2Nyakati 6:6.
MUNGU muumba mbingu na nchi ni MUNGU anaeujua mwisho tokea Mwanzo, upinzani wote huu unaonekana baada ya Raisi wa Marekani, Donald Trump anaetumuwa na MUNGU kuutambua JERUSALEM kama mji mkuu wa Israel, Ni vitu ambavyo vilitabiriwa zamani sana Miaka zaidi ya 2700 kwa neno la BWANA kwa vinywa vya manabii.
Kinachoendelea sasa juu ya mji wa YERUSALEM kinatimiza unabii katika kibabu cha ZECHARIA 12:1-3.
Kunakuwa hapo na harufu ya vita kali ambayo itawaka dhidi ya Israel, ambayo pia katika unabii inatajwa katika KITABU CHA EZEKIEL, Ambacho vilevile kimeandikwa miaka 2700 iliopita , EZEKIEL 38:1-23, EZEKIEL 39:1-16. Mataifa ya URUSI(Gogu), Uturuki(magogu), Mataifa ya Kiarabu, Iran wakisaidiwa na china ambalo lina jeshi la watu milioni 200(kama inavyotajwa katika UFUNUO 9:16),Mataifa yote hayo yatainuka Kupigana na Israel.
ISRAEL Toka Mwaka 1948, imepigana vita kubwa Nne,Ambazo wakati wote mataifa zaidi ya matano yalikuwa yanaungana kuikabili ISRAEL, LAKINI wakati wote iliwafutilia mbali maadui zake kwa ushindi mkubwa,HII NI KWA SABABU MUNGU YUKO UPANDE WA ISRAEL.
Na Mungu Ambae ni BWANA wa MAJESHI anasema yeyote anaeigusa ISRAEL anaigusa mboni ya jicho lake, ZECHARIA 2:7-8.
Kama tunavosoma katika biblia, Mungu akiitetea na kuipigania ISRAEL, HATA SASA MUNGU bado ataishindia ISRAEL na mataifa haya yatachakazwa vibaya.
Swali la kujiuliza: KUNA MIJI MIKUU MINGI SANA DUNIANI, LAKINI KWANINI NI YERUSALEM PEKEE YAKE NDIO INALETA SHIDA NA KUITIKISA DUNIA YOTE?
YERUSALEM, ni mji wa MUNGU alie HAI, ambao miaka zaidi ya 3000 daudi aliuanzisha na BWANA mwenyewe kauchagua ili jina lake liwe humo,(2NYAKATI 6:6).
YESU KRISTO mwokozi wa ulimwengu alifia YERUSALEM, AKAPAA KWENDA MBINGUNI KUTOKEA YERUSALEM na YESU atarudi tena YERUSALEM, KUUTAWALA ulimwengu wote kwa miaka ELFU.
Yerusalem ina maana kubwa sana katika Mambo ya rohoni, NDIO MAAANA MATAIFA HAYA yote Yasio na Mungu wa Kweli yanahangaika sana inapotajwa YERUSALEM.
nabii Yoeli anasema katika YOELI 3:17
17 Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
Yoeli 3 :17.
KWA SABABU HIO UKISHINDANA NA KUIPINGA YERUSALEM, UNASHINDANA NA MUNGU MWENYEWE..HUWEZI KUBAKI SALAMAAA!!!!!!
Yesu ni Mungu wa kweli, Muamini Leo utakuwa salama mbali na maangamizo yanayokuja ulimwenguni muda ambao si mwingi ujao.
#Prepare_the_Way_Jesus_Is_Coming_Soon
#Maranatha
#Isaiah_Membe ▶0764569023.
No comments:
Post a Comment