Friday, January 19, 2018

KUVAA WIGI NI KUABUDU SANAMU.

ANAE VAA NYWELE BANDIA(WIGI) ANAABUDU MIUNGU BILA KUJUA..

Kama ulikuwa hufahamu ni kwamba mawigi kwa asilimia kubwa yanatokana na nywele za wahindi.

Nywele hizi zinatokana na hekalu moja kubwa sana na maarufu sana India linaloitwa VENKATESWARA TEMPLE, ambapo wanamuabudu mungu(sanamu) wanaemwuita vishnu au lord balaji»» angalia www.tirumala.org«««.

Kinachofanyika sasa ni kwamba wahindi wengi hutoa sadaka nywele zao kwa hio miungu yao kwa  kunyolewa nywele zote na kuwekwa kwenye mapipa maalum, baadae  ndio zinanunuliwa na makampuni wa urembo kisha hutengenezwa wigi. Na wanasema katika mtandao makampuni haya kuwa wanatengeneza haya mawigi, kwa watu wanaojiona  duni vile Mungu amewaumba, ili wafunike nywele zao kwa kuvalia wigi juu yake.

BIBLIA INASEMA NINI JUU YA KUTOA SADAKA KWA MIUNGU

MUNGU anasema watu wanaotoa sadaka kwa miungu wanatoa kwa kwa mashetani na anatuonya vitu vyote vilivotolewa sadaka kwa mashetani tusivishiriki kwa namna yeyote {1WAK 10:14,19-22, KUM 32:17, ZAB 106;37}

Watu zaidi ya million 20 hukatwa nywele zao katika hekalu hilo kila mwaka, sasa emu tujiulize ni wanawake wangapi wanavaa hivo nywele bandia leo? Ni wangapi wanaingia makanisani na nywele zilizotolewa sadaka kwa miungu? Ni Mungu yupi wanaemwabudu, aliewapa nywele wakaona hazifai au wale miungu wanaotolewa sadaka za nywele?

Kwa kuvaa wigi hata kama umeokoka unajiungamanisha moja kwa moja na ibada ya miungu na wengi sana ni vipofu katika hili BWANA ATUSAIDIE KIZAZI HIKI,WENGI WANAPOTEA!!

Mwanamke nywele ni fahari (utukufu)kwako katika uhalisi wake 1WAK 11:15. Unapovaa nywele za mtu mqingine maana yake  unaungamanishwa nae katika ibada yake angalia KUMBUKUMBU 7:26. BWANA AKUPE UFUNUO ILI UTOKE KATIKA KUABUDU MIUNGU, NA UMUABUDU MUNGU ALIEKUUMBA HIVO ULIVO.

             GO NATURAL,AMEN.

Wednesday, January 17, 2018

KWAKO KIJANA-MUHIMU

KWAKO KIJANA;

Hii inakuhusu wewe kijana ulieokoka au ambae hujaokoka.tafadhali soma hadi mwisho kwa kutafakari.

Mtume Paulo katika waraka wake  kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye yote ASIUDHARAU ujana wako, bali uwe KIELELEZO kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.JITUNZE nafsi yako, na mafundisho yako. DUMU katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA’ (1Timotheo 4:12 & 14).
Sentensi hizi zinatuonyesha kwamba kijana yeyote ambaye amefanya uamuzi wa kuokoka, kwa hakika amefanya maamuzi ambayo yanamtaka amaanishe katika kumfuata kwake Yesu au kuuishi wakovu wake. Pamoja na kumpa Yesu maisha yake ni lazima kijana afanye maamuzi ya kuishi maisha ya kudumu kumpendeza Mungu kwa kuzikubali gharama zinazohusiana na wokovu aliouchagua na si kuishi maisha yenye kupelekea jina la BWANA kutukanwa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana wengi leo.
Ukisoma mstari huu wa 1Timotheo 4:14.

Jambo muhimu ambalo Mtume Paulo alikuwa akilisisitiza hapa ni hili; jambo muhimu si tu kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako, bali kila mwamini ana kazi kubwa ya kufanya ili KUULINDA NA KUUTUNZA WOKOVU WAKE.

Moja ya changamoto kubwa sana ambazo zinawakabili vijana wengi waliokoka leo ni kuipenda dunia. Kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana wengi na kwa sababu ya kuipenda dunia; 

(a) Mahusiano ya vijana wengi na Mungu wao yameharibika 
(b) Maisha ya vijana wengi yamekosa uelekeo 
(c) Kutokana na uovu wao jina la Bwana Yesu limekuwa likitukanwa.

Katika kile kitabu cha 1Yohana 2:16 ni dhahiri kwamba dunia imejaaTAMAA YA MWILI, TAMAA YA MACHO NA KISHA KIBURI CHA UZIMA. Tamaa ina nguvu ya kuvuta pamoja na kudanganya, naam inamuingiza mtu kwenye jaribu. Hii ina maana tamaa ni mlango, naam mlango huu unapaswa kufungwa mapema usikupoteze.
(Samweli 11:1-2). Hapa Tunaona anguko la Daudi lilisaabishwa na kumpa Ibilisi nafasi kwa kutokwenda vitani. Mkristo akipoa katika kuvipiga vita vya kiroho inakuwa rahisi kwake kuanguka dhambini (Yakobo 1:14-15), na kumbuka kwamba siku zote tamaa inalenga kumfurahisha mtu binafsi (self-pleasing) bila kujali matokeo yake.

Hivyo katika nyakati tulizonazo sasa suala la kuipenda dunia ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu miongoni mwa vijana wetu. Ujumbe huu mfupi unalenga kueleza kwa namna gani kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana na nini vijana wafanye ili kuikabili na kuishinda changamoto husika.
Pia katika  2Timotheo 2:15 Mtume Paulo anaendelea kumwambia kijana Timotheo ‘Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu,mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli’.

Pengine kila mmoja wetu atafakari maisha yake kwa kuhusianisha na maelekezo ya Paulo kwa Timotheo. Naomba jiulize na kujijibu kwa uaminifu kwamba mosi, je, ujana wako wako unaheshimika au unadharauliwa? Pili, je, kwa waamini wenzako umekuwa kielelezo cha kweli kwa habari ya imani, upendo, usafi, usemi na mwenendo au la?


Naam katika kusoma na kutafakari neno la Mungu nimejifunza kwamba zifuatazo ni njia ambazo zitatusaidia sisi vijana wa leo kuifikia kweli hii ya neno la Mungu.

1. Kijana adumu katika kuomba na kusoma (kutafakari + kulitenda) neno la Mungu.

Katika Zaburi 119:9 & 11 Biblia inasema ‘Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii AKILIFUATA neno lako’. Pia kwenye ule mstari wa 11 inasema ‘moyoni mwangu nimeliweka neno lako, NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI’.
Naam katika Mathayo 26:41 imeandikwa ‘Kesheni, mwombe, MSIJEmkaingia majaribuni; roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu’. Yohana 17:17 inasema ‘uwatakase kwa ile kweli ;neno lako ndiyo kweli. Mambo haya mawili yanapaswa kwenda kwa pamoja nakijana akidumu katika kuomba na kusoma neno la Mungu ushindi ni lazima.

2. Kijana asimpe Ibilisi nafasi.

Kijana anapaswa kujiuepusha na mazingira yenye kumfanya aiepende na kuifuatisha namna ya dunia hii.
Katika kitabu cha 1Wakorinto 6:12 imeandikwa ‘Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote VIFAAVYO; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya UWEZO wa kitu chochote’.  Ni vizuri ukahakikisha kwamba ufahamu wako hautawaliwi na mambo yasiyo ya msingi– Je ufahamu wako umetawaliwa ni nini??
Hii ndiyo sababu iliyomfanya Paulo awaambie Waefeso ‘Wala msimpe Ibilisi nafasi’ (Waefeso 4:27) na pia awaambie Warumi “Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili hata kuwasha tamaa zake’ (Warumi 13:14).
➡ Je hivi leo ni kwa namna gani vijana wanaungalia mwili na kumpa Ibilisi nafasi? – Mitandao ya kijamii, kuangalia na kusoma vitu vichafu, hasira, mawazo, mazingira.

Mfano wa Vijana
3. Kijana azikimbie tamaa za ujanani.

Katika 2Timotheo 2:22 imeandikwa ‘LAKINI ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi’. Kijana anawezaje kuzikimbia tama za ujanani?angalia mfano wa Yusufu. Ushindi wa Yusufu dhidi ya mke wa potifa (Mwanzo 39:2-9). 

Hii ni habari ya kijana Yusufu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mali za Potifa.
Pamoja na ushawishi aliokutana nao Yusufu alijibu kwamba ‘Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?’ Mwanzo 39:12 inasema ‘huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake akakimbia akatoka nje. Ili kuzikimbia tamaa za ujanani kijana anapswa,

(a) ajiepushe na mazingira/marafiki wabaya (Mithali 1:10 & 1Wakorinto 15:33).

(b) Ajitenge na uovu (Mithali 16:17, Zaburi 1:1).

Ni muhimu ukakumbuka kwamba hukupewa mwili kwa ajili ya zinaa maana miili yenu ni ni viungo vya Kristo na tena hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorinto 6:15 & 19), tena yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye (1 Wakorinto 6:17) maana tena imeandikwa ‘Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili’ (1Wakorinto 6:13b). Tena imeandikwa ‘Lakini uasherati USITAJWE kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu’   (Waefeso 5:3)
Rafiki, mkimbilie Yesu leo akuwezeshe kuishi maisha yanayompendeza maana unazo nguvu za kumshinda ibilisi.

  BWANA AWABARIKI SANA.

Na Isaiah membe, mtumwa wa Kristo.

KUWAOMBEA WATU KWA FEDHA

WANAPOTEA KWA KUWA HAWAYAJUI MAANDIKO-KUWAOMBEA WATU KWA FEDHA.
Yesu alisema nyakati za mwisho kutakuwako mitume na manabii wa Uongo MAT 24:24 ambao watapoteza wengi hata waliowateule. Lakini pia alisema watu watakuwa wenye kupenda fedha kuliko kumpenda Mungu, 2TIMOTHEO 3:1-2.

Lakini katika UFUNUO 2:2 anasema tuwajaribu hao wajiitao mitume ili tujue kuwa ni waongo au namna gani, Mungu pia anasema tuzijaribu hizo roho tuone kama zinatokana na Mungu au La! tunawapima kwa NENO LA MUNGU.

Kuna wimbi kubwa la watu ambao wanatajwa ni watumishi wa Mungu, wanafanya maonbezi kwa watu kwa kuwatoza fedha. utaskia Mambo kama haya;
*kumuona mchungaji sh.10000.
*kuombewa ugonjwa fulani Sh.100,000 na mengi yanayofanana na hayo!

Maombezi yote ya uponyaji wa kibiblia kamwe hayafanyiki kwa fedha {MATHAYO 10:7-8.}

Karama zote tunazozipokea kutoka kwa Mungu, Mungu anatupa bure kabisa hakuna anaemlipa Mungu ili apate karama yeyote ile.

Neno KARAMA kama linavotajwa katika 1wakorintho sura ya 12 katika lugha ya asili linamaanisha ZAWADI (gift of the holy spirit).
Zawadi mara zote inatolewa bure bila kuilipia chochote.

Wokovu pia ni karama ambao tunaupokea bure Inayotupa uzima wa milele. Ukisoma andiko hili la WARUMI 6:23 kwa kiingereza utaona neno, THE GIFT OF ETERNAL LIFE.
Tunahesabiwa haki bure katika kristo Yesu pekee, WARUMI 3:23-24.

Sasa mtu anaombea watu kwa fedha, inabidi na mtu akitaka kuokoka basi amtoze afanye hivohivo amtoze pesa pia. Kama haiwezekani na hawafanyi hivo wanapowataka watu waokoke, basi na uponyaji ni vilevile, inawapasa kuwaombea watu bure bila fedha yeyote {ZABURI 103:3}

Yeyote anaeombea watu kwa fedha sio mtumishi wa Mungu alie hai hata kama ni mtu HUYO anajiita nabii,mtume,askofu na jina lolote lingine.

Uponyaji wote Yesu kaulipia na kuugharamia kwa kazi alioifanya msalabani aliposema yote yamekwisha( IT IS PAID IN FULL).Uponyaji wa magonjwa yote umeshalipiwa ,huna haja ya kutoa fedha kwanza ndio uombewe. Kufanya hivo ni kutokuifahamu Kweli ya NENO.

Watumishi wa Mungu wa nyakati za biblia walikuwa hawaombei watu kwa fedha mfano:

NABII ELISHA ,2WAFALME 5:13-18,20-27.

MTUME PETRO, MATENDO8:9-24.

Na mitume wote na nyakati za kanisa la kwanza.

Acha kudanganywa na mitume na manabii Hawa feki ambao ni maajenti wa ibilisi, hawana tofauti na GEHAZI mtumishi wa elisha, wamejaa uongo mwingi sana, utaskia wanasema "Bwana amesema na mimi, unipe gari lako" "Bwana amesema nami unipe nyumba yako" na mengi tu mengine yanayofanana na hayo.

Maandiko yanasema hizi ni nyakati za hatari,wengi watajitenga na imani wakiskiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani 1TIMOTHEO 4:1, 2TIMOTHEO 3:1.

Itafute KWELI ya NENO la MUNGU, IKUWEKE HURU ili  usije ukachukuliwa na roho hizi za nyakati za mwisho.

Bwana akubariki sana.

Isaiah Membe,Mtumwa wa Kristo.

KIPIMO SIO KWENDA KANISANI.

KIPIMO SIO KWENDA KANISANI

Watu wengine siku za ibada kama Jumapili au jumatano, wanakuwa katika mambo yao wenyewe, wengine watakuwa bar, wengine shambani, wengine kwenye biashara zao nakadhalika. 

Kutokana na hili sasa wengi watawachukulia wale wanaokwenda kanisani kuwa ndio watu wa Mungu Na wale wasioenda ni watu wa shetani.

Lakini jambo hapa la kufahamu ni kuwa hata  katika kundi hilo la watu waendao kanisani kuna wengi pia ambao wako mbali sana na Mungu.
Wengine wanaenda kanisani kupotezeza Muda tu, wengine kutafuta wachumba, wengine kutafuta uponyaji, wengine kutafuta baraka tu nakadhalika.

