WATUBU.
➡Matendo ya Mitume 17 :30.
"16 Basi TUBU; na USIPOTUBU, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.
➡Ufunuo wa Yohana 2 :16.
Neno hili Linamhusu kila mmoja bila kujali nafasi na cheo chake katika jamii, Tangu Rais mpaka raia wa kawaida, maadam ni mwanadamu, Mungu anakutaka KUTUBU kabla ya kuuendea mwaka mwingine wa 2018.
Mwaka wote huu umefanya mabaya mengi na dhambi nyingi tu, umewafanya watu wengi kuumia, umedhulumu watu wengi, umekandamiza haki za watu, na dhambi nyingine zote ambazo umekuwa ukifanya.
Mungu ni kama alikuwa haoni yote hayo, sasa Amekuhurumia anakutaka UTUBU! vinginevyo ukiendelea kuwa na moyo mgumu usiotaka kushuka na kutubu.
➡UNAJIWEKEA AKIBA YA HASIRA YA MUNGU AMBAYO ITASHUKA KWAKO MUDA WOWOTE ULE.
WARUMI 2:4-8
"4 Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate KUTUBU?
"5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na TOBA, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,
"6 atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake;
"7 wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele;
"8 na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu;
➡WARUMI 2:4-8.
#Utubu_na_kugeuka.
No comments:
Post a Comment