✔Mungu anajali na kuuangalia mwili wako wakati wote sio moyo wako pekee. Moyo unaonyenyekea kweli kwa Mungu(uliotakaswa) Utafahamu kuwa Mungu anamhitaji kuwa mtu huyo kuvaa mavazi ya heshima na kujistiri {1TIM 2:9}.
✔Mungu anaangalia jinsi gani utautoa mwili wako kuwa dhabihu kuliko hata sadaka zingine kama kusifu na kuimba kwaya.
➡ Nyie mnaojiita ni walokole wa kisasa, manaosema Mungu haaangalii nje( mwili), anaangalia roho tu, BADILIKENI 2018.
✔Huwezi kuuona uwepo wa Mungu, ukiwa nusu uchi, umevaa mapambo yan namna yeyote ( heleni, mikufu, mabangili, mawig, marasta n.k), Umeweka make ups, umevaa suruali mwanamke au vazi lolote la Mtego. Kinyume chake hicho unachokiita uwepo wa Mungu ni uwepo wa mapepo!!!! { MWZ 35:1-5}
➡Mnaosema kujipamba hakuna shida, Wakati Mungu anasema kuna shida, BADILIKENI 2018, kabla maangamizo hayajaja kwenu.
✔Wachungaji wa Kisasa na injili zenu za kisasa, mnahubiri na kufundisha kuwa Wanawake wanaovaa mavazi marefu kuwa ni washamba,wamepitwa na wakati.Mnafundisha et Mungu amebadili namna ya kuvaa, Kwa hio mnaviondoa viwango vya Mungu vya utakatifu, mnaweka viwango vyenu, Bila kujua mnalifanya kanisa kujaa dhambi na mnawaongoza watu kwenda motoni.
➡wachungaji wote wa Namna hii, Hamna mbingu ya kuwapeleka watu kwa viwango vyenu, NANYI BADILIKENI 2018,Kinyume chake mtapata hukumu ilio kubwa zaidi {YAKOBO 3:1}.
✔Wanawake wote mnaosema et Tunauhuru wa kufanya chochote, kwa kuwa majira haya ni ya NEEMA. Kwa hio Mnavaa suruali na nyie kama wanaume, wengine mnampa Mungu sababu et kwa Sababu ya baridi, MUNGU alijua baridi ipo ila amezuia {KUMB 22:5} .
✔NEEMA gani hio inayompa mtu kufanya chochote kinyume na neno la Mungu? HAKUNA NEEMA ya namna hio, Dada,maMma na binti mchungaji wako anaekwambia ni sawa anakudanganya na anakupeleka motoni na suruali zako hivo utavuna mauti ya milele {RUM 6:23} maana ni machukizo Kwa Bwana.
➡Wanawake Mnavaa suruali, sio neema hio ni Ushamba wa kiroho huo na upungufu wa maarifa ya neno la Mungu, BADILIKENI 2018,Neema bado ipo!!!
✔KAMA umepata kibali cha kuingia 2018, na bado unafanya hayo yote, Mungu amaekupa neema tu na nafasi ili utubu maana 2017 yote amekuwa akisema na wewe ila umeendelea kukaidi, ANASEMA NA WEWE LEO TENA.
✔Itafikia mahali Mungu kukuchoka kutokana na Moyo wako usio na TOBA ambao unashindan na Neno la Mungu, Na sasa kitakachofata ni Ghadhabu yake juu yako {WARUMI 2:5}… na Neno la Mungu, Na sasa kitakachofata ni Ghadhabu yake juu yako {WARUMI 2:5}.
TUBU! TUBU! TUBU!! MAJIRA YA NEEMA BADO HAYAJAFIKA MWISHO.
➡Bwana ni mwanifu hatakutupa nje, atakusamehe na kukupa uwezo wa kuyaishi hayo maisha mapya ya Usafi na utakatifu!!! Anachokitaji kwako ni utii na utayari,MENGINE ANAFANYA MWENYEWE.
#Holiness_and_righteousness
Ndugu Yako katika Kristo;
Isaiah Membe.
No comments:
Post a Comment