Bwana Mungu anasema watu hawa wanaenda ibadani na hukaa kama watu wa Mungu lakini sio watu wanaompenda Mungu. EZEKIEL 33:30-33. MARCO 7:6.

Sikiliza kipimo si kwenda kanisani, kipimo sio kuhubiri wala kufundisha, Kipimo sio kujionyesha kwa watu kwa unafiki tu LAKINI  Kipimo ni kuishi MAISHA YAKO sawasawa na NENO la MUNGU.(ZABURI 119:6,9).

Wengi wa hao waendao makanisani hawalifurahii NENO la MUNGU, kwa sababu silo walilolifata hapo, hawataki kukemewa Maovu yao wala hawataki kuonywa KINYUME chake wanapenda MANENO LAINI YADANGANYAYO, ISAYA 30:9-11.

Wako wengi wanaenda kanisani lakini hawataki maisha yao ya dhambi yaguswe Kabisa katika mahubiri kwa sababu Ndani yao hamna kitu, wako kanisani kwa Lengo lingine kabisa!
Kuwa watu wa Mungu ni vile tunavolitii na kulifurahia  neno la Mungu (ZABURI 119,9,103), Vile tunavyokuwa Tayari kukemewa na kuonywa kwa Neno la MUNGU (ZABURI 119:105), Kuwa mtu wa Mungu ni jinsi gani tunavyonyenyekea na kuwa tayari kuongozwa na NENO la Mungu.

Ukisema unampenda Mungu wakati neno lake hulipendi  ambalo Ndilo hasa linalotusafisha na kututakasa (YOHANA 17:17), NENO ndilo linagusa maisha yako ya dhambi na kuweka wazi uchafu wote wa uovu na kutufanya Kutubu, KAMA HULIFURAHII NENO rafiki, HAPO hakuna kumpenda Mungu, 

kumpenda Mungu ni kuzishika amri zake YOHANA 14:21,23-24. wakati unakuja ambapo Magugu na ngano vitatengwa.Maana Yesu alisema yaacheni magugu na ngano vikae pamoja ila wakati unakuja atakapoyatenganisha magugu na ngano na hapo ndipo itakuwa wazi nani alikuwa MBUZI na nani alikuwa KONDOO, 

USIKUBALI KUWA katika kundi la Mbuzi au Magug,  Kama unaamua Amua kuwa mtu wa Mungu kweli kwa Kumaanisha kulishika Neno lake lote bila kuchaguachagua ya kushika na yanayokugharimu unayaacha.ZABURI 119:6,9,11,98-100.

Ubarikiwe sana.

Isaiah Membe,Mtumwa wa Kristo.

NINI MAANA HALISI YA KUFUNGA.

NINI MAANA HALISI YA KUFUNGA.

wako baadhi ya watu Katika  kipindi cha KWARESMA kwa mujibu wa imani yao huwa wanakuwa wanafunga kwa namna fulani fulani, lakini yako mambo ya kujifunza hapa⤵⤵

Neno “KUFUNGA“ linatokana na neno la Kiyunani “NESTEVO“, ambalo nalo linatokana na maneno mawili ya Kiyunani “NE“ na “ESTHIO“.  Neno “NE“ maana yake “BILA“ au “HAPANA“, Kiingereza “NO“ au “WITHOUT“.  Neno “ESTHIO“ maana yake “KULA CHAKULA AU KINYWAJI“, Kiingereza “TO EAT SOLID OR LIQUID FOOD“. 

Neno “NESTEVO” sasa linaunga maneno hayo mawili ya Kiyunani ”NE” na “ESTHIO”, na lina maana “BILA KULA CHAKULA AU KINYWAJI CHOCHOTE”.

➡  Hivyo maana ya kufunga, ni “BILA KULA CHAKULA AU KINYWAJI CHOCHOTE”.

Kufunga siyo kuacha kusoma gazeti ulilozoea, kuacha kuchana nywele n.k., ni kuacha kabisa kula au kunywa kinywaji chochote.  Maana hii ya kufunga, inathibitishwa na maandiko yafuatayo:- EZRA 10:6; YONA 3:7; 2 SAMWELI 3:35; ESTA 4:16; KUMBUKUMBU LA TORATI 9:9; MATENDO 9:9.

Kufunga siyo kuacha kula vyakula kama ugali au wali halafu ukawa unakunywa soda, maziwa, uji au kula matunda n.k. Ni kuacha kula chochote wala kunywa chochote kile.  Andiko linalotumika kuhalalisha kula vitu vidogo vidogo ni DANIELI 10:2-3.  Katika andiko hili “SIKULA CHAKULA KITAMU”, chakula kitamu ni “DESSERTS” kwa Kiingereza au “PUDDING” – ndizi, nanasi, papai, machungwa n.k.
✔  Katika mistari hiyo Danieli anasema hakula lolote kabisa.

Kwa hio kama tunafunga lazima kuacha kula kwa muda fulani kulingana na ratiba yako kuwa unafunga kwa muda gani, masaa 12, 24 n.k.

™Neno from Bishop Zachary kakobe.

AMKENI USINGIZINI.



(Chungu lakini inaponya!!).

Ujumbe  unatoka:  ISAYA 56:10-11,

"Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana MAARIFA; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala usingizi. Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na ni WACHUNGAJI wasioweza kufahamu NENO; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote".


Giza nene la Kiroho linazidi kuisonga dunia yetu kwa sababu ya viongozi wa dini, na watu wengi sana wataangamia siku ya mwisho kwa sababu ya kupotoshwa na viongozi. Neno linasema HOSEA 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani wangu mimi; kwa kuwa umeisahau Sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahu watoto wako”

Kizazi chetu kiko kwenye hatari kubwa, kwani Shetani ametunga falsafa nyingi za uongo, juu ya kweli ya NENO la MUNGU.

Wapendwa! Amkeni pambazuko liko karibu, mnapoona Dini na Madhehebu mengi yakianzishwa huku kila mmoja akiwa na mafundisho tofauti na mengine yaliyo kinyume neno la Mungu, jueni unabii unatimia, ukibahatika kuufahamu ukweli, CHANGAMKA! amua kuufuata ukweli. 

Mungu anasema ISAYA 9:16“Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia” .

Hapa hakuna usalama, Wachungaji wasiojua kweli ya Mungu na Waumini wao wanaokubali chochote bila kuchunguza ukweli, wote wataangamia.


Ujumbe huu ni sauti ya Matengenezo kwa kila anayejiita Mtumishi, bila kujali cheo chake Wala wadhifa wake. 

Neno linasema; wachungaji wamekuwa ni sawa na Mbwa Bubu asiyebweka adui anapovamia zizi la kondoo, hebu jiulize – Inakuwaje Uovu unadumu kati ya waumini? Kama Mtumishi anazini na waumini, au ni mlevi, muuza madawa ya kulevya n.k. waumini watakuwaje?Tunaona, Kwa sababu ya Maslahi! wenye pesa makanisani na miskitini hawakemewi hata kama wanafanya Dhambi za wazi, Viongozi wamepofushwa macho kwa sababu ya Maslahi.

Oooh! Wapendwa; wakemeaji wa dhambi siku hizi wako wapi?? Manabii na waonyaji, kama akina Isaya, yeremia, Hosea, Ezekiel n.k. wako wapi siku hizi? Mbona wote wamegeukia Injili ya UTAJIRI na Kujikusanyia watu wenye Pesa kwa ajili ya maslahi yao binafsi?


Wakati wote wanafundisha Ujumbe laini, mafundisho yadanganyayo, wanikazia - uponyaji, utajiri, Baraka, Kupanda mbegu, Zaka na sadaka, amani n.k. huku waumini wakidumu kwenye Dhambi na hatimaye kuingia kwenye maisha magumu zaidi ya walivyokuwa mwanzo. 

aKatika historia ya Biblia hakuna Nabii wala Mtume aliyekuwa na Injili ya akijilimbikizia Mali za Dunia hii kwa mgongo wa injili na sadaka za waumini, mbali na Kuonya na Kukemea dhambi.

Hebu jiulize Wewe mchungaji: Je Ni kweli wewe umetumwa na unaongozwa na Mungu KWELI?

Huo ulevi, Hiyo tamaa ya Ngono, huko kupenda Fedha na utajiri, Hiyo mipango unayoungana na Dini ya mashetani kupinga kweli ya Mungu, huo upendeleo kwa wenye Pesa na kudharau maskini, na hiyo nyumba ndogo ULIONAYO, na huyo bwana asiye mume wako, na hayo madawa ya kulevya na biashara haramu.

huo utapeli na udanganyifu, na huko kugombania madaraka na kufanya kampeni kama vyama vya siasa, hiyo michezo michafu ya kuchezea mabinti za watu,na hizo hirizi unazotumia kuvuta watu na kutenda miujiza ukihadaa roho za watu kwa jina la Upako, hizo hasira,chuki, visasi na Mambo yanayofanana na hayo; Unaamini yanatokana na Roho Mtakatifu??.

MSIDANGANYIKE; Mungu anasema “Tokeni kwake (Shetani na Mpinga Kristo), enyi watu wangu, msishiriki Dhambi zake, wala msipokee mapigo yake” Ufunuo 18:4. TOKENI HARAKA YESU ANARUDI, KWA WATEULE!!!!

Mbwa mwitu wamevamia kundi, nani wa kusimama kupiga kelele, wakati utitili wa mafundisho potofu yaliyo kinyume na ukweli wa neno la Mungu yanaiingia kanisani!  nani wa kutoa maonyo na kutengeneza? Neno linasema 2TIMOTHEO 4:2-4 “Lihubiri NENO, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, KARIPIA, KEMEA, na KUONYA kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundsho yenye uzima … na kuzigeukia hadithi za Uongo” 

 "Neema imefunuliwa ili kutuweka HURU mbali na Dhambi", sio kuhalalisha dhambi, kama wengi wanavyodai, huku wakizidi kuzama katika matope ya Dhambi. Washirika kueni makini mnaweza kujikuta mnatumbukizwa shimoni na kupotea milele katika jehanam ya moto na kisha ziwa la Moto kwa kuzifanya shingo zenu kuwa Ngumu. AMKENI ITAFUTENI KWELI YOTE, NYAKATI HIZI NI ZA HATARI SANA,kilaa mmoja ajiangalie mwenyewe na kuutimiza wokovu wake kwa kuogopa na kutetemeka.WAFILIPI 2:12.


GOATU

JE, UNAJUA G.O.A.T.U. NI NINI?

✔Wanachama wa Kikundi cha siri cha freemason wanamwabudu mungu
anayeitwa GAOTU – Great Architect Of The Universe – yaani ‘Mbunifu mkuu wa
ulimwengu.’ Freemason hawamwabudu Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Sala zao zote huelekezwa kwa GAOTU.

✔Architect ni mtu anayebuni ramani za majengo,
majengo unayoyaona katika nchi mbalimbali yakiwemo yale yaliyomo ndani ya miji ya
nchi yetu, yanatokana na ubunifu wa watu wanaoitwa Architects. Ni watu wenye elimu
kubwa sana kuhusu mambo ya ubunifu na ujenzi wa majengo.

✔Freemason nao ni
wajenzi wa maadili wanayoyataka wao na pia wanaye Architect (mbunifu) wao mkuu
ambaye ndiye wanayemwabudu, jina la Architect wao ni GAOTU. Huyo ndiye mbunifu
mkuu wa shughuli za Freemason katika ujenzi wa ulimwengu, wengine ni
watekelezaji tu.

✔Wapo watu pia wanaoelekeza sala zao kwa viumbe badala ya kuelekeza kwa Muumbaji. Wao pia hawatofautiani na Freemason maana wote
wanakwenda kinyume na Mungu, na ukweli ni kwamba wanafanya hivyo kutokana na ubunifu wa GAOTU
maana kazi yake ni kubuni mbinu mbalimbali za kuwafanya watu wawe mbali na Mungu.

✔ Yesu anasema kwamba tunapotaka kusali tusali hivi, “Baba yetu uliye
mbinguni……” Mathayo 6:9-13, ikimaanisha kwamba sala zetu zote tuzielekeze kwa
Mungu aliye mbinguni tena kwa Jina la Yesu.
➡ GAOTU anajua kwamba Mungu alisema,
“mtu akijikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote” Yakobo 2:10, ndio maana
anajitahidi kuwafanya watu wamkosee Mungu hata katika kitu kidogo, na watakuwa wamemkosea juu ya yote. Hivyo unaweza ukawa mlokole, msabato, mkatoliki,
muislamu, mbudha, myahudi nk. lakini ukimkosea Mungu katika jambo moja tu
umemkosea juu ya yote.

✔Ndio maana leo hii katika dunia nzima kuna utitiri wa
madhehebu na dini za kila aina. Wataalamu wanasema kuna dini zaidi ya elfu tatu! Je,
wote watakwenda Paradiso? Biblia inasema, “Je! Hamjui ya kuwa wale washindanao
kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja?” 1 Wakorintho
9:24. Hivyo pamoja na kuwa na dini nyingi kiasi hicho na dini zote zikiwa zinadai
kupiga mbio ili kupata tuzo ya uzima wa milele, ni wale tu wanaotii kila moja ya amri za Mungu ndio wanaopiga mbio vizuri na ndio watakaopata tuzo, nao watatoka katika dhehebu moja tu.

✔Kwa nini watu huingia Freemason? Ni kwa sababu ya kutaka utajiri wa dunia hii.
➡Wakati shetani anamjaribu Yesu, alimwonyesha utajiri, “Kisha ibilisi akamchukua
mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.” MATHAYO 4:8, 9.
✔Baada ya ibilisi kushindwa kumnasa Yesu, sasa aliendelea kutumia njia hiyo hiyo kwa kumtumia mnyama ili awape watu utajiri kupitia Freemason, ➡tunasoma kwamba, “Lakini katika
mahali pake atamheshimu mungu wa ngome; na mungu ambaye baba zake hawakumjua
atamheshimu, kwa dhahabu na fedha, na vito vya thamani na vitu vipendezavyo…..na
yeye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataigawa nchi kwa rushwa.” Danieli 11:38,39. Ndio maana watu wengi wanaingia kwenye vyama vya siri kama Freemason na kila anayeingia humo hufanywa apate Kumiliki vitu vingi na kuwa tajiri mkubwa.
➡➡Ni sehemu ndogo ya neno la uzima kutoka kwa mtumishi wa MUNGU, ASKOFU ZACHARY KAKOBE. Ukitaka kulisoma somo hili kwa mapana na marefu na kufahamu siri nzito kuhusu FREEMASONS NA ILLUMINATI ingia kupitia link hii⤵⤵
➡www.davidcarol719.wordpress.com/freemasons-na-illuminanti/
UBARIKIWE NA BWANA.

