JE, NI SAHIHI MKRISTO KUCHEZA MICHEZO YA KWENYE KOMPYUTA(GAMES)
Kuna vitu ambavyo biblia haijavieleza waziwazi kutokana na kutokuwepo nyakati hizo ambavyo leo vinaleta utata kwa watu mbalimbali ambao wanataka kila kitu wakione kwenye biblia kama kilivo kwa nyakati za leo.
Mtu mmoja ameniuliza swali leo kwamba Je, naweza kucheza michezo ya kwenye simu au computer( video games)?? Nilimjibu lakini nikaona bora niliseme na hapa kwa faida ya wengi.
Jambo hili la kucheza michezo hii ya kwenye computer au simu huwezi kulikuta moja kwa moja kwenye biblia kama lilivyo ila tutaangalia misingi ya kibiblia ambayo bado inatumika pamoja na kwamba mambo haya hayakuepo nyakati hizo ila misingi hii inatupa kujua kwa upana zaidi juu ya jambo lolote tunalolifanya.
Mwenyewe nilikuwa mchezaji mzuri wa michezo hii kwenye simu na computer ila kwa neema ya Mungu nimeacha badala yake natumia muda huo sasa kumtumikia Mungu.
Kabla ya kuendelea ni muhimu kufahamu kuwa jambo lolote ambalo linatutoa kwenye upendo wetu wa kwanza katika kumpenda Mungu na kufanya mapenzi yake hatuna budi kuliangalia vizuri jambo hilo na kuliacha kabisa maana linaweza kuwa sanamu kwetu(mungu wetu).
Misingi inayotupa kujua na kujibu maswali yote yanayohusu kucheza michezo hii ya kompyuta, kuangalia filamu, ushabiki wa mipira nakadhalika.
1.JE, MICHEZO HII INAKUJENGA AU INAKUBURUDISHA?
Jiulize michezo hii itakufanya uongoze upendo wako kwa Mungu? Au maarifa yeyote ya Mungu na kuwafundisha wengine? Maandiko yanasema 'vitu vyote ni halali lakini si vyote vifaavyo (1wakorintho 10:23-24) (Warumi 14:19).
Mungu anapotupa muda wa kupumzika ,tutafute vitu vinavompa Mungu utukufu (wagalatia5:13-17).
2.JE, MICHEZO HII INATIMIZA MATAKWA YAKO AU YA MUNGU?
Mapenzi ya Mungu yanajumuishwa katika Amri kuu ya "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wote, akili zako zote na nguvu zako zote" (Luka 10:27). Kusudi la Mungu kwa mwanadamu linafunikwa na dhambi na Yesu ametuokoa na sasa hatufanywi matakwa yetu wenyewe ila Matakwa ya Kristo (Wafilipi 3:7-9). Lazima mapenzi ya Mungu yawe juu ya mapenzi yetu (Zaburi 143:10 ) (zaburi 40:8a), (waebrania 13:21).
3.JE,MICHEZO HII INAMTUKUZA MUNGU?
Mingi ya michezo hii inatukuza vurugu, uasherati, uonevu, wizi, ujambazi, n.k. kama wakristo Vitu tunavofanya lazima vilete utukufu kwa Mungu (1wakorintho 10:31) na vinatusaidia kukua katika maarifa na neema Ya kristo.
4.JE,MICHEZO HII INATUPELEKA KUFANYA MATENDO MEMA?
"Maana tu kazi yake,tuliumbwa katika Kristo Yesu,tutende matendo mema,ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo". Michezo hii haitupeleki kutenda matendo mema ambayo Mungu anakusudia kwetu.
5.JE,MICHEZO HII INAKUPELEKA/KUKUFANYA KUWA MTUMWA?
Watu wengi michezo hii inawafanya kuwa watumwa hasa(addicted).Mambo haya hayana nafasi katika ukristo. Paulo mtume anasema michezo yetu iwe ya rohoni na anaifananisha kama mwana riadha ambae anajizuia katika mambo mengi kama kulewa ovyo, kutembea ovyo n.k ili ajiweke afya yake kuwa vizuri kwa ajili ya kupata tuzo. Maisha ya mkristo ni hivohivo pia unapaswa kujizuia katika mambo menhi ili upate uzima wa milele na tuzo isioharibika. (1Wakorintho 9:25-27).
6.JE, MICHEZO INAKUFANYA UUKOMBOE WAKATI?
Kumbuka utatoa hesabu juu ya ulivotumia muda wako mfupi uliopewa na Mungu duniani. Kupoteza muda wa masaa kucheza michezo hii,kunakupotezea muda mwingi ambao ungeutumia kwa Bwana au kusoma neno.
Ishi kama mtu mwenye busara ukuukomboa wakati maana zamani hizi ni za uovu,yajue mapenzi ya Mungu ni yapi kwako.(Efeso 5:15-17, 1petro 4:2, kolosai 4:5, yakobo 4:14, 1petro 1:14-22).
7. JE, MICHEZO HII INAKUFANYA KUFIKIRI YA MUNGU AU YA KIDUNIA?
Wafilipi 4:8 "Hatimae ndugu zangu,mambo yote yalio ya kwel, yoyote yalio ya staha, yo yote yalio ya haki, yo yote yalio safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema;ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa njema, yatafakarini hayo."
8.JE, MICHEZO HII INAENDANA NA KUSUDI LA MUNGU KWAKO.
Paulo mtume aliandika ,siku za mwisho watu watakuwa wenye kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu (2Timotheo 3:4).
Utamaduni wa magharibi unatimiza haya maandiko maana watu leo wanavutwa zaidi(kulevywa) na vitu vinavoitwa burudani kama vile filamu(series), mipira, miziki ya kidunia kuliko wanavyoweza kuvutwa na neno la Mungu.
Kama umeokoka na wewe unavutwa na vitu hivi huna tofauti na mataifa wafilipi 2:15. 3:7-10, 1yohana 2:15-17.
9.JE, MICHEZO HII ITAKUFANTA KUUTAZAMIA UZIMA WA MILELE.
Tunaishi tukiwa na tumaini la kupaya thawabu kutokana na kama tumeishi kwa kusudi la Mungu na kwa uaminifu duniani (mathayo 6:19-21), (1wakorintho 3:11-16)
Kama tunautazamia uzima wa milele ,tutatoa muda wetu na mioyo yetu kwa Bwana katika huduma (Wakolasai 3:1-2,23-24).
Vitu tunavovimiliki au tunavovifanya ambavyo vinatufaya tuukose uzima wa mileke na kutufanya upendo waetukupoa lazima tuwe tayari kuachana navyo (Luka 12:33-37).
Wengi wanajaribu kutimiza/kutumikia kotekote Mungu na matakwa yao Lakini Yesu alisema wazi kuwa hatuwezikuwatumikia mabwana wawili Mathayo 6:24.
Tunapopata muda wa kupumzika kama Yesu alivofanya (Marco 6:31),tuchague vitu vitakavyo tujenga na kumtukuza Mungu.
God bless you, prepare for eternity!
No comments:
Post a Comment