UKITAKA KUIONA HASIRA YA MUNGU BAADA YA KUTOKA DUNIANI.
Ufunuo 14:10
Yakobo 1:20
Yeremia 7:20.
Kama unafanya haya mpaka utakapo ondoka duniani bila kutubu, utaiona hasira ya Mungu.
Kama utaendelea kusujudu mbele ya sanamu yeyote ikiwamo ile wanayiita "bikira maria"
Mpe Talaka mke wako au mume wako.
Endelea kuvaa suruali mwanamke.
Kopa halafu kataa kulipa deni au kurudisha.
Acha kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
Kataa kusamehe wengine
Endelea tu na uasherati wako na usitubu.
Kazana tu kwenda kanisani na vimini vyako.
Endelea kuangalia picha na video ya ngono.
Endelea kumdanganya na kumuongopea mme/mke wako.
Mwanamke Acha kumtii Mume wako katika Bwana.
Endelea kupiga punyeto
Endelea kudanganya watu
Endelea kuchelewa kanisani kila ibada.
Tumia cheo chaka kuwanyanyasa na kuwakandamiza wengine wengine.
Endelea na wizi na ufisadi wako.
Endelea kupaka rangi midomoni na kwenye kucha.
Endelea kuvalia mapambo na kuweka nywele bandia
Endelea tu kujikweza na kujiinua na kuwaona wengine si kitu.
Endelea kufanya kazi na vyeti feki vya wizi.
Endelea tu kufundisha mafundisho ya uongo.
Endelea kulipuuza neno la Mungu na kuacha kulitii.
Penda fedha kuliko Mungu.
Acha kuwaheshimu baba na mama yako ktika yalio sahihi mbele za Bwana.
YOTE HAPO JUU NI DHAMBI na mengine mengi pia yanatosha kabisa kumfanya Mungu akasirike juu yako.
kama unataka Mungu asikasirike juu yako baada ya kuondoka duniani TUBU sasa.
Sababu inayomfanya Mungu asionyeshe hasira yake kwa wanadamu ni kwa sababu YESU aliununua muda huu kwa ajili yako na mimi ili atukomboe, ndio inayoitwa NEEMA Baada ya hapo hasira ya Mungu itafunuliwa kwa wanadamu.
Unao muda mwingi sana wa KUTUBU ukiwa duniani baada ya hapa ni HUKUMU
Waebrania 9:27.
No comments:
Post a Comment