WOKOVU NI AMANI

WOKOVU NI AMANI MAISHANI MWANGU, SIJUI KWAKO???

✔Wokovu au ukombozi umenitoa katika utumwa mzito wa dhambi na uovu mwingi.
Wokovu ni zawadi ya moyo mpya wa nyama na roho mpya.

✔Wokovu unapatikana kwa njia ya mwana wa Mungu YESU KRISTO pekee, MATENDO 4:10-12.
Wokovu unauhusiano mkubwa na ufalme wa mbinguni ambao hata sasa tunao kwa njia ya Yesu kristo alietupenda.

✔Wokovu upo kwa wale wanaomtii na kumfata YESU,na hii ndio siri ya injili.

Wokovu katika biblia unaelezwa kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo.
1. Ni siri ya MUNGU iliofunuliwa kwetu.
▪Waefeso 3:9, 6:19

2. Ni mpango wa MUNGU uliowekwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.
▪Waefeso 1:3-14

3. Ni nuru iliofunuliwa kwa mataifa
▪Luka 2:30-32

4. Ni kupita kutoka mautini na kuingia uzimani
▪Yohana 5:24

5.Ni ujumbe maalum kwa wenye dhambi wote utakaowageuza nia zao.
▪Marco 2:17

6.Ni zawadi ya neema tunayoipokea kwa imani wala si kwa matendo
▪Waefeso 2:8-9

7.Ni haki ya MUNGU iliofunuliwa au iliodhihirishwa kwa wanadamu wote
▪Warumi 1:16-17,Warumi 4:22-25.

8.Ni upatanisho wa MUNGU na wanadamu
▪2Wakorintho 5:18-19

9.Ni kuzaliwa mara ya pili katika roho.
▪Yohana 3:1-11.

10. Ni kuwa mfu katika dhambi na kuwa huru mbali na dhambi zote
▪Warumi 6 yote.

11. Ni kuwa na Amani na MUNGU
▪Warumi 5:1

✔Wokovu ni badiliko halisi la kimwili na kiroho ambalo lina ushuhuda wa wazi kabisa kwa mtu.
Msingi wa wokovu ni kutubu dhambi zote kwa kumaanisha kuziacha kwa imani na kuambana na ubatizo wa maji tele
▪Matendo 2:38, 20:21.

✔Lakini Wokovu si kutubu dhambi tu lakini ni kutubu dhambi na kuzaa matunda yapasayo toba na kuweka imani yako kwa YESU
▪Marco 16:15, Yohana 6:47.

✔Kwa YESU tulichaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu(waefeso 1:4), kwa imani tumeokolewa(warumi 8:24) Na kwa njia ya msalaba ni Nguvu kubwa ya MUNGU kwa wale wanaondelea kuokolewa( 1wakorintho 1:18).

✳RAFIKI, UTAPATAJE KUPONA NA HATARI YA KWENDA MOTONI USIPOUJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII?

✳TUBU LEO NA KUAMUA KUMFATA YESU ANAEBADILISHA, ACHANA NA MAFUNDISHO MANYONGE ,ACHANA NA DHAMBI NA UOVU, LITAFUTE NENO LA KWELI LA KRISTO LINALOHUISHA MWILI NA ROHO.

✔ISAYA 55:6-7
"Mtafuteni BWANA maadamu       anapatikana,
mwiteni,maadamu yu karibu.
Mtu mbaya na aache njia yake,
na mtu asiehaki aache
mawazo yake;
Na amrudie BWANA,
Naye atamrehemu;
Na arejee kwa MUNGU wetu, Nae atamsamehe kabisa..

LENGO LAKO NI NINI?

LENGO LAKO NI NINI?

✔Ni kweli kabisa wanadamu tunawaza na tunamalengo mengi ambayo yanatofautiana kati ya mtu na mtu mfano Katika LUKA 12:16-21, tunaona mtu mmoja aliekuwa na lengo la kujiwekea akiba mavuno yake katika ghala kubwa asijue muda wake wa kuishi duniani umekwishaa.

✔pamoja na malengo yote tulionayo, ila lengo kuu ni kuupata uzima wa milele,hili ndio liwe la kwanza katika maisha yetu na hayo malengo mengine tutazidishiwa tu. MATHAYO 6:33.
✴Ukikosa uzima wa milele utakuwa umepata hasara ya milele.

✔Hakikisha jina lako limeandikwa kwenye kitabu cha uzima, hutaweza kuandikwa huko kama lengo lako kuu ni kuyapata yaliochini tu, wakati yote unayafikiri yaliochini (duniani).

✔Mtu mwenye lengo kuu la kuupata uzima wa milele anaweza kustahimili majaribu na mikikimikiki ya adui na hawezi kurudi nyuma hata akiyakosa haya madogomadogo.

✔Yesu Akasema itakufaidia nini ukiupata ulimwengu huu wote na ukapata hasara ya nafsi yako? Hakuna faida zaidi ya kuishia jehanam ya moto.

✔Kaka zangu,dada zangu bado kitambo kidogo tu YESU atakuja,wala hawatakawia LAKINI wanaositasita MUNGU hapendezwi nao
🔹wengine wanawaza ngoja niache wokovu kwa muda nitaokoka tena baadae.
✴rafiki Yesu akasema hatujui ni siku ipi wala saa ipi atakayokuja mwana wa adamu
🔹 Ni Muda mfupi sana umesalia, Yesu atakuja kulichukua kanisa,ni wale tu waliojiweka tayari kumsubiri Bwana wao.

✔watakatifu waliotutangulia waliutazamia mji ule wa mbinguni kwa imani, hata walipopita katika magumu hawakutetereka wala kubabaika, WAEBRANIA 11:8-10..

✔Hukumu haina huruma kwake Yeye asie na huruma, Yesu ametuokoa kwa upendo wake kwetu ili tusiangamie na anatutaka na sisi tuwahurumia wengine na kuwaleta kwake.
🔹kama hatushuhudii wengine habari njema,hatuwahubiri wengine waokoke, hatuwaaliki walisikie neno la Kristo,watuwaombei wengine,watuwafundishi wengine kama hivi mitandaoni nasi pia mbinguni hatutaingia.
✴BWANA AMPE NEEMA KILA MMOJA KUUKOMBOA WAKATI✴

BARUA INAYOSOMWA NA WATU WOTE

YEYOTE ULIEOKOKA ZINGATIA WEWE NI BARUA INAYOSOMWA NA WATU WOTE.
✔Kila mtu alieokoka Maandiko yanasema imempasa kuwa nuru kwa ulimwengu ili watu ambao hawajaokoka wakimwona wamtukuze Mungu lakini pia waokoke.

✴2wakorintho 3:2-3 "Ninyi ndinyi barua yetu,ilioandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote......"

✔Lakini katika majira haya ya Laodikia kumekuwa na wimbi kubwa la wokovu vuguvugu kwa watu ambao wameokoka, wokovu umekuwa kitu cha kawaida kwao kiasi cha kushindwa kutofautisha waliookoka na wasiookoka.

✔Wokovu na viwango vya Mungu vya utakatifu havibadilishwi na mazingira yaliotuzunguka, kaka dada jihoji mwenyewe kama bado una wokovu uliupokea mwanzo au la!

✴Mpendwa katika jamii unayoishi unasomekaje? Watu wanauona wokovu ulionao au unalitukanisha jina Bwana!?
✴Binti ulieokoka mavazi unayovaa yanautangaza wokovu au unasomeka kama kahaba kwa mavazi yako yanayoacha sehemu zako kama matiti,mgongo,tumbo,mapaja wazi?
✴kijana unasomekaje unapokuwa chuoni au shuleni?
✴wazazi, mnasomekaje kwa watoto wenu?
✴waimbaji mnachokiimba mnakitenda? au mnaimba kwa desturi na mazoea tu?
✴wahubiri,wainjilisti,walimu,wachungaji tunasomekaje? Je,ni kweli Tunachokifundisha tunakiishi?

✔Kama mataifa watatusema watuseme kwa maisha Yetu kuwa na ushuhuda mzuri lakini ni fedheha mkristo ulieokoka mataifa wanakusema kwa⤵
🔹uzinzi na uasherati wako,
🔹umbea wako,
🔹uchonganishi wako n.k.

✔1PETRO 2:12 maandiko yanasema," Mwe na mwenendo mzuri kati ya mataifa,ili iwapo huwasingizia kuwa ni watenda mabaya,wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa".

✔Wewe ambae umeokoka lakini unadumu katika dhambi unamfanya Yesu aliekufa msalabani ni mpuuzi na watu wanautukana wokovu kwa sababu yako.

~Neno linasema katika 2TIMOTHEO 2:19," Lakini msingi wa Mungu uliobora umesimama,wenye muhuri hii,Bwana awajua walio wake.Na tena kila alitajae jina la Bwana na auache uovu."

✔Kama unajijua ni vuguvugu unachanganya masomo, duniani umo na kwa Mungu umo uwe na bidii UKATUBU kwa maana Vuguvugu wote watatapikwa watoke katika kinywa cha Bwana Yesu, NDIKO KUTAKUWAKO KILIO NA KUSAGA MENO!!

UDUNIA

UDUNIA
(1 yohana 2:15-17)
Neno dunia linalotumika hapa halimaanishi sayari ile ambayo wanadamu tunaishi lakini ni zaidi ya maana hiyo, kuna maneno matano ya kiyunani yanayotafsiri dunia/ulimwengu
1/Ge
2/aion
3/aionios
4/oikoumene(hii ndiyo sayari tunayoishi)
5/Kosmos(leo tutaliangalia hili zaidi)
Katika mistari hapo juu katika lugha ya kiyunani unakuta neno Kosmos(yaani msiipende Kosmos wala mambo yaliyo katika Kosmos)
(2Timotheo 4:10) Dema aliniacha akiipenda KOSMOS.
Kuipenda Kosmos ni kuishi maisha ya udunia
(Yohana 14:30) Mkuu wa Kosmos ni shetani mwenyewe (2Wakorintho 4:3-4) m ndogo inamzungumzia shetani, yana anaitwa mungu wa dunia hii.jina lake kiyunani ni KOSMOKRATOR.Nyuma ya udunia(kosmos) kuna huyu kosmokrator.
KOSMOS(dunia) ina maana nyingi ambazo zimefichika
Katika mambo ya udunia yapo ambayo ni dhambi moja kwa moja na mengine yaweza kuwa mazuri lakini yakawa kosmos.
Moja ya mambo ya dunia

1/Mapambo ya Uzuri
Kutokana neno Kosmos tunapata neno la kiingereza "cosmetics" (1 Petro 3:3-6)(Isaya 3:16-24)(kutoka 33:1-6)
Mapambo yoyote kwa mwanamke ambayo yanalenga kuwavuta wanaume kwa uzinzi na uasherati, ili aonekane ni mzuri, anavutia, hivi vyombo vyote vya uzuri nyuma yake yupo kosmokrator, mtu atajichubua ngozi, na kosmokrator anaweza akawatumia wachache kuanzisha mitindo(fashion) na wengine wataiga mfano watu wanavaa milegezo kwa sababu waliwaona watu wanafanya hivyo(Warumi 12:2) "Do not be conformed with fashion of this world. Hatutakiwi kufuatisha namna(mitindo) ya dunia hii mana nyuma yake kuna Kosmokrator(Yakobo 4:4) tukiwa na urafiki na udunia tumekuwa adui wa Mungu(1 yohana 5:4)(1 yohana 2:15-17). Ndani ya dunia kuna kiburi cha uzima, kuna vitu unaweza ukafanya kwa sababu wewe ni mzima, kuna mahari mtu huugua sana hata haoni maana ya vitu hivyo.
Kuipenda dunia kuanaambatana na tamaa
Moja ya sehemu ambayo kuna kosmos ni mitandao(kutumia muda mwingi mitandaoni kuliko maombi au kazi ya Mungu) (Wakolosai 3:1-2)(yohana 17:14-16)
Roho ya kosmokrator ndo ipo nyuma ya michezo yote hii ya dunia, mipira, riadha n.k. watu hushughulishwa na michezo hiyo hata hukosa muda wa kumuhudumia Bwana.
Michezo ya kompyuta(games), karata, draft, bao
(Mathayo 13:22)Biashara, kazi, magari, pikipiki zinazokufanya ushughurishwe hata kukosa ibada kuliko kumpenda Mungu zote hizo ni kosmos(Mwanzo 19:31)(Waefeso 2:2)
(Wafilipi 3:19). Wakati mwingine tumbo nalo linaweza kutufanya tuwaze tu chakula kuliko kumuhudumia Bwana
TUNAUSHINDAJE UDUNIA.
Ni kwa kuwezeshwa na Yesu
Kwanza tunatubu kwa kumaanisha kuacha udunia
Baada ya kuzaliwa mara ya pili tunamwambia Yesu atufanye kuwa kama yeye.ili tuweze kuishinda dunia.

#BishopKakobe

Imeandikwa na Fredie Haule.

USILIFANYE KANISA KUWA PANGO LA WANYANG'ANYI

Somo no 3:NENO KWA MCHUNGAJI-USILIFANYE KANISA KUWA PANGO LA WANYANG'ANYI.

