NINI MAANA HALISI YA KUFUNGA.
wako baadhi ya watu Katika kipindi cha KWARESMA kwa mujibu wa imani yao huwa wanakuwa wanafunga kwa namna fulani fulani, lakini yako mambo ya kujifunza hapa⤵⤵
Neno “KUFUNGA“ linatokana na neno la Kiyunani “NESTEVO“, ambalo nalo linatokana na maneno mawili ya Kiyunani “NE“ na “ESTHIO“. Neno “NE“ maana yake “BILA“ au “HAPANA“, Kiingereza “NO“ au “WITHOUT“. Neno “ESTHIO“ maana yake “KULA CHAKULA AU KINYWAJI“, Kiingereza “TO EAT SOLID OR LIQUID FOOD“.
Neno “NESTEVO” sasa linaunga maneno hayo mawili ya Kiyunani ”NE” na “ESTHIO”, na lina maana “BILA KULA CHAKULA AU KINYWAJI CHOCHOTE”.
➡ Hivyo maana ya kufunga, ni “BILA KULA CHAKULA AU KINYWAJI CHOCHOTE”.
Kufunga siyo kuacha kusoma gazeti ulilozoea, kuacha kuchana nywele n.k., ni kuacha kabisa kula au kunywa kinywaji chochote. Maana hii ya kufunga, inathibitishwa na maandiko yafuatayo:- EZRA 10:6; YONA 3:7; 2 SAMWELI 3:35; ESTA 4:16; KUMBUKUMBU LA TORATI 9:9; MATENDO 9:9.
Kufunga siyo kuacha kula vyakula kama ugali au wali halafu ukawa unakunywa soda, maziwa, uji au kula matunda n.k. Ni kuacha kula chochote wala kunywa chochote kile. Andiko linalotumika kuhalalisha kula vitu vidogo vidogo ni DANIELI 10:2-3. Katika andiko hili “SIKULA CHAKULA KITAMU”, chakula kitamu ni “DESSERTS” kwa Kiingereza au “PUDDING” – ndizi, nanasi, papai, machungwa n.k.
✔ Katika mistari hiyo Danieli anasema hakula lolote kabisa.
✔ Katika mistari hiyo Danieli anasema hakula lolote kabisa.
Kwa hio kama tunafunga lazima kuacha kula kwa muda fulani kulingana na ratiba yako kuwa unafunga kwa muda gani, masaa 12, 24 n.k.
™Neno from Bishop Zachary kakobe.
No comments:
Post a Comment