✴Mtu anapokosa mtoto anapokuwa katika ndoa yake huwa anaumia sana kiasi cha wengine kuiacha imani na kwenda kwa mitume na manabii kutafuta miujiza baada ya kuona wameomba sana hawapati majibu.Hii yote ni kwa sababu wana uchungu wa kupata watoto.
✴Wengine wanaenda mbali zaidi na kuamua kuishia kwa waganga wa kienyeji kwa sababu haipendezi kukaa bila mtoto katika ndoa,Haipendezi kuwa tasa katika mwili.Ni zaidi sana katika Roho.
✴Tunamuona Hana kwenye biblia aliekuwa tasa iliamua kwenda masafa marefu sana katika maombi mazito ya kufunga na kumlilia Bwana kwa ajili ya kupata kupata mtoto wa kimwili tu. 1SAMWELI 1:1-20. Hatuna budi vilevile kuwa hivo katika roho.
✴Vivyo hivyo katika Roho Kuna kuwa na utasa wa kiroho, una muda mrefu umeokolewa lakini hadi leo hujamzalia Bwana mtoto hata mmoja. Huna watu wa kuonyesha mbele za Bwana kama matunda ya kazi aliotupa Bwana MATHAYO 28:19. Maana tumeokolewa sisi ili kuwaleta wengine kwa Yesu.
✴Tusiridhike tu kukaa wenyewe hivohivo siku zote katika hali ya utasa, badala yake tuugue na kuhuzunika na kuwa na uchungu mioyoni mwetu, hata kumlilia Bwana ili atutoe katika utasa huo wa rohoni, Kwa maana tawi lisilo zaa litakatwa!!
✴Inapendeza sana kuwa na watoto wa kiroho ambao umewapata kwa kazi na tabu yako kwa msaada wa Bwana,Ambao watakuwa ni taji yako ya kujionea fahari.
DANIEL 12:3
"3 Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele."
Danieli 12 :3
Mwenye hekima huvuta roho za watu
©Isaiah Membe, Mtumwa wa Kristo.
No comments:
Post a Comment