Tuesday, January 16, 2018

SHIKA SANA NENO SIO DINI.

SHIKA SANA NENO SIO DINI.

Mpendwa, ikiwa tunataka kuingia mbinguni hatuna budi kukishika Neno la Mungu, sio dini.

Biblia inasema katika
ZABURI 119:9.
"Jinsi gani kijana aisafishe njia yake ,ya kwenda mbinguni ni kwa kutii ,akilifuata neno lako". Biblia hapa haisemi kwa kutii, akiifuata dini yake, bali Neno la Mungu".

Kumbuka kwamba mtu anapokufa hataulizwa alikuwa dini gani, kitakachoangaliwa ni Je alikuwa  MTAKATIFU, Ambao pasipo huo utakatifu haitawezekana kwa namna yeyote kumuona Mungu. WAEBRANIA 12:14.

Kulishika Neno la Mungu ndio kumshika YESU, maana Yesu  anaitwa neno la Mungu UFUNUO 19:13.

Dini haiwezi kumpa mtu uwezo wa kushinda dhambi, ni YESU tu Ndie mwenye uwezo Huo.

Ndio maana watu wengi ambao ni
makahaba, majambazi, Walevi
Wavuta bangi, Watukanaji, Washirikina, Bado wanadini zao pia na wana majina ya kidini kabisa lakini dini zao hazijawasaidia au kuwawezesha kushinda dhambi, bado wamekuwa watumwa wa dhambi pamoja na kwenda kanisani jumapili.

NJIA NI MOJA TU, NJIA NI YESU KRISTO HAKUNA KWENDA KUSHOTO AU KULIA, anasema katika:-

YOHANA 14:6,
"Mimi ndimi njia na kweli na uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi(Yesu)".

Mpendwa najua una dini yako Unayoipenda lakini jihoji mwenyewe Moyoni mwako na uwe mkweli je, maana dhamiri ni mkalimani mzuri wa maisha Yetu, jiulize je, una uwezo wa kushinda dhambi? Dhamiri yako inazungumza kwa sababu maisha yako unayajua ni maisha yakiojaa dhambi pamoja na kusema una dini,
HUNA tofauti yeyote na mpagani maana mpagani analewa pombe na wewe unalewa pombe, mpagani anavuta sigara na wewe unavus sigara, mpagani anacheza dansi na wewe unaejiita Mkristo unacheza dansi, tofauti yake na wewe ni nini?

kama Unajigundua kabisa bado ni mwenye dhambi na hauna uwezo wa kushinda dhambi, nafasi bado ipo ya kurekebisha njia zako,

ANZA UPYA LEO, SEMA YATOSHA MAISHA YA DHAMBI, na sasa unachotakiwa kufanya ni kumkimbilia Yesu na kumwambia  Akusamehe kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha (MITHALI 28:13) na umwambie Yesu leo akupe uwezo kushinda dhambi zote(YOHANA 1:12) Nawe utaokoka maana ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako, UTAOKOKA( WARUMI 10:9-10).

Ubarikiwe sana.

Na Isaiah Membe, Mtumwa wa Kristo.

No comments:

Post a Comment