Neno la Msingi: LUKA 2:10-11
"10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
Luka 2 :10
11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana."
Luka 2 :11.
Sababu ya Yesu kuacha Enzi, Utukufu na Mamlaka ili aje duniani azaliwe kama mwanadamu kwa ajili ya kutukomboa sisi wanadamu ambao tulikuwa tumepotea katika dhambi{YOHANA 1:29}
Nikupongeze wewe ambae tayari umeisikia sauti ya Yesu na kuokolewa na kuwekwa Huru mbali na dhambi, HONGERA SANA. endelea kushikamana na utimilifu wako siku zote.
Zimesalia siku chache tu ili kusherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo mwokozi wetu, Lakini pamoja na kusherekea yako mambo machache hapa ya kuangalia na kujifunza.
Wako watu wanajiita wakristo duniani kote ambao bado hawana Ushindi juu wa dhambi kimsingi hawajaokoka! Watu hawa pamoja na kusherekea Lakini bado ni watumwa wa dhambi sana, Huyu Mwokozi,YESU KRISTO wanaedai kumsherekea bado hawajakutana bae katika maisha yao,KWA HIO KWAO NI DESTURI NA MAZOEA KUSHEREKEA CHRISTMAS.
Rafiki, najua unajiandaa, unajipanga kusherehekea Kuzaliwa kwa Yesu, lakini kama wewe bado ni mtumwa wa dhambi, unakuwa huna hasa sifa za kusherekea sikukuu hii.
Tunasoma katika, YOHANA 1:4-5.
"4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Yohana 1 :4
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza."
Yohana 1 :5
Yesu Kristo ni Nuru ambayo inang'aa gizani SASA Kama wewe bado ni mlevi, mvuta sigara, mzinzi, mwasherati, mwizi, jambazi, tapeli, NA DHAMBI NYINGINE YEYOTE, jua bado uko gizani, Kwa shetani maana yake ni Muongo wewe kusema unamsherekea Mwokozi ambae bado hajakuokoa, MAAAN HAKUNA MAPATANO KATI YA GIZA NA NURU.
Unajua mipango uliopanga katika msimu huu wa sikukuu, umepanga mengi ambayo ni machafu sana mbele za Kristo Mwokozi.Yamkini umepanga kwenda disco na kumbi mbalimbali za starehe, yamkini umepanga kwenda Guest fulani na dada au mke wa mtu kufanya nae uzinzi na mengi yanayofanan na hayo. MIPANGO YAKO YOTE BWANA ANAIJUA.
Rafiki, Kabla ya kusherekea sikukuu hii jihoji na kutafakari maisha yako mbele za Mungu Alie Hai. Mwenendo wa maisha yako unampendeza Bwana? Au katika kusherekea Kuzaliwa Mwokozi ndio unamhuzunisha zaidi kwa kufanya uchafu wa kila namna.
Ukigundua tu hauna uhusiano Mzuri na Mungu, tafuta uhusiano mzuri na Mungu mapema kabla ya Christmas Maana Mungu bado anampango mzuri na wewe!{YEREMIA 29:11}
MPANGO WA MUNGU WA WOKOVU KWAKO AMBAE BADO NI MTUMWA WA DHAMBI, TUNAPOELEKEA CHRISTMAS HII.
1. Lisikie NENO la KRISTO {WARUMI 10:17}
2. Liamini NENO la KRISTO {YOHANA 8:24}.
3. TUBU dhambi zako Zote Kwa Kumaanisha kabisa kuziacha {LUKA 13:3}
4. Ubatizwe {Marco 16:16}
5. DUMU Kuwa MWAMINIFU kwa BWANA.{UFUNUO 2:10}.
CHRISTMAS HII ITAKUWA NA MAANA KUBWA KWAKO IKIWA UTAKUWA MIONGONI MWA KUNDI LA WATAKATIFU WALIOOSHWA NA KUSAFISHWA DHAMBI ZAO KWA KUZALIWA UPYA MARA YA PILI KATIKA ROHO..
#MAY_GODS_BLESSINGS_BE_YOURS_THIS_CHRISTMAS
#Merry_Christmas_All_Friends.
#Remember_to_be_holy_JESUS_is_coming_soon.
No comments:
Post a Comment