Wednesday, January 17, 2018

TOFAUTI YA UNYAKUO NA KUJA KWA YESU MARA YA PILI.

TOFAUTI YA KUJA KWA YESU WAKATI WA KUNYAKULIWA KANISA NA  KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.

Wako watu wengi sana wanachanganya matukio haya mawili kiasi cha wengine kudhani kuwa kanisa litakuwepo wakati wa dhiki kubwa.

Matukio haya ni tofauti sana;

KUJA KWA YESU WAKATI WA KUNYAKULIWA KANISA
🔹Hapa Bwana Yesu atakuwa anakuja kama Bwana Arusi kumchukua bibi harusi ambalo ni kanisa takatifu lisilo na doa,waa wala kunyanzi (EFESO 5:27, YOH 14:1-3).
🔹Yesu atakuwa anakuja kukutana na watakatifu wake mawinguni. Yesu hatakanyaga juu ya uso duniani huu wa kunyakuliwa kanisa, walioko duniani hawatamwona wakati huu (1WATHEEALONIKE 4:17).
🔹Kunyakuliwa kwa kanisa ni kabla ya dhiki kubwa kuanza duniani(UFUNUO 3:10, LUKA 21:22-23,34-36, 1Wathesalonike 1:10).

KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
Mara ya kwanza Yesu kuja duniani ni pale alizozaliwa kama mwanadamu na akaishi kimaskini hadi alipomaliza kazi yake duniani na kurudi mbinguni. Mara ya pili atarudi kama Bwana wa Mabwana na mfalme wa wafalme.
🔹Hapa Bwana Arusi Yesu kristo atakuwa anakuja pamoja na bibi Arusi(watakatifu) aliowanyakua miaka saba iliopita kwa lengo la kutawala( YUDA 1:14,UFUNUO 1:7.)
🔹Wakati wa kuja Yesu mara ya pili duniani, atakuja na kukanyaga katika mlima wa mizeituni mahali pale alipoondokea alikuja mara ya kwanza duniani. Kila jicho la watakaokuwako duniani watamwona(ZEK 14:4-5, MAT 24:27).
🔹Kuja kwa Yesu mara pili duniani ni mara baada ya dhiki kubwa kuisha au kumalizika duniani (MATHAYO 24:29-30, 2WATHESALONIKE 2:1-4).

Bwana awabariki wote!!

No comments:

Post a Comment