ACHA POMBE, WALEVI WOTE HAWAURITHI UFALME WA MUNGU.
MITHALI 23:20, WALAWI 10:9.
Neno la Mungu linasema waziwazi kuwa tusiwe miongoni mwao wanywao pombe,inazungumzia kunywa sio suala la kulewa tu.
Mtu awae yeyote anaesema kuwa tunaruhusiwa kunywa kidogo ilimradi tusilewe ni sawa na kusema tunaruhusiwa kufanya uzinzi kidogo,hakuna tofauti yeyote.
Yako maandiko kadha wa kadha ambayo watu wanayatumia kuhalalisha unywaji wa pombe na wengine wanajiita ni wachungaji, wainjilisti, maaskofu, mapadri, mitume na manabii lakini kwa bidii wanafundisha hivo kuwa kunywa pombe hakuna shida yeyote.
Yako maandiko katika biblia zetu ambayo yanaonekana kuwa na utata kuhusu suala la kunywa pombe. Moja ya maandiko hayo ni haya yafuatayo;
Kumbukumbu 14:26, Mhubiri 9:7, Mwanzo 27:28 na mengine ambayo tutayaona mbele.
Tuone basi hayo maandiko yanamaana gani?
Ni muhimu sana kufahamu kuwa biblia zetu zimetafsiriwa kutoka katika lugha mbili kiebrania na kiyunani. Lugha hizi mbili ni lugha ambao msamiati wake ni mpana sana tofauti kwa mbali na kiswahili chetu.
Hivyo kama wanafunzi wa biblia hatuna budi kutafuta maana halisi ya maneno yaliotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili kutoka katika lugha hizi.
Katika kiebrania kwa mfano kuna maneno kumi ambayo yote katika kiswahili yanatafsiriwa kiholelaholela divai, mvinyo bila hasa kuzingatia uzito na maana halisi ya neno hilo katika Lugha ya asili.kwa ufupi maneno haya ni kama ifuatavyo;
1.TIYROSH(tee-roshe)
Hili neno katika kiebrania ni juisi iliokamuliwa kutoka kwenye zabibu ambayo haijachachuka. Katika biblia zetu kuna mahali wamejitahidi kueleza vizuri kwa kutumia neno DIVAI MPYA (mithali 3:10, ISAYA 65:8). Mahali popote Inapotajwa zaka za divai ni hii divai mpya(tiyrosh) inayozungumziwa, mfano katika( KUMBUKUMBU 14:23, WAAMUZI 9:13,NEHEMIA 5:11,N.K).
2.YAYIN
Yayin ni neno lingine ambalo katika kiebrania ni neno la jumla linalojumuisha divai iliochachuka na ile ambayo haijachachuka. Kwa mfana katika haya maandiko neno linalotumika hapo ni Yayin. (MWANZO14:18, 19:32-35,KUTOKA 29:40, MWANZO 27:25,37. MWANZO 49:11, KUMBU 14:26).
3.SHEKAR
Hili neno katika kiebrania ni kileo ambacho hakitokani na zabibu, kinatokana na mchanganyiko wa mmea wa shayir, asali na tende. Kuna maandiko Katika biblia zetu panatumika neno KILEO CHENYE NGUVU au STRONG DRINK kwa kiingereza lakini kwa sehemu kubwa linatumika neno kileo. Kwa mfano katika haya maandiko neno linalotumika ni shekar.(HESABU 6:3, 28:7, WALAWI 10:9, WAAMUZI 13:4,7,14, ISAYA 5:11,22, 24:9, 28:7,29:9,ZAB 69:12 n.k).haya yote kuna ole na katazo katika kutumia kileo sawasawa na maana halisi ya neno lenyewe maana shekar ni pombe halisi.
4. MAMSAK
Hii ni divai iliochachuka, ikaongezwa maji na kuchanganywa na viungo vingine mbalimbali.( MITHALI 23:30, ISAYA 65:11).
