Tuesday, January 16, 2018

WAJIBU WA RUNGU, NA SILAHA ZA VITA

WAJIBU WA RUNGU NA SILAHA ZA VITA

Nyakati hizi za mwisho mwisho kabla ya kanisa kunyakuliwa, tunahitaji kuelewa na kujua Sana wajibu wetu kwa Mungu.

Iko vita kali ambayo inaendelea kati ya Mungu na shetani.Mungu anataka kuendelea kulisafisha kanisa lakini pia ajipatie watakatifu wengi kote duniani, lakini upande wa pili shetani nae anataka kuhakikisha Mungu anapata hasara kwa kuwafanya wengi wajikwae na kuiacha imani kabisa.

Maandiko yanasema shetani ameshuka mwenye ghadhabu nyingi, akijua wakati wake ni mchache sana.UFUNUO 12:12.

MUNGU wetu anaitwa Bwana wa majeshi; Bwana wa vita; Ni Bwana wa majeshi yote ya Mbinguni na duniani{ AMOSI 9:5, ZEKARIA 2:8,3:7, MALAKI 3:7. Mungu aliyatumia majeshi yake ya Mbinguni kumtimua aliekuwa malaika mkuu Mbinguni,Ambae ni shetani leo na malaika zake{ UFUNUO 12:7-9}.

Mungu, Ambae ni Bwana wa vita anapigana vita Na shetani alietupwa hapa duniani,  kwa kutumia silaha vilevile ambao sasa si Malaika. Maandiko yanasema katika YEREMIA 51:20-24.

20 Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; …
Yeremia 51 :20.

Maana yake silaha ambazo Mungu anazitumia Leo ni mimi na wewe ambao tumeokolewa.

Jaribu kujiuliza,

wanaokwenda Jehanamu ni wengi sana, Walioko dhambini ni wengi vilevile, LAKINI tunajua kuwa Mungu ni mwenye  Nguvu kuliko shetani Wakati wote.

Kinachomkwamisha Mungu kupata matokeo mazuri ni silaha anazozitumia ambazo ni mimi na wewe,

Mtu anaweza kuwa na nguvu nyingi akawa mpambanaji sana LAKINI kama atakuwa na silaha dhaifu ambayo haifanyi kazi, atajikuta anashindwa na mtu ambae hakuwa na nguvu kama Yeye ila alikuwa ana silaha inayofanya kazi.

Shetani anahakikisha watumishi wake ambao ni wachawi, wanafanya kazi kwa bidii sana ndio maana inaonekana ni kama anakuwa na matokeo mazuri, anafanikiwa kuwafanya wengi kuwa walevi, makahaba, wazinzi, na uchafu mwingine wote.

Sisi ni silaha za vita tumepewa mamlaka, Yesu katika huduma yake duniani,alikusudia kuzunguka kote kote ila hakuweza LAKINI ALIWAPA WANAFUNZI WAKE MAMLAKA NA KUWATUMA WAENDE KULE AMBAKO YEYE HAKUWEZA KWENDA, Matokeo yalikuwa mazuri sana kwa sababu walijua wajibu wao, kwa sababu hio walirudi kwa furaha {LUKA 10:1,17}.

Hata leo mamlaka hio ipo kwetu, ni suala la kujua tu kuwa sisi ni silaha za Bwana na kuwa tayari kutoka.

Kama tukiona hakuna matokeo ya wazi kabisa ,tujue bado hatujajua wajibu wetu kama silaha za Bwana, na upande wa pili watatushinda kwa sababu wanajua wajibu wao kama silaha za Yule mwovu.

Mungu haangalii udhaifu wako, labda ni mtoto mchanga umeokoka karibuni, wala vyovyote ulivyo, Mungu anataka ujue tu wajibu wako wakati wote,Yeye Mwenye Nguvu akikushika wewe kama silaha USHINDI NI LAZIMA.

DAUDI alimshinda Goliath kwa sababu alijua wajibu wake mbele za Bwana  NA Mungu akamtumia Daudi kijana mdogo sana mbelw za Goliath.{ 1SAMWELI 17:38-50}

KAMA ULIKUWA UMELALA, AMKA KUTOKA USINGIZINI

KAMA ULIKUWA UMEKUFA, FUFUKA LEO, Bwana anataka kukutumia wewe.

Ukijua wewe ni Rungu, na silaha za Bwana Bwana za vita, UTAONGEZA MAOMBI, KUZIBOMOA KAZI ZA SHETANI, Utaongeza bidii kuhubiri injili popote unapopata nafasi, nakadhalika nakadhalika.

HAKIKISHA BWANA ANAPATA USHINDI KUPITIA WEWE WAKATI HUU WA KUMALIZIA NA shetani UNAMPA HASARA KUBWA.

No comments:

Post a Comment