Tuesday, January 16, 2018

MAVAZI NA MTAZAMO WA KIKAHABA

MAVAZI NA MTAZAMO WA KIKAHABA.

MWANZO 38:15 ,"YUDA ALIPOMWONA ALIMDHANIA YA KUWA NI KAHABA...".

Mbinguni unaweza kusajiliwa wewe ni kahaba kwa sababu ya uvaaji wako tu wala haiitaji kuwa unafanya uzinzi au uasherati au kuuza mwili wako kabisa, LAKINI bado mbinguni utahesabika wewe ni kahaba na jina lako kuondolewa katika kitabu cha uzima kutokana tu na mavazi yako.

kwa hakika! Unaweza kuwa bikira kabisa lakini mbinguni unaonekana wewe ni kahaba, hii inatokeaje? inatokea kutokana na kile unachokivaa.

kama mwanamke unavaa mavazi yanayoacha uchi wako wazi, mavazi mafupi(vimini)ambayo yanaacha mapaja yako wazi kabisa, mavazi yanayoacha matiti yako wazi kwa namna yeyote, mavazi yanayoacha tumbo, mgongo na makwapa wazi.

Unapovaa mavazi kama hayo, mbele za Mungu unaonekana kama kahaba.

vilevile umapovaa mavazi yanayokubana mwili ili kuchora maungo na maumbile yako vizuri na kuwaonyesha watu waone maumbile yako,mavazi ambayo ukikaa hayafuniki magoti, Mbele za Mungu wewe ni kama kahaba..

Inaweza ikawa ni ngumu kwako kulipokea neno hili,LAKINI NDIO VIWANGO VYA UTAKATIFU VYA WATU WANAOWAZA KUINGIA MBINGUNI.

Unaweza kuwa mchungaji, mhubiri, mwimbaji au yeyote yule umaeweza kuwa, lakini kwa Mungu ukaonekana wewe ni kahaba mwenye heshima kwa wanadamu.

kama ni ngumu sana wewe kuliamini neno hili unaweza kusubiri wakati ule katika geti la mbingini watakapobaguliwa kondoo na mbuzi,ambapo utakuwa tayari umeshachelewa na SITAKUSHAURI kusubir wakati huo.

Kutakuwa na mshangao mkubwa siku ile ya unyakuo lakini pia siku ile ya hukumu ya aibu na kudharauliwa milele, watu watasema Bwana mimi sikuwahi kuwa Kahaba hata siku moja.

Na kama mwanamke wa Kikristo hio ndio itakuwa sababu yako mbele za Mungu kwa kuvaa mavazi yanaacha uchi wako wazi? utajiteteaje kwa mavazi yaliokuwa yanakubana mwili wako, mavazzi yaliokuwa yanaonyesha nguo zako za ndani, utajiteteaje kwa vimini na suruali unazozivaa?

MWANZO 38:21,"AKAULIZA WATU WA MAHALI PALE,AKISEMA YUKO WAPI YULE KAHABA ALIEKUWAPO ENAIMU KANDO YA NJIA? WAKASEMA HAKUWAKO HAPA KAHABA.

wengi wanafikiri kahaba ni yule anaesimama kando ya barabara akisubiri wanaume. KAHABA ni mwanamke yeyote ambaye anaefanya uzinifu na mwanaume kwa ajili ya kupata kitu fulani, hata kama haonekani hadharani..

kama wewe mwanamke ,ulifanya ngono au mapenzi ili kupata kazi unayoifanya,mbele za Mungu wewe ni kahaba hata kama ni mara moja tu.

kama wewe mwanamke ulimruhusu mwanaume kulala na wewe ili upandishwe cheo kazini, urudishwe kazini, uingie mkataba au kwa ajili ya masomo yako(ufaulu mitihani,upate cheti n.k) Mbinguni wewe unatambulika kama kahaba(prostitute) bila kujali ni mara moja au mara nyingi!!!

UKWELI HUU HAPA⤵

Chochote unachokipata au ulivyovipata kwa wewe kulala na mwanaume,hata kama vitu hivi ilikuwa ni haki yako lakini kwa sababu uliruhusu mwanaume kulala na wewe kabla ya kuvipata, Mbinguni unahesabika kama kahaba:- kazi, vyeti na faida unayoipata ni matokeo ya ukahaba wako hata mshahara unaoupata kutokana na ukahaba unaitwa ni mshahara wa kahaba.

JAMBO KUBWA NI KUWA.

Kama unatoa fungu la kumi au sadaka kutokana na ukahaba wako,unajitafutia hukumu kubwa mbele za Mungu katika maisha yako Kwa sababu MUNGU ameonya kuwa mshahara wa kahaba kamwe usiletwe katika Nyumba yake(MUNGU).

Hili hapa neno la Mungu katika;-

KUMBUKUMBU 23:17-18 "PASIWE NA KAHABA KATIKA BINTI ZA ISRAEL, WALA PASIWE NA HANITHI KATIKA WANA WA ISRAEL WANAUME. USILETE UJIRA WA KAHABA, WALA MSHAHARA WA MBWA, KATIKA NYUMBA YA BWANA MUNGU WAKO,KWA AJILI YA NADHIRI YEYOTE; KWANI HAYA NI MACHUKIZO KWA BWANA MUNGU WAKO,YOTE MAWILI.

Mchungaji anaepokea zaka na sadaka zako na hata anaweza kusema mtu yeyote tu anaweza kuleta zaka na sadaka kwa sababu yuko hapo kwa sababu ya pesa zako na wewe ukadanganyika.

Ili upate rehema za Mungu  unatakiwa kutubu toba ya dhati na kweli na Ufanye malipizo yanayoambatana na kutubu kwako.

Na. Isaiah Membe, Mtumwa wa Kristo.

No comments:

Post a Comment