Wednesday, January 17, 2018

KIONGOZI KIPOFU

UKIONGOZWA NA KIPOFU WOTE MTATUMBUKIA SHIMONI(KUZIMU).

Usikubali kuongozwa na kiongozi kipofu kabisa maana anakuongoza kwenda shimoni(kuzimu).MATHAYO 15:14

Mchungaji anaetumia jina la Yesu kwa maslahi yake binafsi ni kipofu mkimbie utaangamia nae. Mchungaji ambae macho yake yote yako kwenye mfuko wako ni kipofu toka kwake, uiponye roho yako. Mchungaji anaekwambia unaweza kuvaa vyovyote hakuna shida, huyo ni kipofu anakupeleka motoni.

Mchungaji ambae hahubiri juu ya dhambi wala hakemei dhambi, mahubiri take yote ni mafanikio  ya kimwili tu, huyo ni kipofu,anakuongoza kwenda motoni.
Mchungaji ambae hakufundishi juu ya unyakuo Wa kanisa na kukuweka tayari kujiandaa kumlaki Bwana Yesu, hakupendi in kiongozi kipofu. Mchungaji ambae hata haamini wokovu duniani ni kipofu huyo anakuongoza kwenda motoni.

Mchungaji ambae hakiishi anachokifundisha ni kipofu utaangamia nae. Mchungaji anaekwambia jipambe tu hakuna shida,Mungu haangalii ndani ni kipofu Huyo wala hana mbingu yake ya kukupeleka, anakuongoza kwenda motoni.

Mchungaji ambae ni mpiga dili anakuuzia vitambaa,sabuni, maji na mafuta ya upako, ni kipofu mkubwa huyo anakupeleka upotevuni. Mchungaji ambae hahubiri juu ya jehanam ya moto,anahubiri mafundisho laini yadanganyayo ni kipofu usipokuwa makini utaangamia nae. Mahali ambapo uko guru pamoja na dhambi zako hapakufai mahali hapo, kimbia..

Acha kufanya mchezo na roho yako wokovu ni Mara moja tu ukiupoteza hakuna SECOND CHANCE  maana MTU amewekewa kufa Mara moja tu na baada ya kifo ni hukumu.WAEBRANIA 9:27

Mungu anasema tokeni kati yao mkatengwe nao, Mara moja ukigundua kiongozi,Mchungaji anaekuongoza ni kipofu toka haraka kimbia uiponye nafsi na roho yako 2WAKORINTHO 6:14-18.

#utii ni bora kuliko dhabihu.

MARANATHA.

No comments:

Post a Comment