UTAKUJA WAKATI WATAKAPOYAKATAA MAFUNDISHO YA UZIMA.
YESU alihubiri injili ya kweli, akasulibiwa.
STEPHANO alihubiri injili ya kweli, akapigwa mawe hadi kufa.
MITUME walihubiri injili ya kweli, wengine walichemshwa kwenye mafuta wangali hai,wengine walikatwa vichwa vyao, wengine walisulibiwa msalabani kichwa chini miguu juu, wengine walifungwa na kuburutwa barabarani n.k.
LAKINI leo Mchungaji,Padri,Askofu, Mtume au Nabii wako, ANAHUBIRI NA KUFUNDISHA KINYUME KABISA NA NENO LA MUNGU(UONGO), Mnashangilia na kupiga miruzi, NANI ANAMDANGANYA NANI???
NENO linasema,
2Timotheo 4:3-4," maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wanamaskio ya utafiti; Nao watajiepusha wasisikie yalio kweli, na kuzigeukia hadithi za Uongo."
Pia 2Timotheo 3:1-9, 2Petro 2:1-3, Yeremia 23:1-10.
wachungaji ambao ni maajenti wa ibilisi wanaopenda pesa kuliko Roho za watu.
Na Isaiah Membe, Mtumwa wa Kristo.
No comments:
Post a Comment