Kama wachungaji lazima tufahamu kanisa tunalolichunga sio letu, kanisa ni la Yesu Kristo mwenyewe(Mathayo 16:18)(Waebrania 13:20)
Yesu Kristo anaitwa mchungaji mkuu, na wachungaji wako chini ya mchungaji mkuu(Yohana 21:15-17), hivyo tunavyolisha wanakuwa sio kondoo wetu bali kondoo ni wa Yesu Kristo aliye Mchungaji Mkuu na kanisa ni lake.(hivyo hakuna mtu kusema kanisa langu, kondoo wangu, huduma yangu).(1wakorintho 3:10-11). Wachungaji wanatakiwa kujenga kanisa juu ya msingi uliokwishawekwa yaani (Yesu Kristo) na sio misingi yetu tunayoijua wenyewe.
(1Timotheo 4:1).Nyakati za mwisho sio tu washirika lakini wapo hata wachungaji watakaojitenga na imani, kuna roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani ambayo yamezifanya nyakati hizi kwa wachungaji wanaochunga kanisa kuwa hatarini, na moja ya roho hizo ni roho ya mashindano.
Wachungaji watashindana na kusema kanisa langu ni kubwa kuliko makanisa yote Tanzania, Afrika mashariki n.k. Wanashindania idadi ya watu(umati).
Nyakati hizi ni rahisi kwa mchungaji kupata umati wa watu na ni kutokana na msingi alioweka katika kujenga kanisa.
(2 Timotheo 4:1-5)Nyakati hizi za mwisho kutakuwa na kundi kubwa la watu ambao wanatafuta kusikia yale wanayotaka wao na sio yale Mungu anataka, hawataki kusikia kweli(mafundisho ya uzima) wanataka hadithi za uongo, na kama wakipata mchungaji aliye tayari kuwadanganya watamfurahia na kumpenda na hivyo watamgeukia(watavutika)
(Isaya 30:8-10), nyakati hizi za mwisho wachungaji tukiingia kwenye mtego na kuhubiri maneno laini au hadithi za uongo ili kuwavuta watu, tunaweza tukawa na watu wengi, tukawa maarufu sana,tukatajwa kila kona lakini hatimaye siku ile ya mwisho tukajikuta tumeachwa.
(MATHAYO 21:12-13)Kuhibiri hadithi za uongo ili kuwavuta watu ni kulifanya kanisa kuwa pango la wanyang'anyi.
(LUKA 10:29-37)Nyakati za biblia kulikuwa na mapango ya wany'anganyi(ambayo leo yanaweza kuitwa magheto, masikani,vilingeni n.k) na yalikuwa ni mashimo yaliyochongwa kwenye mawe milimani kwa juu ili kuwavizia watu na kuwapora, wakiwa kwenye mapango inakuwa rahisi kuwaona watu wakiwa wanashuka kutoka milimani na kuona ana nini na kujipanga kumpora, ndio mfano wa yule mtu aliyekuwa akishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko akawa anaonekana na wanyang'anyi hawa wakiwa kwenye mapango yao akaporwa kila kitu na akapigwa sana karibu ya kufa akaja kusaidiwa na msamalia mwema. Watu hawa walio katika pango wanakuwa ni watu waovu, wauaji, wahuni,wakabaji, wabakaji, walawitiwavuta bangi, na uchafu wa kila namna unaukuta ndani ya pango la wanyang'anyi.
Yesu anaposema nyumba yangu sio pango la wanyang'anyi anamaanisha sio mahara pa watu waovu bali ni karakana ya kubadirisha watu maisha yao, na kimsingi kanisa ni la watu waliookolewa (Matendo 2:47).
Kanisa la Kristo vilevile ni kanisa la wazaliwa wa kwanza ambao majina yao yameandikwa mbinguni (Waebrania 12:22-23)

(Zaburi 50:16-22) Kwanza mchungaji kabla hajasimama kuhubiri lazima yeye mwenyewe awe amezaliwa mara ya pili(awe ameokoka), awe mbali na dhambi, kuhubiri injili kunafananishwa na kufanya biashara,Yesu anasema tufanye biashara hata ajapo(Luka 19:13) tunaitangaza biashara, na biashara yenyewe tunatangaza kwamba kuna kifaa cha kusafisha mioyo, tunawezaje kutangaza biashara hiyo wakati sisi mioyo yetu ni michafu, tunawezaje pia kutangaza juu ya sabuni(Yesu) kwamba inasafisha wakati mavazi yetu ni machafu?
Kwa hiyo wachungaji kwanza tutubu dhambi zetu ili nasi tuwe safi na tuzaliwe mara ya pili na hapo ndipo tunapopata uwezo wa kushinda dhambi (warumi 1:16) maana Sauli alibadirishwa akawa Paulo Mtume
Lazima tufahamu pasipo utakatifu hapana mtu atakayemuona Mungu(1Timotheo
1:12-15)(Tito 3:3-6).
(Waebrania 12:14)(1 petro 1:15-16) (Mathayo 5:48). Mungu amewaweka wachungaji katika kanisa ili kuwakamilisha watakatifu wafikie cheo na kimo cha utimilifu wa Kristo na huu ndo msingi uliowekwa ambao wachungaji wanatakiwa kujenga kanisa juu yake (Waefeso 4:11-15) (Yohana 15:3). Neno ambalo linatakiwa kufundishwa ni neno la usafi ili kuwafanya hao wanaolishwa hilo neno kuwa safi na wanapelekwa hatua kwa hatua ili wafike cheo na kimo cha utimilifu wa Kristo, na kama wachungaji hawazingatii hili wanajenga kanisa lao na sio la Kristo, hata kama mchungaji akiwa na jina kubwa sana siku ile ya mwisho atakataliwa (1wakorintho 2:10)
(1  Wathesalonike 1:7)(Ufunuo 21:7)(2Timotheo 2:19)
Msingi wa mahubiri ya wachungaji yanatakiwa kuwa ni mtu kuacha uovu na si vinginevyo.(Ufunuo 3:16)
(1Petro 5:1-4) Wako wachungaji wanaitwa matajiri wakubwa lakini wamejipatia fedha ya aibu, wanaombea watu kwa pesa, wanahubiri hadithi za uongo ili watu wajae watoe sadaka
(Daniel 12:3) (Ufunuo 3:17).
(Matendo 8:18-24)Wachungaji wengi wanaonekana ni matajiri, na wengine wanadhani kufanikiwa ni kuwa na magari, majumba, matreni, mandege n.k,wanaweza wakawa na vyote hivi lakini vikawa vimetokana na fedha ya aibu,.
Paulo aliogopa kwamba asije akawahubiri wengine na yeye mwenyewe akawa mtu wa kukataliwa( 1wakorintho 9:27).
Wachungaji nao watasimama nao mbele za Mchungaji Mkuu kutoa hesabu za kazi walizozijenga(Waebrania 13:17)
Wako wahubiri wanafanya deal na watu kwamba waonekane wanaombea watu na wanapokea miujiza, lakini ni miujiza ya kutengeneza, iko mifano mingi ya wahubiri wanaolipa watu pesa ili waseme wamepokea miujiza lengo hasa ni kuwadanganya watu waonekane wana upako ili wavute watu wengi zaidi(Waebrania 1:9),upako wa mchungaji haupimwi kwa miujiza anayofanya bali unapimwa kwa jinsi ambavyo anachukia dhambi(maasi) na kuyakemea na kufundiaha haki.
Kanisa la Kristo halikujengwa kwenye miujiza, Historia ya biblia inasema muda Yesu alioutumia kufanya miujiza ni sawa na siku 21(usiku na mchana)(yohana 6:26-27) muda mwingi aliutumia kufundisha neno la usafi na utakatifu(Waebrania 13:20-21)(Yohana 6:60-61, 66-68) Maneno ya uzima yanaweza yakawa magumu yakamfanya mtu akimbie lakini tusishushe viwango, na ikiwa wachungaji watahubiri kweli walio wa Kristo watakaa(Yohana 16:13)(1yohana 2:19)(Luka 6:26)(Mathayo 18:6-7)
(Yakobo 3:1)..kule motoni kuna adhabu kwa madaraja, ataanza shetani atakuja nabii wa uongo na mpinga kristo, watafuata malaika walioasi kisha watafuata walimu wa uongo wanaodanganya watu mana kuna adhabu kubwa kwa walio walimu, (1wakorintho 2:13-15)
(Yohana 5:41, 44) Mchungaji anatakiwa atafute utukufu kwa Mungu na sio wa wanadamu.

#BishopKakobe

Imeandikwa na Fredie Haule

WOKOVU WA KUIGIZA

WOKOVU WA KUIGIZA.
✔kwa wale wote ambao wokovu wao ni wa jumapili tu, ikifika siku ya ibada unajifanya ni mtakatifu, unajifanya kuvaa mavazi yenye heshima ila ukitoka tu tayari unakuwa mbwa mwitu!!

Hayo yote unayofanya ndio, unaweza kumdanganya mchungaji wako, unaweza kuwadanganya washirika LAKINI YUKO MUNGU AMBAE NI MWISHO WA YOTE, HUWEZI KUMFICHA WALA KUMDANGANYA. Mungu kwake giza na nuru ni sawasawa.Hata ungejificha wapi macho ya Mungu kama mwale wa moto bado yatakuona tu!

✔Matendo yako yote record zake ziko mbinguni na siku inakuja Mungu atakapozifuchua siri zote za wanadamu sawasawa na matendo yao.
🔹ZABURI 139:7-12.
"7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.

✔Mungu hadhihakiwi, ujanja ujanja unaoufanya utaufanya hadi lini? Utaendelea kuigiza hadi lini rafiki? Badilisha muelekeo wako. Acha wokovu wa kuigiza kuna OLE kwa wote wanaofanya UNAFIKI!
kama unakaa kwenye wokovu kaa kwa kumaanisha...

ASOMAE NA AFAHAMU

ASOMAE NA AFAHAMU;

Niliweka ujumbe katika post yangu iliopita kuhusu maandalizi ya ujenzi wa hekalu israel, lakini wamekuwepo watu ambao hawaelewi uhusiano uliopo kati ya ujenzi wa hilo hekalu na kunyakuliwa kwa kanisa.

Kwa faida ya wengine pia nitajaribu kueleza kidogo ili waelewe uhusiano uliopo katika mambo hayo mawili.

Hekalu linalokwenda kujengwa ni hekalu la tatu na la mwisho katika israel, ambapo ndipo litakapokuja kusimama chukizo la uharibifu DANIEL 9:27. Chukizo hili ni mpinga kristo ambae pia ni Asi, mpingamizi au mnyama!.

Ikumbukwe tu katika wakati wa dhiki kubwa wa miaka saba ndipo mpinga kristo huyu atakuwa wazi sana, na kipindi hicho cha dhiki kubwa kinagawanywa katika sehemu mbili, miaka mitatu na nusu ya mwanzo au miezi 42 au siku 1260 na kipindi cha pili cha miaka mitatu na nusu mingine.

Katika kipindi cha kwanza mpinga kristo atafanya agano thabiti na israel na kuisapoti israel sana hata katika ujenzi huo na isrel itadanganyika sana LAKINI baadae sasa mwishoni mwa  miaka mitatu n nusu ya mwanzo atalivunja agano na atawageuka waisrael na ndipo chukizo hilo litasimama sasa!

Ikumbukwe kuwa wakati wa dhiki kubwa ni israel peke yao ambao wana neema ya kuokolewa maana wakati wa mataifa(majira ya neema yatakuwa yamefika mwisho), ikiwa israel watafata maelekezo ya Bwana Yesu katika MATHAYO 24:15-22.

Sasa haya yote hayawezi kutokea kabla ya kanisa kunyakuliwa, yaani mpinga kristo hawezi kufunuliwa wazi kwa sababu kanisa bado lipo duniani na ndio linalozuia 2WATHESALONIKE 2:3-7, nanukuu mstari wa 6 na 7 "na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake, Maana ile siri ya kuasi inatenda kazi hivi sasa,LAKINI yuko azuiaye hata atakapoondolewa.

Kuja kwa Bwana Yesu kulinyakua kanisa(watakatifu) itakuwa inamaana ya kupisha kipindi cha dhiki kubwa duniani na kufunuliwa kwa mpinga kristo sasa. Mungu wakati kabla ghadhabu yake haijashuka huwa na anawatenga wenye haki kama ilivokuwa kwa nuhu, luthu na hata Lahabu..

Kanisa halitapitia kwenye dhiki kubwa ya miaka saba kama wengine wanavyodai, ndio maana Bwana Yesu atawanyakuwa juu mbinguni kupisha dhiki kubwa duniani.

Sasa basi kama ukisikia habari za israel kufanya agano au kuweka mkataba na umoja wa nchi za ulaya ukiwa duniani ujue tayari umeachwa!!!
BWANA AMSAIDIE KILA MMOJA WETU ASIWE MTU WA KUACHWA BAADA KUSOMA HAPA,AMEN!!!

HIO HAPO CHINI NI PICHA YA RAMANI ILIONDALIWA AMBAYO NI YA HEKALU LA TATU LINALOTARAJIWA KUJENGWA ISRAEL AMBALO WANASEMA LITACHUKUA MUDA WA MIAKA MITATU KUKAMILIKA!!!

TOFAUTI YA UNYAKUO NA KUJA KWA YESU MARA YA PILI.

TOFAUTI YA KUJA KWA YESU WAKATI WA KUNYAKULIWA KANISA NA  KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.

Wako watu wengi sana wanachanganya matukio haya mawili kiasi cha wengine kudhani kuwa kanisa litakuwepo wakati wa dhiki kubwa.

Matukio haya ni tofauti sana;

KUJA KWA YESU WAKATI WA KUNYAKULIWA KANISA
🔹Hapa Bwana Yesu atakuwa anakuja kama Bwana Arusi kumchukua bibi harusi ambalo ni kanisa takatifu lisilo na doa,waa wala kunyanzi (EFESO 5:27, YOH 14:1-3).
🔹Yesu atakuwa anakuja kukutana na watakatifu wake mawinguni. Yesu hatakanyaga juu ya uso duniani huu wa kunyakuliwa kanisa, walioko duniani hawatamwona wakati huu (1WATHEEALONIKE 4:17).
🔹Kunyakuliwa kwa kanisa ni kabla ya dhiki kubwa kuanza duniani(UFUNUO 3:10, LUKA 21:22-23,34-36, 1Wathesalonike 1:10).

KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
Mara ya kwanza Yesu kuja duniani ni pale alizozaliwa kama mwanadamu na akaishi kimaskini hadi alipomaliza kazi yake duniani na kurudi mbinguni. Mara ya pili atarudi kama Bwana wa Mabwana na mfalme wa wafalme.
🔹Hapa Bwana Arusi Yesu kristo atakuwa anakuja pamoja na bibi Arusi(watakatifu) aliowanyakua miaka saba iliopita kwa lengo la kutawala( YUDA 1:14,UFUNUO 1:7.)
🔹Wakati wa kuja Yesu mara ya pili duniani, atakuja na kukanyaga katika mlima wa mizeituni mahali pale alipoondokea alikuja mara ya kwanza duniani. Kila jicho la watakaokuwako duniani watamwona(ZEK 14:4-5, MAT 24:27).
🔹Kuja kwa Yesu mara pili duniani ni mara baada ya dhiki kubwa kuisha au kumalizika duniani (MATHAYO 24:29-30, 2WATHESALONIKE 2:1-4).

