Somo no 3:NENO KWA MCHUNGAJI-USILIFANYE KANISA KUWA PANGO LA WANYANG'ANYI.
Kama wachungaji lazima tufahamu kanisa tunalolichunga sio letu, kanisa ni la Yesu Kristo mwenyewe(Mathayo 16:18)(Waebrania 13:20)
Yesu Kristo anaitwa mchungaji mkuu, na wachungaji wako chini ya mchungaji mkuu(Yohana 21:15-17), hivyo tunavyolisha wanakuwa sio kondoo wetu bali kondoo ni wa Yesu Kristo aliye Mchungaji Mkuu na kanisa ni lake.(hivyo hakuna mtu kusema kanisa langu, kondoo wangu, huduma yangu).(1wakorintho 3:10-11). Wachungaji wanatakiwa kujenga kanisa juu ya msingi uliokwishawekwa yaani (Yesu Kristo) na sio misingi yetu tunayoijua wenyewe.
(1Timotheo 4:1).Nyakati za mwisho sio tu washirika lakini wapo hata wachungaji watakaojitenga na imani, kuna roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani ambayo yamezifanya nyakati hizi kwa wachungaji wanaochunga kanisa kuwa hatarini, na moja ya roho hizo ni roho ya mashindano.
Wachungaji watashindana na kusema kanisa langu ni kubwa kuliko makanisa yote Tanzania, Afrika mashariki n.k. Wanashindania idadi ya watu(umati).
Nyakati hizi ni rahisi kwa mchungaji kupata umati wa watu na ni kutokana na msingi alioweka katika kujenga kanisa.
(2 Timotheo 4:1-5)Nyakati hizi za mwisho kutakuwa na kundi kubwa la watu ambao wanatafuta kusikia yale wanayotaka wao na sio yale Mungu anataka, hawataki kusikia kweli(mafundisho ya uzima) wanataka hadithi za uongo, na kama wakipata mchungaji aliye tayari kuwadanganya watamfurahia na kumpenda na hivyo watamgeukia(watavutika)
(Isaya 30:8-10), nyakati hizi za mwisho wachungaji tukiingia kwenye mtego na kuhubiri maneno laini au hadithi za uongo ili kuwavuta watu, tunaweza tukawa na watu wengi, tukawa maarufu sana,tukatajwa kila kona lakini hatimaye siku ile ya mwisho tukajikuta tumeachwa.
(MATHAYO 21:12-13)Kuhibiri hadithi za uongo ili kuwavuta watu ni kulifanya kanisa kuwa pango la wanyang'anyi.
(LUKA 10:29-37)Nyakati za biblia kulikuwa na mapango ya wany'anganyi(ambayo leo yanaweza kuitwa magheto, masikani,vilingeni n.k) na yalikuwa ni mashimo yaliyochongwa kwenye mawe milimani kwa juu ili kuwavizia watu na kuwapora, wakiwa kwenye mapango inakuwa rahisi kuwaona watu wakiwa wanashuka kutoka milimani na kuona ana nini na kujipanga kumpora, ndio mfano wa yule mtu aliyekuwa akishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko akawa anaonekana na wanyang'anyi hawa wakiwa kwenye mapango yao akaporwa kila kitu na akapigwa sana karibu ya kufa akaja kusaidiwa na msamalia mwema. Watu hawa walio katika pango wanakuwa ni watu waovu, wauaji, wahuni,wakabaji, wabakaji, walawitiwavuta bangi, na uchafu wa kila namna unaukuta ndani ya pango la wanyang'anyi.
Yesu anaposema nyumba yangu sio pango la wanyang'anyi anamaanisha sio mahara pa watu waovu bali ni karakana ya kubadirisha watu maisha yao, na kimsingi kanisa ni la watu waliookolewa (Matendo 2:47).
Kanisa la Kristo vilevile ni kanisa la wazaliwa wa kwanza ambao majina yao yameandikwa mbinguni (Waebrania 12:22-23)
(Zaburi 50:16-22) Kwanza mchungaji kabla hajasimama kuhubiri lazima yeye mwenyewe awe amezaliwa mara ya pili(awe ameokoka), awe mbali na dhambi, kuhubiri injili kunafananishwa na kufanya biashara,Yesu anasema tufanye biashara hata ajapo(Luka 19:13) tunaitangaza biashara, na biashara yenyewe tunatangaza kwamba kuna kifaa cha kusafisha mioyo, tunawezaje kutangaza biashara hiyo wakati sisi mioyo yetu ni michafu, tunawezaje pia kutangaza juu ya sabuni(Yesu) kwamba inasafisha wakati mavazi yetu ni machafu?