Yako maneno mengine kama, CHEMER, CHAMAR, GATH,YEQEB,ASIY ambayo yanaeleza namna mbali mbali ya vinywaji vitokanavyo na zabibu.
Kwa hio Katika kutoa tafsiri yeyote ya maandiko ni muhimu sana kujua katika Lugha ya asili ni neno lipi limetumika hapo na linamaanisha nini.
Wako watu wengine wanasema Yesu alitengeneza pombe katika arusi ya kana ya galilaya, wanatumia andiko la YOHANA 2:9-10. Je ni kweli Yesu alitengeneza pombe, jibu ni hapana, ufunguo wa hilo andiko tunaupata katika mstari wa 11, unasema,
"11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Yohana 2 :11.
Maandiko yanasema Yesu aliudhihirisha utukufu wake baada ya kufanya muujiza huo mkubwa wa kubadili maji kuwa divai njema.
Kulikuwa na mambo mawili katika nyakati za biblia kufanya jambo la kuudhirisha utukufu wa Mungu au Aibu. Angalia kwa mfano katika HABAKUK 2:15-16 "15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Habakuki 2 :15
16 Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.
Habakuki 2 :16.
Kama Yesu alifanya vile akaudhihirisha utukufu wake wala sio aibu, ni dhahiri kabisa haikuwa pombe. Yesu kamwe hakutengeneza pombe.
Andiko lingine ni 1TIMOTHEO 5:23, Ambalo wanalitumia kusema tunywe pombe kidogo.
"23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara"
1 Timotheo 5 :23
Kinachotajwa hapo ni mvinyo kama dawa ya tumbo, ni tofauti na leo watu hawaendi kunywa gongo, kangara, pombe yeyote kwa sababu wanaumwa wanataka dawa.
Nyakati za biblia hakukuwa na visima vingi virefu vya kupata maji safi kiasi kwamba vile vilivokuwepo vilirithiwa kizazi hadi kizazi na kutunzwa ili visiharibiwe (YOH 4:12)
"12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
Yohana 4 :12.
Wengine walilazimika kwenda umbali mrefu kupata hayo maji masafi, wengine vijana wakawa wanawavizia watu wanaotoka kuchota maji na kuwaibia, kwa hio wizi wa maji ulikuwa wa kawaida MITHALI 9:17 "
Wengi sasa walilazimika kuchimba visima vyao vya karibu lakini maji yake yalikuwa machafu na yakawa yanawasababishia magonjwa ya tumbo, akiwemo timotheo.
Katika Andiko hilo sasa paulo Mtume anamweleza timotheo atumie mvinyo,dawa sio anywe pombe kidogo asilewe.
Nyakati za biblia uko mvinyo uliotumika kama dawa, tunaliona hili katika LUKA 10: 30-37 "30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang'anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.
Luka 10 :30
31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
Luka 10 :31
32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.
Luka 10 :32
33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,
Luka 10 :33
34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
Luka 10 :34
35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
Luka 10 :35
36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang'anyi?
Luka 10 :36
37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.
Luka 10 :37.
Hata kama hatuelewi sana maandiko lakini tunaweza kujua kitu hiki ni dhambi kwa kuangalia kanuni tu. Tunafundishwa kanuni katika MATHAYO 7:17-18 17 "Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
Mathayo 7 :17
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
Mathayo 7 :18.
Kwa msingi huo sasa pombe ni kitu kiovu,sio mti mzuri tunapoangalia matokeo ya ulevi. Kwa mfano angalia baadhi ya matokeo ya ulevi
MWANZO 9:20-21.
MWANZO 19:30-36.
WALEVI WOTE HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU , Huyo Padri, Mchungaji, askofu, mtume, nabii, anaekwambia kuwa unaweza kunywa pombe tu hamna shida,HANA MBINGU ,sikiliza neno hili,ACHA POMBE UTUBU LEO,WALEVI HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU KAMWE
9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
1 Wakorintho 6 :9
10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
1 Wakorintho 6 :10.
Yesu Anarudi, Rekebisha njia zako.
Na Isaiah Membe.
No comments:
Post a Comment