Bwana awabariki wote!!

WAIGIZAJI MADHABAHUNI

WAIGIZAJI MADHABAHUNI.
Mathayo 24:24-25

Mengi sana yamefanyika kuudharilisha mwili wa kristo, manabii na mitume wengi wauongo wametokea ambao wanamajengo makubwa ya makanisa na umati mkubwa wa watu na
Wako kila mahali duniani. NI WAIGIZAJI SIO WACHUNGAJI.

Dalili zao;
✔Wao wenyewe staili zao za kunyoa ni mapunk.
✔Katika vidole vyao wamejaza mapete.
✔wanaruhusu watu kujipamba na kuvaa nywele bandia.
✔Hawahubiri utakatifu katika makanisa yao.
✔Wanapenda kujiita majina makubwa makubwa.
✔Wanauza pafyumu, vitambaa na mafuta ya upako kwa ajili ya uponyaji.
✔Wanasema punyeto sio dhambi.
✔Wanasema mtu ukiokoka umeokoka moja kwa moja.
✔Hawahubiri juu ya unyakuo wa kanisa, ni mafanikio tu ya kimwili.
✔Bidii yao ni kutangaza miujiza yao ili watukuzwe wao.

Kama utaendelea kwenda kwenye makanisa ambayo viongozi wake ni waigizaji sio wachungaji;
🔹utaikosa mbingu wakati wa unyakuo wa kanisa.
🔹Hutaweza kuielewa biblia kwa ufasaha na kwa tafsiri halisi.
🔹Huwezi kuwa imara katika kristo.
🔹Huwezi kuwa na tofauti yeyote na mataifa(watu ambao hawajaokoka).
🔹Dhambi bado itaendelea kukutawala.
🔹huwezi kuwa na maandalizi yeyote ya kwenda mbinguni.
🔹utakuwa mtu wa kidunia kawaida tu na mbingu utaikosa.

JINSI YA KUFANYA:
✔Toka hapo..kimbia hapo si mahali salama kwa roho yako..
✔Nenda,

mahali wanapohubiri utakatifu wa mwili na roho kwa msisitizo.

mahali ambapo dhambi inakemewa kwa uwazi kabisa! Utakuwa salama na nafasi kubwa ya kunyakuliwa na kuingia mbinguni.

HASIRA YA MUNGU

UKITAKA KUIONA HASIRA YA MUNGU BAADA YA KUTOKA DUNIANI.

Ufunuo 14:10
Yakobo 1:20
Yeremia 7:20.

Kama unafanya haya  mpaka utakapo ondoka duniani bila kutubu, utaiona hasira ya Mungu.

Kama utaendelea kusujudu mbele ya sanamu yeyote ikiwamo ile wanayiita "bikira maria"

Mpe Talaka mke wako au mume wako.

Endelea kuvaa suruali mwanamke.

Kopa halafu kataa kulipa deni au kurudisha.

Acha kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

Kataa kusamehe wengine

Endelea tu na uasherati wako na usitubu.

Kazana tu kwenda kanisani na vimini vyako.

Endelea kuangalia picha na video ya ngono.

Endelea kumdanganya na kumuongopea mme/mke wako.

Mwanamke Acha kumtii Mume wako katika Bwana.

Endelea kupiga punyeto

Endelea kudanganya watu

Endelea kuchelewa kanisani kila ibada.

Tumia cheo chaka kuwanyanyasa na kuwakandamiza wengine wengine.

Endelea na wizi na ufisadi wako.

Endelea kupaka rangi midomoni na kwenye kucha.

Endelea kuvalia mapambo na kuweka nywele bandia

Endelea tu kujikweza na kujiinua na kuwaona wengine si kitu.

Endelea kufanya kazi  na vyeti feki vya wizi.

Endelea tu kufundisha mafundisho ya uongo.

Endelea kulipuuza neno la Mungu na kuacha kulitii.

Penda fedha kuliko Mungu.

Acha kuwaheshimu baba na mama yako ktika yalio sahihi mbele za Bwana.

YOTE HAPO JUU NI DHAMBI na mengine mengi pia yanatosha kabisa kumfanya Mungu akasirike juu yako.

kama unataka Mungu asikasirike juu yako  baada ya kuondoka duniani TUBU sasa.

Sababu inayomfanya Mungu asionyeshe hasira yake kwa wanadamu ni kwa sababu YESU aliununua muda huu kwa ajili yako na mimi ili atukomboe, ndio inayoitwa NEEMA Baada ya hapo hasira ya Mungu itafunuliwa kwa wanadamu.

Unao muda mwingi sana wa KUTUBU  ukiwa duniani baada ya hapa ni HUKUMU

Waebrania 9:27.

JINSI UNASHIRIKI DHAMBI KUPITIA MIZIKI YA KIDUNIA.

Mwanamuziki mmoja aitwae Rihana, aliimba DIAMOND IN THE SKY! lakini cha kushangaza huwezi kukuta almasi(diamond) Angani.

Alikuwa anamaanisha nini sasa anaposema DIAMOND in the sky??

BIBLIA katika EZEKIEL 28:13, inasema, "Ulikuwa ndani ya adeni bustani ya Mungu,kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako,akiki,na yakuti manjano,na ALMASI,na zabarajadi,na shohamu, na yaspi,na Yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari."

KIINGEREZA inasema, "You were in Eden, the garden of God;
Every precious stone was your covering:
The sardius, topaz, and DIAMOND,
Beryl, onyx, and jasper,
Sapphire, turquoise, and emerald with gold.
The workmanship of your timbrels and pipes
Was prepared for you on the day you were created.

Shetani ndio kiumbe pekee anaetajwa kuumbwa kwa Almasi(DIAMOND).

Shetani ndio almasi anaekaa au ambae makazi yake yako mbingu ya pili.

Kila anaeimba na kuzishabikia nyimbo kama hizi,
Amini usiamini kwa kinywa chako unamkiri shetani na kujiungamanisha nae na kwa namna hiyo KUZIMU inakusubiri.

MKRISTO NA MICHEZO YA COMPUTER

JE, NI SAHIHI MKRISTO KUCHEZA MICHEZO YA KWENYE KOMPYUTA(GAMES)

Kuna vitu ambavyo biblia haijavieleza  waziwazi kutokana na kutokuwepo nyakati hizo ambavyo leo vinaleta utata kwa watu mbalimbali ambao wanataka kila kitu wakione kwenye biblia kama kilivo kwa nyakati za leo.

Mtu mmoja ameniuliza swali leo kwamba Je, naweza kucheza michezo ya kwenye simu au computer(  video games)?? Nilimjibu lakini nikaona bora niliseme na hapa kwa faida ya wengi.

Jambo hili la kucheza michezo hii ya kwenye computer au simu huwezi kulikuta moja kwa moja kwenye biblia kama lilivyo ila tutaangalia misingi ya kibiblia ambayo bado inatumika pamoja na kwamba mambo haya hayakuepo nyakati hizo ila misingi hii inatupa kujua kwa upana zaidi juu ya jambo lolote tunalolifanya.

Mwenyewe nilikuwa mchezaji mzuri wa michezo hii kwenye simu na computer ila kwa neema ya Mungu nimeacha badala yake natumia muda huo sasa kumtumikia Mungu.

Kabla ya kuendelea ni muhimu kufahamu kuwa jambo lolote ambalo linatutoa kwenye upendo wetu wa kwanza katika kumpenda Mungu na kufanya mapenzi yake hatuna budi kuliangalia vizuri jambo hilo na kuliacha kabisa maana linaweza kuwa sanamu kwetu(mungu wetu).

Misingi inayotupa kujua na kujibu maswali yote yanayohusu kucheza michezo hii ya kompyuta, kuangalia filamu, ushabiki wa mipira nakadhalika.

1.JE, MICHEZO HII INAKUJENGA AU INAKUBURUDISHA?

Jiulize michezo hii itakufanya uongoze upendo wako kwa Mungu? Au maarifa yeyote ya Mungu na kuwafundisha wengine? Maandiko yanasema 'vitu vyote ni halali lakini si vyote vifaavyo (1wakorintho 10:23-24) (Warumi 14:19).
Mungu anapotupa muda wa kupumzika ,tutafute vitu vinavompa Mungu utukufu (wagalatia5:13-17).

2.JE, MICHEZO HII INATIMIZA MATAKWA YAKO AU YA MUNGU?

Mapenzi ya Mungu yanajumuishwa katika Amri kuu ya "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wote, akili zako zote na nguvu zako zote" (Luka 10:27). Kusudi la Mungu kwa mwanadamu linafunikwa na dhambi na Yesu ametuokoa na sasa hatufanywi matakwa yetu wenyewe ila Matakwa ya Kristo (Wafilipi 3:7-9). Lazima mapenzi ya Mungu yawe juu ya mapenzi yetu (Zaburi 143:10 ) (zaburi 40:8a), (waebrania 13:21).

3.JE,MICHEZO HII INAMTUKUZA MUNGU?

Mingi ya michezo hii inatukuza vurugu, uasherati, uonevu, wizi, ujambazi, n.k. kama wakristo Vitu tunavofanya lazima vilete utukufu kwa Mungu (1wakorintho 10:31) na vinatusaidia kukua katika maarifa na neema Ya kristo.

4.JE,MICHEZO HII INATUPELEKA KUFANYA MATENDO MEMA?

"Maana tu kazi yake,tuliumbwa katika Kristo Yesu,tutende matendo mema,ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza  ili tuenende nayo". Michezo hii haitupeleki kutenda matendo mema ambayo Mungu anakusudia kwetu.

5.JE,MICHEZO HII INAKUPELEKA/KUKUFANYA KUWA MTUMWA?

Watu wengi michezo hii inawafanya kuwa watumwa hasa(addicted).Mambo haya hayana nafasi katika ukristo. Paulo mtume anasema michezo yetu iwe ya rohoni na anaifananisha kama mwana riadha ambae anajizuia katika mambo mengi kama kulewa ovyo, kutembea ovyo n.k ili ajiweke afya yake kuwa vizuri kwa ajili ya kupata tuzo. Maisha ya mkristo ni hivohivo pia unapaswa kujizuia katika mambo menhi ili upate uzima wa milele na tuzo isioharibika. (1Wakorintho 9:25-27).

6.JE, MICHEZO INAKUFANYA UUKOMBOE WAKATI?

Kumbuka utatoa hesabu juu ya ulivotumia muda wako mfupi uliopewa na Mungu duniani. Kupoteza muda wa masaa kucheza michezo hii,kunakupotezea muda mwingi ambao ungeutumia kwa Bwana au kusoma neno.
Ishi kama mtu mwenye busara ukuukomboa wakati maana zamani hizi ni za uovu,yajue mapenzi ya Mungu ni yapi kwako.(Efeso 5:15-17, 1petro 4:2, kolosai 4:5, yakobo 4:14, 1petro 1:14-22).

7. JE, MICHEZO HII INAKUFANYA KUFIKIRI YA MUNGU AU YA KIDUNIA?

Wafilipi 4:8 "Hatimae ndugu zangu,mambo yote yalio ya kwel, yoyote yalio ya staha, yo yote yalio ya haki, yo yote yalio safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema;ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa njema, yatafakarini hayo."

8.JE, MICHEZO HII INAENDANA NA KUSUDI LA MUNGU KWAKO.

Paulo mtume aliandika ,siku za mwisho watu watakuwa wenye kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu (2Timotheo 3:4).

Utamaduni wa magharibi unatimiza haya maandiko maana watu  leo wanavutwa zaidi(kulevywa) na vitu vinavoitwa burudani kama vile filamu(series), mipira, miziki ya kidunia kuliko wanavyoweza kuvutwa na neno la Mungu.

Kama umeokoka na wewe unavutwa na vitu hivi huna tofauti na mataifa wafilipi 2:15. 3:7-10, 1yohana 2:15-17.

9.JE, MICHEZO HII ITAKUFANTA KUUTAZAMIA UZIMA WA MILELE.

Tunaishi tukiwa na tumaini la kupaya thawabu kutokana na kama tumeishi kwa kusudi la Mungu na kwa uaminifu duniani (mathayo 6:19-21), (1wakorintho 3:11-16)
Kama tunautazamia uzima wa milele ,tutatoa muda wetu na mioyo yetu kwa Bwana katika huduma (Wakolasai 3:1-2,23-24).

Vitu tunavovimiliki au tunavovifanya ambavyo vinatufaya tuukose uzima wa mileke na kutufanya upendo waetukupoa lazima tuwe tayari kuachana navyo (Luka 12:33-37).
Wengi wanajaribu kutimiza/kutumikia kotekote Mungu na matakwa yao Lakini Yesu alisema wazi kuwa hatuwezikuwatumikia mabwana wawili Mathayo 6:24.

Tunapopata muda wa kupumzika kama Yesu alivofanya (Marco 6:31),tuchague vitu vitakavyo tujenga na kumtukuza Mungu.

God bless you, prepare for eternity!

KIONGOZI KIPOFU

UKIONGOZWA NA KIPOFU WOTE MTATUMBUKIA SHIMONI(KUZIMU).

Usikubali kuongozwa na kiongozi kipofu kabisa maana anakuongoza kwenda shimoni(kuzimu).MATHAYO 15:14

Mchungaji anaetumia jina la Yesu kwa maslahi yake binafsi ni kipofu mkimbie utaangamia nae. Mchungaji ambae macho yake yote yako kwenye mfuko wako ni kipofu toka kwake, uiponye roho yako. Mchungaji anaekwambia unaweza kuvaa vyovyote hakuna shida, huyo ni kipofu anakupeleka motoni.

Mchungaji ambae hahubiri juu ya dhambi wala hakemei dhambi, mahubiri take yote ni mafanikio  ya kimwili tu, huyo ni kipofu,anakuongoza kwenda motoni.
Mchungaji ambae hakufundishi juu ya unyakuo Wa kanisa na kukuweka tayari kujiandaa kumlaki Bwana Yesu, hakupendi in kiongozi kipofu. Mchungaji ambae hata haamini wokovu duniani ni kipofu huyo anakuongoza kwenda motoni.