Kwa hiyo wachungaji kwanza tutubu dhambi zetu ili nasi tuwe safi na tuzaliwe mara ya pili na hapo ndipo tunapopata uwezo wa kushinda dhambi (warumi 1:16) maana Sauli alibadirishwa akawa Paulo Mtume
Lazima tufahamu pasipo utakatifu hapana mtu atakayemuona Mungu(1Timotheo
1:12-15)(Tito 3:3-6).
(Waebrania 12:14)(1 petro 1:15-16) (Mathayo 5:48). Mungu amewaweka wachungaji katika kanisa ili kuwakamilisha watakatifu wafikie cheo na kimo cha utimilifu wa Kristo na huu ndo msingi uliowekwa ambao wachungaji wanatakiwa kujenga kanisa juu yake (Waefeso 4:11-15) (Yohana 15:3). Neno ambalo linatakiwa kufundishwa ni neno la usafi ili kuwafanya hao wanaolishwa hilo neno kuwa safi na wanapelekwa hatua kwa hatua ili wafike cheo na kimo cha utimilifu wa Kristo, na kama wachungaji hawazingatii hili wanajenga kanisa lao na sio la Kristo, hata kama mchungaji akiwa na jina kubwa sana siku ile ya mwisho atakataliwa (1wakorintho 2:10)
(1 Wathesalonike 1:7)(Ufunuo 21:7)(2Timotheo 2:19)
Msingi wa mahubiri ya wachungaji yanatakiwa kuwa ni mtu kuacha uovu na si vinginevyo.(Ufunuo 3:16)
(1Petro 5:1-4) Wako wachungaji wanaitwa matajiri wakubwa lakini wamejipatia fedha ya aibu, wanaombea watu kwa pesa, wanahubiri hadithi za uongo ili watu wajae watoe sadaka
(Daniel 12:3) (Ufunuo 3:17).
(Matendo 8:18-24)Wachungaji wengi wanaonekana ni matajiri, na wengine wanadhani kufanikiwa ni kuwa na magari, majumba, matreni, mandege n.k,wanaweza wakawa na vyote hivi lakini vikawa vimetokana na fedha ya aibu,.
Paulo aliogopa kwamba asije akawahubiri wengine na yeye mwenyewe akawa mtu wa kukataliwa( 1wakorintho 9:27).
Wachungaji nao watasimama nao mbele za Mchungaji Mkuu kutoa hesabu za kazi walizozijenga(Waebrania 13:17)
Wako wahubiri wanafanya deal na watu kwamba waonekane wanaombea watu na wanapokea miujiza, lakini ni miujiza ya kutengeneza, iko mifano mingi ya wahubiri wanaolipa watu pesa ili waseme wamepokea miujiza lengo hasa ni kuwadanganya watu waonekane wana upako ili wavute watu wengi zaidi(Waebrania 1:9),upako wa mchungaji haupimwi kwa miujiza anayofanya bali unapimwa kwa jinsi ambavyo anachukia dhambi(maasi) na kuyakemea na kufundiaha haki.
Kanisa la Kristo halikujengwa kwenye miujiza, Historia ya biblia inasema muda Yesu alioutumia kufanya miujiza ni sawa na siku 21(usiku na mchana)(yohana 6:26-27) muda mwingi aliutumia kufundisha neno la usafi na utakatifu(Waebrania 13:20-21)(Yohana 6:60-61, 66-68) Maneno ya uzima yanaweza yakawa magumu yakamfanya mtu akimbie lakini tusishushe viwango, na ikiwa wachungaji watahubiri kweli walio wa Kristo watakaa(Yohana 16:13)(1yohana 2:19)(Luka 6:26)(Mathayo 18:6-7)
(Yakobo 3:1)..kule motoni kuna adhabu kwa madaraja, ataanza shetani atakuja nabii wa uongo na mpinga kristo, watafuata malaika walioasi kisha watafuata walimu wa uongo wanaodanganya watu mana kuna adhabu kubwa kwa walio walimu, (1wakorintho 2:13-15)
(Yohana 5:41, 44) Mchungaji anatakiwa atafute utukufu kwa Mungu na sio wa wanadamu.
#BishopKakobe
Imeandikwa na Fredie Haule
No comments:
Post a Comment