Wednesday, January 17, 2018

GOATU

JE, UNAJUA G.O.A.T.U. NI NINI?

✔Wanachama wa Kikundi cha siri cha freemason wanamwabudu mungu
anayeitwa GAOTU – Great Architect Of The Universe – yaani ‘Mbunifu mkuu wa
ulimwengu.’ Freemason hawamwabudu Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Sala zao zote huelekezwa kwa GAOTU.

✔Architect ni mtu anayebuni ramani za majengo,
majengo unayoyaona katika nchi mbalimbali yakiwemo yale yaliyomo ndani ya miji ya
nchi yetu, yanatokana na ubunifu wa watu wanaoitwa Architects. Ni watu wenye elimu
kubwa sana kuhusu mambo ya ubunifu na ujenzi wa majengo.

✔Freemason nao ni
wajenzi wa maadili wanayoyataka wao na pia wanaye Architect (mbunifu) wao mkuu
ambaye ndiye wanayemwabudu, jina la Architect wao ni GAOTU. Huyo ndiye mbunifu
mkuu wa shughuli za Freemason katika ujenzi wa ulimwengu, wengine ni
watekelezaji tu.

✔Wapo watu pia wanaoelekeza sala zao kwa viumbe badala ya kuelekeza kwa Muumbaji. Wao pia hawatofautiani na Freemason maana wote
wanakwenda kinyume na Mungu, na ukweli ni kwamba wanafanya hivyo kutokana na ubunifu wa GAOTU
maana kazi yake ni kubuni mbinu mbalimbali za kuwafanya watu wawe mbali na Mungu.

✔ Yesu anasema kwamba tunapotaka kusali tusali hivi, “Baba yetu uliye
mbinguni……” Mathayo 6:9-13, ikimaanisha kwamba sala zetu zote tuzielekeze kwa
Mungu aliye mbinguni tena kwa Jina la Yesu.
➡ GAOTU anajua kwamba Mungu alisema,
“mtu akijikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote” Yakobo 2:10, ndio maana
anajitahidi kuwafanya watu wamkosee Mungu hata katika kitu kidogo, na watakuwa wamemkosea juu ya yote. Hivyo unaweza ukawa mlokole, msabato, mkatoliki,
muislamu, mbudha, myahudi nk. lakini ukimkosea Mungu katika jambo moja tu
umemkosea juu ya yote.

✔Ndio maana leo hii katika dunia nzima kuna utitiri wa
madhehebu na dini za kila aina. Wataalamu wanasema kuna dini zaidi ya elfu tatu! Je,
wote watakwenda Paradiso? Biblia inasema, “Je! Hamjui ya kuwa wale washindanao
kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja?” 1 Wakorintho
9:24. Hivyo pamoja na kuwa na dini nyingi kiasi hicho na dini zote zikiwa zinadai
kupiga mbio ili kupata tuzo ya uzima wa milele, ni wale tu wanaotii kila moja ya amri za Mungu ndio wanaopiga mbio vizuri na ndio watakaopata tuzo, nao watatoka katika dhehebu moja tu.

✔Kwa nini watu huingia Freemason? Ni kwa sababu ya kutaka utajiri wa dunia hii.
➡Wakati shetani anamjaribu Yesu, alimwonyesha utajiri, “Kisha ibilisi akamchukua
mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.” MATHAYO 4:8, 9.
✔Baada ya ibilisi kushindwa kumnasa Yesu, sasa aliendelea kutumia njia hiyo hiyo kwa kumtumia mnyama ili awape watu utajiri kupitia Freemason, ➡tunasoma kwamba, “Lakini katika
mahali pake atamheshimu mungu wa ngome; na mungu ambaye baba zake hawakumjua
atamheshimu, kwa dhahabu na fedha, na vito vya thamani na vitu vipendezavyo…..na
yeye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataigawa nchi kwa rushwa.” Danieli 11:38,39. Ndio maana watu wengi wanaingia kwenye vyama vya siri kama Freemason na kila anayeingia humo hufanywa apate Kumiliki vitu vingi na kuwa tajiri mkubwa.
➡➡Ni sehemu ndogo ya neno la uzima kutoka kwa mtumishi wa MUNGU, ASKOFU ZACHARY KAKOBE. Ukitaka kulisoma somo hili kwa mapana na marefu na kufahamu siri nzito kuhusu FREEMASONS NA ILLUMINATI ingia kupitia link hii⤵⤵
➡www.davidcarol719.wordpress.com/freemasons-na-illuminanti/
UBARIKIWE NA BWANA.

No comments:

Post a Comment