Mchungaji ambae hakiishi anachokifundisha ni kipofu utaangamia nae. Mchungaji anaekwambia jipambe tu hakuna shida,Mungu haangalii ndani ni kipofu Huyo wala hana mbingu yake ya kukupeleka, anakuongoza kwenda motoni.

Mchungaji ambae ni mpiga dili anakuuzia vitambaa,sabuni, maji na mafuta ya upako, ni kipofu mkubwa huyo anakupeleka upotevuni. Mchungaji ambae hahubiri juu ya jehanam ya moto,anahubiri mafundisho laini yadanganyayo ni kipofu usipokuwa makini utaangamia nae. Mahali ambapo uko guru pamoja na dhambi zako hapakufai mahali hapo, kimbia..

Acha kufanya mchezo na roho yako wokovu ni Mara moja tu ukiupoteza hakuna SECOND CHANCE  maana MTU amewekewa kufa Mara moja tu na baada ya kifo ni hukumu.WAEBRANIA 9:27

Mungu anasema tokeni kati yao mkatengwe nao, Mara moja ukigundua kiongozi,Mchungaji anaekuongoza ni kipofu toka haraka kimbia uiponye nafsi na roho yako 2WAKORINTHO 6:14-18.

#utii ni bora kuliko dhabihu.

MARANATHA.

Tuesday, January 16, 2018

JEHANAM YA MOTO.

JEHANAM YA MOTO.

Walioko jehanamu wanajua tayari wameshapotea,wanajua hawana nafasi ya kuokoka kama ulionayo wewe,wanaelewa kabisa bila kumkubali yesu na kuokolewa na kuishi maisha matakatifu kwa watu walioduniani nao wataenda huko waliko.

Utampokea yesu lini ndugu yangu? Muda umeisha sasa wewe unaesoma ujumbe huu na bado hujaokoka kwa kumaanisha.

Ukifa dhambini hata kama unasali kanisa la kiroho utaishia motoni, kwanini usiokoke leo rafiki!? Walioko motoni wanakumbuka nafasi walizozichezea wakiwa duniani kama vile ambavyo umekuwa ukipuuza injili na maonyo unayokutana nayo.

Umekutana na neno mara ngapi linalokuonya juu ya dhambi, hata humu facebook ni post ngapi ambazo zimekuwa zinakuonya juu ya dhambi na kukutaka uokoke na kumwamini yesu lakini unaishia ku LIKE na ku COMMENT 'amen' kumbe ni mwathirika wa dhambi na huchukui hatua yeyote.

Rafiki yangu ninakupenda sitaki upotee milele ndio maana nakueleza haya ,sitaki uje ujute na kuzikumbuka post hizi ukiwa motoni ambapo majuto hayatakuwa na msaada tena kwako.

sasa kama utanipuuza nitakuwa nimefanya sehemu yangu nimemaliza na kumbuka wakati uliokubalika ndio sasa,siku ya wokovu ndiyo sasa 2WAKORINTHO 6:2. Mungu yuko tayari kukupokea kama utamgeukia leo.

Wakati tulionao ni wakati wa hatari siku tusioidhani Bwana wetu anarudi kuwachukua watakatifu. je,utakuwa miongoni mwao? Dhamiri yako inakushuhudia.

Kumbe si wakati wa kufanya mchezo na dhambi ni wakati wa kutubu na kurekebisha njia zetu na kuzidi kuomba neema ya kumaliza safari kwa ushindi.

Neema ya kristo iwe nanyi nyote.

MADHARA NA HASARA ZA KUVAA WIGI.

MADHARA NA HASARA ZA KUVAA WIGI AU NYWELE BANDIA.

uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususan wakina dada  na wanawake wengi Wa kiafrika.

zifuatazo ni baadhi ya hasara au madhara kiroho  na kiafya ya uvaaji wigi na usukaji wa nywele za bandia..

1.KUTENGWA NA MUNGU MILELE.
Ukifa katika hali bado unavaa mawigi na nywele bandia zote ni unakwenda Jehanam ya moto moja kwa moja kwa sababu umeshindwa kumheshimu Mungu.

2.UNAKUWA UNAABUDU MIUNGU BILA KUJUA.
Asili ya mawigi haya yanayotokana na nywele za wahindi, ni miungu inayoabudiwa huko na miungu hio inatolewa sadaka za nywele na hatimae mawigi yanatengenezwa,sasa unaevaa vitu vilivotolewa sadaka kwa sanamu moja kwa moja unashiriki ibada za miungu.

3.UNAPOTEZA MUDA NA FEDHA.
Wengi wanaovaa mawigi wanahitaji kuwa nayo mengi ili kubadilisha lakini pia wale wanayafumia kichwani kabisa ni gharama sana kufanya hivo.Okoa fedha zako acha kuwaa mawigi mwanamke.

4.MAUMIVU YA KICHWA.
kutokana na kuvalia mawigi wengi wanakuwa na maumivu ya kichwa kwa sababu ya kubanwa sana kichwani na mawigi.kichwa hakipumui wakati wote kimefunikwa na helmet yako(wigi lako)

5.KUPATA MBA NA HARUFU MBAYA.
Mba zinakuja kwa sababu ya kichwa  kukosa hewa ya kutosha kitaalam inajulikana kama scalp hypixia ambayo inaweza kuleta harufu mbaya sana kama mba hizo zitachanganyikana na jasho.

6.UNAWEZA KUPATA MZIO(ALLERGY) NA KUNYONYOKA NYWELE.
wigi linakuwa na chemikali ambayo zinaweza kukusababishia madhara kwako kama hazitaoana na mwili wako. Na nywele pia zinaweza kuanza kunyonyoka na kichwa kuwasha sana.

Madhara hayo yote unaweza kuyapata wewe mwanamke unaeendelea kung'ang'ania mawigi yako ila mbaya zaidi ni Kutengwa na MUNGU Milele na kutupwa Jehanam ya Moto.

Mungu alikuumba,tayari aliona unapendeza na lazima tuishi katika viwango vya Adam na Hawa ambao Mungu alipowaumba akasema "na Tazama ni chema mbele zake", wanapendeza hivo hivo walivyo bila kuongeza makorokoro yoyote.

USIDANGANYIKE WIGI NI HATARI KWA MWILI NA ROHO YAKO. CHUKUA HATUA,UWE SALAMA.

#Jesus is #coming soon.

Na Isaiah Membe.

UZURI BANDIA

UZURI/UREMBO BANDIA, UTAKUPELEKA MOTONI.

UFUNUO 21:27 "Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilichokinyonge,wala yeye afanyae machukizo na uongo,bali wale walioandikwa katika katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo".

Andiko hilo kwa kiingereza,NIV linasomeka hivi , "Nothing impure will ever enter it, nor will anyone who does what is shameful or deceitful, but only those whose names are written in the Lamb’s book of life"

Yeyote alie Mnyonge [impure] na anafanya machukizo [Abomination/shameful] na ni mdanganyifu/mwongo [deceitful/false] hana sehemu katika UZIMA wa milele.

Kwa msingi huo sasa yeyote anaetumia;
NYWELE BANDIA [FALSE HAIR]
KUCHA BANDIA [FALSE NAILS]
LIPS BANDIA [FALSE LIPS]
NYUSI BANDIA [FALSE EYELASHES]
USO BANDIA [FALSE FACE/MAKE UPS]
UZURI BANDIA [FALSE BEAUTY].

Wote hawa wanafanya machukizo na Uongo na hawana sehemu katika  uzima wa milele.

UFUNUO 21:8, Waongo wote (all lairs/false) seheme yao ni katika lile  ziwa la Moto na kiberiti.

Wanawake wengi wanakwenda motoni kwa sababu ya mambo haya au yanayofanana na haya.

Njia ile ni Nyembamba, wanaiendea ni wachache na ni wale wasio na machanganyo yeyote wala hawafanyi machukizo yeyote yale. Ni watakatifu(holy and pure) katika njia zao zote.

Huu ni wakati wa kutubu na kuacha mambo yote ya uongo(false/fake) ya ibilisi na kumaanisha kukaa kwenye kweli(neno la Mungu) kwa gharama yeyote.

Amua moja Kutubu au upotee milele,

#Yesu anakuja kulitwaa #kanisa takatifu lisilo na #doa wala #waa wala #kunyanzi.

Na. Isaiah Membe.

ITAFUTE KWELI, USIFATE UMATI

USIFATE UMATI WA WATU, ITAFUTE KWELI YA NENO.

Yesu alisema wazi kabisa kuwa njia inayoenda uzimani ni nyembamba sana, tena imesonga na zaidi ni wachache wanaoiona na wanaopita njia hio. lakini pia wengi watajitahidi kuingia kwenye njia hio wasiweze.(Mathayo 7:13-14).

Kinyume chake, Njia ni PANA sana, hakuna kubanana, kuna uhuru mwingi na WENGI wanaenda katika njia hio ambayo inaenda UPOTEVUNI kwa shetani.

KATIKA NJIA PANA
#Kuna uhuru wa kufanya lolote unalotaka kufanya bila kujali biblia inasema nini

#kuna mafundisho laini yadanganyayo,yanayofundishwa na wachungaji ambao nao wako katika njia pana vilevile.

#hakuna kukemewa kwa dhambi na uovu, wanaangalia pesa yako tu basi.

#Injili ya kweli ya utakatifu haihubiriwi katu, ni mafanikio tu ya kimwili ambayo shetani anajua watayaacha yote hapo na kwenda Moja kwa moja motoni.

#Watu wanavaa wanavyotaka kwa mafundisho kuwa Mungu haangalii mambo ya nje anaangalia roho.Mavazi ya hovyo sana yaruhusiwa kanisani bila shida.

#Watu wanaambiwa wako huru ndani ya Yesu kwa hio hakuna shida hata wakivaa wanavyotaka, wakijipamba wanavyotaka.wanafarijiwa wanaenda mbinguni hali wako katika njia PANA.

#Kuna watu vuguvugu ambao hawana nafasi katika uzima wa milele maana watatapikwa na Bwana Yesu watoke katika kinywa chake.

Kwa sababu hio ni UMATI mkubwa wa watu leo wako katika njia pana.

KUPITA njia nyembamba ni gharama, inahitaji kweli kujikana nafsi, kuwa tayari kuacha yote ya dunia, na kuuchukua msalaba wako na kumfata Yesu kwa kila neno.(Luka 9:23-26, Luka 14:25-33, Mathayo 10:27-29).

injili ya Kweli ni ngumu sana, maana wapo wanaohubiri kweli ila sio kweli yote(Zaburi 119:6). haitakuwa rahisi kupita katika
njia hii bila kweli kudhamiria.

#hesabu gharama kabla hujajenga mnara. Itafutwe kweli ya neno itakayokupeleka mbinguni sio umati wa watu kwa mitume na manabii ambako utaishia Jehanam ya moto.

YESU ANARUDI, SAA YA MAAMUZI NI SASA.

Na Isaiah Membe.

MAVAZI NA MTAZAMO WA KIKAHABA

MAVAZI NA MTAZAMO WA KIKAHABA.

MWANZO 38:15 ,"YUDA ALIPOMWONA ALIMDHANIA YA KUWA NI KAHABA...".

Mbinguni unaweza kusajiliwa wewe ni kahaba kwa sababu ya uvaaji wako tu wala haiitaji kuwa unafanya uzinzi au uasherati au kuuza mwili wako kabisa, LAKINI bado mbinguni utahesabika wewe ni kahaba na jina lako kuondolewa katika kitabu cha uzima kutokana tu na mavazi yako.

kwa hakika! Unaweza kuwa bikira kabisa lakini mbinguni unaonekana wewe ni kahaba, hii inatokeaje? inatokea kutokana na kile unachokivaa.

kama mwanamke unavaa mavazi yanayoacha uchi wako wazi, mavazi mafupi(vimini)ambayo yanaacha mapaja yako wazi kabisa, mavazi yanayoacha matiti yako wazi kwa namna yeyote, mavazi yanayoacha tumbo, mgongo na makwapa wazi.

Unapovaa mavazi kama hayo, mbele za Mungu unaonekana kama kahaba.

vilevile umapovaa mavazi yanayokubana mwili ili kuchora maungo na maumbile yako vizuri na kuwaonyesha watu waone maumbile yako,mavazi ambayo ukikaa hayafuniki magoti, Mbele za Mungu wewe ni kama kahaba..

Inaweza ikawa ni ngumu kwako kulipokea neno hili,LAKINI NDIO VIWANGO VYA UTAKATIFU VYA WATU WANAOWAZA KUINGIA MBINGUNI.

Unaweza kuwa mchungaji, mhubiri, mwimbaji au yeyote yule umaeweza kuwa, lakini kwa Mungu ukaonekana wewe ni kahaba mwenye heshima kwa wanadamu.

kama ni ngumu sana wewe kuliamini neno hili unaweza kusubiri wakati ule katika geti la mbingini watakapobaguliwa kondoo na mbuzi,ambapo utakuwa tayari umeshachelewa na SITAKUSHAURI kusubir wakati huo.

Kutakuwa na mshangao mkubwa siku ile ya unyakuo lakini pia siku ile ya hukumu ya aibu na kudharauliwa milele, watu watasema Bwana mimi sikuwahi kuwa Kahaba hata siku moja.

Na kama mwanamke wa Kikristo hio ndio itakuwa sababu yako mbele za Mungu kwa kuvaa mavazi yanaacha uchi wako wazi? utajiteteaje kwa mavazi yaliokuwa yanakubana mwili wako, mavazzi yaliokuwa yanaonyesha nguo zako za ndani, utajiteteaje kwa vimini na suruali unazozivaa?

MWANZO 38:21,"AKAULIZA WATU WA MAHALI PALE,AKISEMA YUKO WAPI YULE KAHABA ALIEKUWAPO ENAIMU KANDO YA NJIA? WAKASEMA HAKUWAKO HAPA KAHABA.

wengi wanafikiri kahaba ni yule anaesimama kando ya barabara akisubiri wanaume. KAHABA ni mwanamke yeyote ambaye anaefanya uzinifu na mwanaume kwa ajili ya kupata kitu fulani, hata kama haonekani hadharani..

kama wewe mwanamke ,ulifanya ngono au mapenzi ili kupata kazi unayoifanya,mbele za Mungu wewe ni kahaba hata kama ni mara moja tu.

kama wewe mwanamke ulimruhusu mwanaume kulala na wewe ili upandishwe cheo kazini, urudishwe kazini, uingie mkataba au kwa ajili ya masomo yako(ufaulu mitihani,upate cheti n.k) Mbinguni wewe unatambulika kama kahaba(prostitute) bila kujali ni mara moja au mara nyingi!!!

