Tuesday, January 16, 2018

JIFUNZE KATIKA NDOA YA KWANZA!


JIFUNZE KATIKA NDOA YA KWANZA.

Tunajifunza katika kitabu cha Mwanzo, kuhusu ndoa ya kwanza kabisa kuwapo Duniani ambayo ni ndoa ya Adamu na Hawa.

MWANZO 2:15-18, 21-24.
Mungu kabla ya kufanya kitu anakuwa anaandaa mazingira kwanza kabla. 

Mfano;

1. Aliumba Maji kwanza kabla ya samaki.

2. Aliumba Ardhi kabla ya Mimea.

3. Alitengeneza bustani kabla ya Mwanadamu.

Vile vile kabla Mungu hajampa Adamu mwanamke, viko vitu ambavyo vilitangulia kwanza.Tuangalie vitu hivi kwa muhtasari.

✴Kitu cha kwanza Mungu alichokifanya kwa Adamu(mwanaume), Alimuweka katika Bustani ya Edeni. Neno Eden katika lugha ya Asili inamaana pana sana, Edeni inazungumzia uwepo wa Mungu.
 
Mwanaume anahitaji kuwa katika UWEPO WA MUNGU kwanza kabla ya Kuoa. wengine wanauacha uwepo wa Mungu wanaenda kutafuta mwanamke. Mwanamke anatakiwa akukute ukiwa tayari katika Uwepo wa Mungu. TULIA KWENYE UWEPO WA MUNGU.

✴Kitu cha Pili Mungu alichompa Mwanaume ni KAZI.

MWANZO 2:15.Mungu akamwambia Adamu ailime bustani na kuitunza. Vivyo hivyo MWANAUME anahitaji au anatakiwa kuwa na KAZI kwanza kabla ya kuwa na mke.

✴Kitu kingine, Mungu akampa Adamu neno.

MWANZO 2:16, ambalo ndio likawa agizo la Mungu kwa Adamu ambalo alitakiwa alitii wakati wote. Mungu hakumpa mwanamke neno Kabla ya Adamu. 

Mwanaume unatakiwa kuwa unalifahamu Neno la Mungu na kulitunza Kabla ya Mungu kukupa Mke.

KATIKA "MWANZO 2:18", Mungu akasema, "BWANA MUNGU akasema si vyema HUYO mtu(Adamu) awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae"

Hatupaswi kupasoma hapo haraka haraka tu, Mungu anasema SI VYEMA HUYO MTU(MWANAUME) AWE PEKE YAKE, MWANAUME YUPI???

Ambae,

1. Yupo katika Uwepo wa Mungu.
2. Tayari ana Kazi na Anafanya kazi.
3. Tayari Analo Na kulifahamu Neno La Bwana.

Kwa hio kama Mtu hayupo katika Uwepo wa Bwana, hafanyi kazi,halijui neno na maagizo ya Mungu,NI VEMA HUYO MTU KUWA PEKE YAKE.

Na Isaiah Membe: Mtumwa wa Kristo.

No comments:

Post a Comment