Wednesday, January 17, 2018

KUWAOMBEA WATU KWA FEDHA

WANAPOTEA KWA KUWA HAWAYAJUI MAANDIKO-KUWAOMBEA WATU KWA FEDHA.
Yesu alisema nyakati za mwisho kutakuwako mitume na manabii wa Uongo MAT 24:24 ambao watapoteza wengi hata waliowateule. Lakini pia alisema watu watakuwa wenye kupenda fedha kuliko kumpenda Mungu, 2TIMOTHEO 3:1-2.

Lakini katika UFUNUO 2:2 anasema tuwajaribu hao wajiitao mitume ili tujue kuwa ni waongo au namna gani, Mungu pia anasema tuzijaribu hizo roho tuone kama zinatokana na Mungu au La! tunawapima kwa NENO LA MUNGU.

Kuna wimbi kubwa la watu ambao wanatajwa ni watumishi wa Mungu, wanafanya maonbezi kwa watu kwa kuwatoza fedha. utaskia Mambo kama haya;
*kumuona mchungaji sh.10000.
*kuombewa ugonjwa fulani Sh.100,000 na mengi yanayofanana na hayo!

Maombezi yote ya uponyaji wa kibiblia kamwe hayafanyiki kwa fedha {MATHAYO 10:7-8.}

Karama zote tunazozipokea kutoka kwa Mungu, Mungu anatupa bure kabisa hakuna anaemlipa Mungu ili apate karama yeyote ile.

Neno KARAMA kama linavotajwa katika 1wakorintho sura ya 12 katika lugha ya asili linamaanisha ZAWADI (gift of the holy spirit).
Zawadi mara zote inatolewa bure bila kuilipia chochote.

Wokovu pia ni karama ambao tunaupokea bure Inayotupa uzima wa milele. Ukisoma andiko hili la WARUMI 6:23 kwa kiingereza utaona neno, THE GIFT OF ETERNAL LIFE.
Tunahesabiwa haki bure katika kristo Yesu pekee, WARUMI 3:23-24.

Sasa mtu anaombea watu kwa fedha, inabidi na mtu akitaka kuokoka basi amtoze afanye hivohivo amtoze pesa pia. Kama haiwezekani na hawafanyi hivo wanapowataka watu waokoke, basi na uponyaji ni vilevile, inawapasa kuwaombea watu bure bila fedha yeyote {ZABURI 103:3}

Yeyote anaeombea watu kwa fedha sio mtumishi wa Mungu alie hai hata kama ni mtu HUYO anajiita nabii,mtume,askofu na jina lolote lingine.

Uponyaji wote Yesu kaulipia na kuugharamia kwa kazi alioifanya msalabani aliposema yote yamekwisha( IT IS PAID IN FULL).Uponyaji wa magonjwa yote umeshalipiwa ,huna haja ya kutoa fedha kwanza ndio uombewe. Kufanya hivo ni kutokuifahamu Kweli ya NENO.

Watumishi wa Mungu wa nyakati za biblia walikuwa hawaombei watu kwa fedha mfano:

NABII ELISHA ,2WAFALME 5:13-18,20-27.

MTUME PETRO, MATENDO8:9-24.

Na mitume wote na nyakati za kanisa la kwanza.

Acha kudanganywa na mitume na manabii Hawa feki ambao ni maajenti wa ibilisi, hawana tofauti na GEHAZI mtumishi wa elisha, wamejaa uongo mwingi sana, utaskia wanasema "Bwana amesema na mimi, unipe gari lako" "Bwana amesema nami unipe nyumba yako" na mengi tu mengine yanayofanana na hayo.

Maandiko yanasema hizi ni nyakati za hatari,wengi watajitenga na imani wakiskiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani 1TIMOTHEO 4:1, 2TIMOTHEO 3:1.

Itafute KWELI ya NENO la MUNGU, IKUWEKE HURU ili  usije ukachukuliwa na roho hizi za nyakati za mwisho.

Bwana akubariki sana.

Isaiah Membe,Mtumwa wa Kristo.

No comments:

Post a Comment