UKWELI HUU HAPA⤵

Chochote unachokipata au ulivyovipata kwa wewe kulala na mwanaume,hata kama vitu hivi ilikuwa ni haki yako lakini kwa sababu uliruhusu mwanaume kulala na wewe kabla ya kuvipata, Mbinguni unahesabika kama kahaba:- kazi, vyeti na faida unayoipata ni matokeo ya ukahaba wako hata mshahara unaoupata kutokana na ukahaba unaitwa ni mshahara wa kahaba.

JAMBO KUBWA NI KUWA.

Kama unatoa fungu la kumi au sadaka kutokana na ukahaba wako,unajitafutia hukumu kubwa mbele za Mungu katika maisha yako Kwa sababu MUNGU ameonya kuwa mshahara wa kahaba kamwe usiletwe katika Nyumba yake(MUNGU).

Hili hapa neno la Mungu katika;-

KUMBUKUMBU 23:17-18 "PASIWE NA KAHABA KATIKA BINTI ZA ISRAEL, WALA PASIWE NA HANITHI KATIKA WANA WA ISRAEL WANAUME. USILETE UJIRA WA KAHABA, WALA MSHAHARA WA MBWA, KATIKA NYUMBA YA BWANA MUNGU WAKO,KWA AJILI YA NADHIRI YEYOTE; KWANI HAYA NI MACHUKIZO KWA BWANA MUNGU WAKO,YOTE MAWILI.

Mchungaji anaepokea zaka na sadaka zako na hata anaweza kusema mtu yeyote tu anaweza kuleta zaka na sadaka kwa sababu yuko hapo kwa sababu ya pesa zako na wewe ukadanganyika.

Ili upate rehema za Mungu  unatakiwa kutubu toba ya dhati na kweli na Ufanye malipizo yanayoambatana na kutubu kwako.

Na. Isaiah Membe, Mtumwa wa Kristo.

WAKATI WATAKAPOYAKAA MAFUNDISHO YA UZIMA

UTAKUJA WAKATI WATAKAPOYAKATAA MAFUNDISHO YA UZIMA.

YESU alihubiri injili ya kweli, akasulibiwa.
STEPHANO alihubiri injili ya kweli, akapigwa mawe hadi kufa.

MITUME walihubiri injili ya kweli, wengine walichemshwa kwenye mafuta wangali hai,wengine walikatwa vichwa vyao, wengine walisulibiwa msalabani  kichwa chini miguu juu, wengine walifungwa na kuburutwa barabarani n.k.

LAKINI leo Mchungaji,Padri,Askofu, Mtume au Nabii wako, ANAHUBIRI NA KUFUNDISHA KINYUME KABISA NA NENO LA MUNGU(UONGO), Mnashangilia na kupiga miruzi, NANI ANAMDANGANYA NANI???

NENO linasema,
2Timotheo 4:3-4," maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wanamaskio ya utafiti; Nao watajiepusha wasisikie yalio kweli, na kuzigeukia hadithi za Uongo."

Pia 2Timotheo 3:1-9, 2Petro 2:1-3, Yeremia 23:1-10.

wachungaji ambao ni maajenti wa ibilisi wanaopenda pesa kuliko Roho za watu.

Na Isaiah Membe, Mtumwa wa Kristo.

WOKOVU NI BADILIKO LA WAZI

MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA, YA KALE YOTE YAMEPITA.

"Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya” (2Wakorintho 5:17)

“Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye KATIKA YEYE TUNA UKOMBOZI YAANI, MSAMAHA WA DHAMBI”.(Wakolosai 1:13,14).

Kumbuka;

(Warumi 8:1-2 )
"Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti."

Yohana 3:18
"Amwaminiye yeye (YESU KRISTO) hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu."

"Amwaminiye Mwana (YESU KRISTO ) yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia." (Yohana 3:36)

Unaweza kusema me tayari nimeshaokoka lakini kumbuka na kuzingatia hili, utakatifu/ukamilifu ni mwili na roho. (2wakorintho 7:1, 1wathesalonike 5:23, 1petro 1:15, Mathayo 5:48, Waebrania 12:14). Utakatifu ni pamoja na tabia zetu za nje, yaani miili yetu katika mavazi, mienendo,Maneno na usemi wetu n.k, Lazima tukae kwa haki bila lawama wala kulaumiwa katika roho na mwili..

Jihoji mwenyewe, je wewe ni mtakatifu wa mwili na roho??Majibu  dhamiri yako inasema wazi, kwa sababu maisha yako unayajua jinsi ambavyo hayana ushuhuda kwa waliokuzunguka kutokana na unavovaa, unavoongea, unavyoishi na watu, pamoja na kusema umeokoka.

Ni uamuzi wako!

Maandiko yanasema kuwa;

"Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako" (Matendo 16:31)

Yesu anabadilisha kabisa maisha ya mtu, inabaki historia na ushuhuda wa wazi kabisa unaonekana kwa wale wanaokufahamu. Kubali Yesu akubadilishe leo.

"Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka" (Warumi 10:9)

Ikiwa unasikia sauti ya MUNGU ndani ya moyo wako ikikuambia unahitaji kubadilika na kumpokeaYESU KRISTO basi kwa kinywa chako na kwa imani fuatusha maneno  haya;

"BWANA YESU,HAKIKA MIMI NI MWENYE DHAMBI, SIJAWA MTAKATIFU WA MWILI NA ROHO.
BWANA YESU NISAFISHE MOYO WANGU KWA DAMU YAKO, NIPE UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI ZOTE NA KUNIWEZESHA KUISHI MAISHA YANAYOKUPENDEZA WEWE. JINA LANGU LIFUTE KWENYE VITABU VYA HUKUMU NA ULIANDIKE UPYA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE. NAJITOA KWAKO KUANZIA LEO UWE BWANA NA MWOKOZI WANGU, NIFANYE KUWA KIUMBE KIPYA SASA.AMEN."

Kama umetamka kwa imanina kudhamiria ndani yako, hakika Bwana amekusamehe. Lakini utahitaji msaada zaidi ili uendelee kudumu katika mafundisho ya usafi na utakatifu.

Kwa msaada zaidi wewe ambae unadhamiria kweli kuwa mtakatifu na kumuona Mungu, tafuta kanisa linalohubiri na kuzingatia utakatifu wa mwili na roho au waweza kunitafuta ili tuendelee kujifunza na kupata maelekezo mengine zaidi..

namba: 0764569023.

Isaya Membe, ndugu yako katika Kristo.

WALEVI WOTE SEHEMU YAO NI KATIKA ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI

ACHA POMBE, WALEVI WOTE HAWAURITHI UFALME WA MUNGU.

MITHALI 23:20, WALAWI 10:9.

Neno la Mungu linasema waziwazi kuwa tusiwe miongoni mwao wanywao pombe,inazungumzia kunywa sio suala la kulewa tu.

Mtu awae yeyote anaesema kuwa tunaruhusiwa kunywa kidogo ilimradi tusilewe ni sawa na kusema tunaruhusiwa kufanya uzinzi kidogo,hakuna tofauti yeyote.

Yako maandiko kadha wa kadha ambayo watu wanayatumia kuhalalisha unywaji wa pombe na wengine wanajiita ni wachungaji, wainjilisti, maaskofu, mapadri, mitume na manabii lakini kwa bidii wanafundisha hivo kuwa kunywa pombe hakuna shida yeyote.

Yako maandiko katika biblia zetu ambayo yanaonekana kuwa na utata kuhusu suala la kunywa pombe. Moja ya maandiko hayo ni haya yafuatayo;

Kumbukumbu 14:26, Mhubiri 9:7, Mwanzo 27:28 na mengine ambayo tutayaona mbele.

Tuone basi hayo maandiko yanamaana gani?

Ni muhimu sana kufahamu kuwa biblia zetu zimetafsiriwa kutoka katika lugha mbili kiebrania na kiyunani. Lugha hizi mbili ni lugha ambao msamiati wake ni mpana sana tofauti kwa mbali na kiswahili chetu.

Hivyo kama wanafunzi wa biblia hatuna budi kutafuta maana halisi ya maneno yaliotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili kutoka katika lugha hizi.

Katika kiebrania kwa mfano kuna maneno kumi ambayo yote katika kiswahili yanatafsiriwa kiholelaholela divai, mvinyo bila hasa kuzingatia uzito na maana halisi ya neno hilo katika Lugha ya asili.kwa ufupi maneno haya ni kama ifuatavyo;

1.TIYROSH(tee-roshe)
Hili neno katika kiebrania ni juisi iliokamuliwa kutoka kwenye zabibu ambayo haijachachuka. Katika biblia zetu kuna mahali wamejitahidi kueleza vizuri kwa kutumia neno DIVAI MPYA (mithali 3:10, ISAYA 65:8). Mahali popote Inapotajwa zaka za divai ni hii divai mpya(tiyrosh) inayozungumziwa, mfano katika( KUMBUKUMBU 14:23, WAAMUZI 9:13,NEHEMIA 5:11,N.K).

2.YAYIN
Yayin ni neno lingine ambalo katika kiebrania ni neno la jumla linalojumuisha divai iliochachuka na  ile ambayo haijachachuka. Kwa mfana katika haya maandiko neno linalotumika hapo ni Yayin. (MWANZO14:18, 19:32-35,KUTOKA 29:40, MWANZO 27:25,37. MWANZO 49:11, KUMBU 14:26).

3.SHEKAR
Hili neno katika kiebrania ni kileo ambacho hakitokani na zabibu, kinatokana na mchanganyiko wa mmea wa shayir, asali na tende. Kuna maandiko  Katika biblia zetu panatumika neno KILEO CHENYE NGUVU au STRONG DRINK kwa kiingereza lakini kwa sehemu kubwa linatumika neno kileo. Kwa mfano katika haya maandiko neno linalotumika ni shekar.(HESABU 6:3, 28:7, WALAWI 10:9, WAAMUZI 13:4,7,14, ISAYA 5:11,22, 24:9, 28:7,29:9,ZAB 69:12 n.k).haya yote kuna ole na katazo katika kutumia kileo sawasawa na maana halisi ya neno lenyewe maana shekar ni pombe halisi.

4. MAMSAK
Hii ni divai iliochachuka, ikaongezwa maji na kuchanganywa na viungo vingine mbalimbali.( MITHALI 23:30, ISAYA 65:11).

Yako maneno mengine kama, CHEMER, CHAMAR, GATH,YEQEB,ASIY ambayo yanaeleza namna mbali mbali ya vinywaji vitokanavyo na zabibu.

Kwa hio Katika kutoa tafsiri yeyote ya maandiko ni muhimu sana kujua katika Lugha ya asili ni neno lipi limetumika hapo na linamaanisha nini.

Wako watu wengine wanasema Yesu alitengeneza pombe katika arusi ya kana ya galilaya, wanatumia andiko la YOHANA 2:9-10. Je ni kweli Yesu alitengeneza pombe, jibu ni hapana, ufunguo wa hilo andiko tunaupata katika mstari wa 11, unasema,
"11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Yohana 2 :11.

Maandiko yanasema Yesu aliudhihirisha utukufu wake baada ya kufanya muujiza huo mkubwa wa kubadili maji kuwa divai njema.

Kulikuwa na mambo mawili katika nyakati za biblia kufanya jambo la kuudhirisha utukufu wa Mungu au Aibu. Angalia kwa mfano katika HABAKUK 2:15-16 "15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Habakuki 2 :15

16 Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.
Habakuki 2 :16.

Kama Yesu alifanya vile akaudhihirisha utukufu wake wala sio aibu, ni dhahiri kabisa haikuwa pombe. Yesu kamwe hakutengeneza pombe.

Andiko lingine ni 1TIMOTHEO 5:23, Ambalo wanalitumia kusema tunywe pombe kidogo.

"23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara"
1 Timotheo 5 :23

Kinachotajwa hapo ni mvinyo kama dawa ya tumbo, ni tofauti na leo watu hawaendi kunywa gongo, kangara, pombe yeyote kwa sababu wanaumwa wanataka dawa.

Nyakati za biblia hakukuwa na visima vingi virefu vya kupata maji safi kiasi kwamba vile vilivokuwepo vilirithiwa kizazi hadi kizazi na kutunzwa ili visiharibiwe (YOH 4:12)

"12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
Yohana 4 :12.

Wengine walilazimika kwenda umbali mrefu kupata hayo maji masafi, wengine vijana wakawa wanawavizia watu wanaotoka kuchota maji na kuwaibia, kwa hio wizi wa maji ulikuwa wa kawaida MITHALI 9:17 "

Wengi sasa walilazimika kuchimba visima vyao vya karibu lakini maji yake yalikuwa machafu na yakawa yanawasababishia magonjwa ya tumbo, akiwemo timotheo.

Katika Andiko hilo sasa paulo Mtume anamweleza  timotheo atumie mvinyo,dawa sio anywe pombe kidogo asilewe.

Nyakati za biblia uko  mvinyo uliotumika kama dawa, tunaliona hili katika LUKA 10: 30-37 "30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang'anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.
Luka 10 :30

31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
Luka 10 :31

32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.
Luka 10 :32

33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,
Luka 10 :33

34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
Luka 10 :34

35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
Luka 10 :35

36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang'anyi?
Luka 10 :36

37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.
Luka 10 :37.

Hata kama hatuelewi sana maandiko lakini tunaweza kujua kitu hiki ni dhambi kwa kuangalia kanuni tu. Tunafundishwa kanuni katika MATHAYO 7:17-18 17 "Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
Mathayo 7 :17

18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
Mathayo 7 :18.

Kwa msingi huo sasa pombe ni kitu kiovu,sio mti mzuri tunapoangalia matokeo ya ulevi. Kwa mfano angalia baadhi ya matokeo ya ulevi

MWANZO 9:20-21.
MWANZO 19:30-36.

WALEVI WOTE HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU , Huyo Padri, Mchungaji, askofu, mtume, nabii, anaekwambia kuwa unaweza kunywa pombe tu hamna shida,HANA MBINGU ,sikiliza neno hili,ACHA POMBE UTUBU LEO,WALEVI HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU KAMWE

9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
1 Wakorintho 6 :9

10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
1 Wakorintho 6 :10.

Yesu Anarudi, Rekebisha njia zako.

Na Isaiah Membe.

SHIKA SANA NENO SIO DINI.

SHIKA SANA NENO SIO DINI.

Mpendwa, ikiwa tunataka kuingia mbinguni hatuna budi kukishika Neno la Mungu, sio dini.

Biblia inasema katika
ZABURI 119:9.
"Jinsi gani kijana aisafishe njia yake ,ya kwenda mbinguni ni kwa kutii ,akilifuata neno lako". Biblia hapa haisemi kwa kutii, akiifuata dini yake, bali Neno la Mungu".

Kumbuka kwamba mtu anapokufa hataulizwa alikuwa dini gani, kitakachoangaliwa ni Je alikuwa  MTAKATIFU, Ambao pasipo huo utakatifu haitawezekana kwa namna yeyote kumuona Mungu. WAEBRANIA 12:14.

Kulishika Neno la Mungu ndio kumshika YESU, maana Yesu  anaitwa neno la Mungu UFUNUO 19:13.

Dini haiwezi kumpa mtu uwezo wa kushinda dhambi, ni YESU tu Ndie mwenye uwezo Huo.

Ndio maana watu wengi ambao ni
makahaba, majambazi, Walevi
Wavuta bangi, Watukanaji, Washirikina, Bado wanadini zao pia na wana majina ya kidini kabisa lakini dini zao hazijawasaidia au kuwawezesha kushinda dhambi, bado wamekuwa watumwa wa dhambi pamoja na kwenda kanisani jumapili.

NJIA NI MOJA TU, NJIA NI YESU KRISTO HAKUNA KWENDA KUSHOTO AU KULIA, anasema katika:-

YOHANA 14:6,
"Mimi ndimi njia na kweli na uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi(Yesu)".

Mpendwa najua una dini yako Unayoipenda lakini jihoji mwenyewe Moyoni mwako na uwe mkweli je, maana dhamiri ni mkalimani mzuri wa maisha Yetu, jiulize je, una uwezo wa kushinda dhambi? Dhamiri yako inazungumza kwa sababu maisha yako unayajua ni maisha yakiojaa dhambi pamoja na kusema una dini,
HUNA tofauti yeyote na mpagani maana mpagani analewa pombe na wewe unalewa pombe, mpagani anavuta sigara na wewe unavus sigara, mpagani anacheza dansi na wewe unaejiita Mkristo unacheza dansi, tofauti yake na wewe ni nini?

kama Unajigundua kabisa bado ni mwenye dhambi na hauna uwezo wa kushinda dhambi, nafasi bado ipo ya kurekebisha njia zako,

ANZA UPYA LEO, SEMA YATOSHA MAISHA YA DHAMBI, na sasa unachotakiwa kufanya ni kumkimbilia Yesu na kumwambia  Akusamehe kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha (MITHALI 28:13) na umwambie Yesu leo akupe uwezo kushinda dhambi zote(YOHANA 1:12) Nawe utaokoka maana ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako, UTAOKOKA( WARUMI 10:9-10).

Ubarikiwe sana.

Na Isaiah Membe, Mtumwa wa Kristo.

WEWE NI NANI KUBADILI SURA NA MFANO WA MUNGU????


MWANADAMU NI NANI KUBADILI SURA NA MFANO WA MUNGU.

Mwanadamu ni nani amjibuye Mungu???

Warumi 9:20 
"20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba kwanini kuniumba hivi?
Hamjui ya kuwa mwili ni hekalu la Mungu? 

chochote unachokifanya, kwa huo mwili Mungu anakuangalia....Sasa sikia hili, Mungu ni Roho na palipo Roho wa Bwana kuna  uhuru.
Kama unasema una huyo Roho wa Mungu, UTAKAA MBALI NA  DHAMBI.

Na Isaiah Membe, mtumwa wa Kristo!

JIFUNZE KATIKA NDOA YA KWANZA!


JIFUNZE KATIKA NDOA YA KWANZA.

Tunajifunza katika kitabu cha Mwanzo, kuhusu ndoa ya kwanza kabisa kuwapo Duniani ambayo ni ndoa ya Adamu na Hawa.

MWANZO 2:15-18, 21-24.
Mungu kabla ya kufanya kitu anakuwa anaandaa mazingira kwanza kabla. 

Mfano;

1. Aliumba Maji kwanza kabla ya samaki.

2. Aliumba Ardhi kabla ya Mimea.

3. Alitengeneza bustani kabla ya Mwanadamu.

Vile vile kabla Mungu hajampa Adamu mwanamke, viko vitu ambavyo vilitangulia kwanza.Tuangalie vitu hivi kwa muhtasari.

✴Kitu cha kwanza Mungu alichokifanya kwa Adamu(mwanaume), Alimuweka katika Bustani ya Edeni. Neno Eden katika lugha ya Asili inamaana pana sana, Edeni inazungumzia uwepo wa Mungu.
 
Mwanaume anahitaji kuwa katika UWEPO WA MUNGU kwanza kabla ya Kuoa. wengine wanauacha uwepo wa Mungu wanaenda kutafuta mwanamke. Mwanamke anatakiwa akukute ukiwa tayari katika Uwepo wa Mungu. TULIA KWENYE UWEPO WA MUNGU.

✴Kitu cha Pili Mungu alichompa Mwanaume ni KAZI.

MWANZO 2:15.Mungu akamwambia Adamu ailime bustani na kuitunza. Vivyo hivyo MWANAUME anahitaji au anatakiwa kuwa na KAZI kwanza kabla ya kuwa na mke.

✴Kitu kingine, Mungu akampa Adamu neno.

MWANZO 2:16, ambalo ndio likawa agizo la Mungu kwa Adamu ambalo alitakiwa alitii wakati wote. Mungu hakumpa mwanamke neno Kabla ya Adamu. 

Mwanaume unatakiwa kuwa unalifahamu Neno la Mungu na kulitunza Kabla ya Mungu kukupa Mke.

KATIKA "MWANZO 2:18", Mungu akasema, "BWANA MUNGU akasema si vyema HUYO mtu(Adamu) awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae"

Hatupaswi kupasoma hapo haraka haraka tu, Mungu anasema SI VYEMA HUYO MTU(MWANAUME) AWE PEKE YAKE, MWANAUME YUPI???

Ambae,

1. Yupo katika Uwepo wa Mungu.
2. Tayari ana Kazi na Anafanya kazi.
3. Tayari Analo Na kulifahamu Neno La Bwana.

Kwa hio kama Mtu hayupo katika Uwepo wa Bwana, hafanyi kazi,halijui neno na maagizo ya Mungu,NI VEMA HUYO MTU KUWA PEKE YAKE.

Na Isaiah Membe: Mtumwa wa Kristo.

KATAA UTASA WA KIROHO.


✴Mtu anapokosa mtoto anapokuwa katika ndoa yake huwa anaumia sana kiasi cha wengine kuiacha imani na kwenda kwa mitume na manabii kutafuta miujiza baada ya kuona wameomba sana hawapati majibu.Hii yote ni kwa sababu wana uchungu wa kupata watoto.

✴Wengine wanaenda mbali zaidi na kuamua kuishia kwa waganga wa kienyeji kwa sababu haipendezi kukaa bila mtoto katika ndoa,Haipendezi kuwa tasa katika mwili.Ni zaidi sana katika Roho.

✴Tunamuona Hana  kwenye biblia aliekuwa tasa iliamua kwenda masafa marefu sana katika maombi mazito ya kufunga na kumlilia Bwana  kwa ajili ya kupata kupata mtoto wa kimwili tu. 1SAMWELI 1:1-20. Hatuna budi vilevile kuwa hivo katika roho.

✴Vivyo hivyo katika Roho Kuna kuwa na utasa wa kiroho, una muda mrefu umeokolewa lakini hadi leo hujamzalia Bwana mtoto hata mmoja. Huna watu wa kuonyesha mbele za Bwana kama matunda ya kazi aliotupa Bwana MATHAYO 28:19. Maana tumeokolewa sisi ili kuwaleta wengine kwa Yesu.

✴Tusiridhike tu kukaa wenyewe hivohivo siku zote katika hali ya utasa, badala yake tuugue na kuhuzunika na kuwa na uchungu mioyoni mwetu, hata kumlilia Bwana ili atutoe katika utasa huo wa rohoni, Kwa maana tawi lisilo zaa litakatwa!!

✴Inapendeza sana kuwa na watoto wa kiroho ambao umewapata kwa kazi na tabu yako kwa msaada wa Bwana,Ambao watakuwa ni taji yako ya kujionea fahari.

DANIEL 12:3
"3 Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele."
Danieli 12 :3

Mwenye hekima huvuta roho za watu

©Isaiah Membe, Mtumwa wa Kristo.

TOBA NI KUMAANISHA KUACHA.

AFICHAE DHAMBI ZAKE HAWEZI KUPATA REHEMA KWA MUNGU.:

MITHALI 28:13

Watu wengi sana katika taratibu za madhehebu yao wanaungama kila  jumapili katika sala ya maungamo lakini ni kwa desturi na mazoea tu, Wala ndani yao hadhamirii kuacha dhambi. Watu wa jinsi hii hawawezi kupata rehema kwa Mungu wala maisha yao hayawezi kubadilika.

Wengine Watakuwa wanaenda wa kwa viongozi wa dini zao kuungama dhambi zao,Lakini watu hawa ni wanafiki kwa sababu utakuta wanaungama dhambi mbili tatu tu tena kwa desturi na mazoea tu.

MARCO 7:6-9.
"6 Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami;

7 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,

8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.

9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.

Ndio maana hakuna badiliko lolote lile la maisha yao baada ya hapo, kwa sababu hawana hata huo mpango wa kuacha dhambi. Anaungama ulevi ndani yake wala hana mpango wa kuacha ulevi n.K,  Huwezi kupata wokovu kwa staili hio hata kidogo.MITHALI 28:13.

Mungu  anasema, anaeungama dhambi na kuziacha huyo ndie atakaepata rehema tena tunatubu kwa Mungu moja kwa moja. WARUMI 10:9-10.

Tubu kwa kumaanisha kuacha, utapata rehema kwa Mungu itakayoambatana na uwezo wa kushinda dhambi zote. YOH 1:12.

Mwl. Isaiah Membe, mtumwa wa Kristo.

UKIOKOKA UMEOKOKA MOJA KWA MOJA(ONCE SAVED ALWAYS SAVED)


# HILI NI FUNDISHO_POTOFU
.

Moja kati ya mafundisho potofu ni lile la kusema kuwa mtu AKISHAOKOKA, ameokoka moja kwa moja, Na mbinguni ataingia tu bila kujali atafanya dhambi tena.

Hili fundisho pia limezaa fundisho lingine la kusema wakati huu wa neema TUKO HURU  ndani ya YESU ,tunaweza kufanya chochote MRADI tu tumeokoka.

Andiko moja wapo Wanalotumia ni YOHANA 10:28, "28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu."
Yohana 10 :28.

Sasa, JE, NI KWELI MTU AKIOKOKA AMEOKOKA MOJA KWA MOJA BILA KUJALI ATAFANYA NINI? 

JIBU NI HAPANA!!!

JIULIZE;
KWANINI YESU Alisema,WAITWAO ni wengi bali WATEULE ni wachache? { MATHAYO 22:14}.

KWANINI YESU alisema, Angalia Umekuwa mzima USITENDE DHAMBI TENA.{YOH 8:11}.

KWANINI YESU alisema, WAKWANZA watakuwa wa MWISHO? { MATHAYO 20:16}.

KWANINI BIBLIA Inasema , UTIMIZENI wokovu wenu kwa Kuogopa na kutetemeka.{WAFILIPI 2:12}.

KWANINI BIBLIA Inasema , mtu atakaeliharibu hekalu(mwili),Mungu atamuharibu mtu huyo {1WAKORINTHO 3:16}.

KWANINI YESU Alisema, HAKI yen isipozidi haki ya mafarisayo,HAMTAINGIA kamwe katika ufalme wa mbinguni.{ MATHAYO 5:20}.

KWANINI Maandiko yanasema kufanya dhambi baada ya kuokolewa ni kumsulubisha Mwana wa Adamu mara ya pili {EBRANIA 6:4-6}.

KWANINI biblia inasema tusafishe mwili roho na nafsi { 2Wakorintho 7:1}.

KWANINI YESU alisema, sio kila aniitae Bwana ataingia katika uzima {MAT 7:21-22}.

Kama Mchungaji wako,anakufundisha kuwa ukiokoka ndio basi umemaliza KILA kitu anakuandalia mazingira ya kukupeleka MOTONI, Maana yake atakuwa anakuhalalishia dhambi zote kwa kisingizio cha moyo Wako umebadilishwa basi mambo mengine hakuna shida.

Ni kweli YESU ameahidi uzima kwa wote waliookolewa, lakini lazima ufahamu HATA kama MUNGU ameahidi hivo,au Mungu akiweka Agano,Bado na wewe unasehemu ya kufanya ili kulikamilisha hilo Agano.

Waisrael katika safari yao ya kwenda kaanan, Lakini la kujiuliza ni kuwa je, Waisrael wote waliotoka MISRI walifika kaanani? Wote waliotamani mabaya na kwenda kinyume na maagizo ya Mungu waliangamizwa jangwani. Safari hii ni kielelezo cha safari Yetu ya Mbinguni.

YESU anasema Tuishi maisha matakatifu, tusiwasilikilize hao wanaotaka tusiishi maisha matakatifu katika mwili na roho.Yesu anasema wao wenyewe hawaingii hivo wasikuzuie na wewe usiingie.
1TIMOTHEO 4:1,
"1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
1 Timotheo 4 :1.
Hakikisha unakuwa Mteule baada ya kuitwa, WATEULE ni wale tu ambao baada ya kuitwa ,wanaendelea kumtii Mungu na kumfata kwa kila NeNo.

KATIKA YOHANA 10:28, Yesu anasema, "
28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
Yohana 10 :28.
Hii Ni ahadi ya Yesu Lakini imeambatana na masharti, YOH 10:27. Ili usipotee na kupokonywa mikononi mwake ni LAZIMA KUIKIA SAUTI YAKE(NENO LAKE) NA LAZIMA KUMFUATA, vinginevyo lazima utapotea.
USIKUBALI KUDANGANYIKA.

Na, Isaiah Membe, mtumwa wa Kristo.